Hongera TotalEnergies si tu kwa kuonyesha upendo, bali kuendeleza upendo. Wengi badala ya kuonyesha upendo, wanaonyeshea ili watu waone

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi,

Hii ni makala ya Jumapili ya leo.

Upendo wa Kweli-.png


Jumatatu ya wiki iliyopita, February 14, Watanzania tumejiunga na nchi nyingine duniani, kuadhimisha siku ya Wapendanao, yaani Valentine Day, ambayo huadhimishwa kwa watu kuonyeshana upendo na kupeana zawadi mbalimbali za kuonyesha upendo wakiwemo wapenzi kupeana maua na zawadi mbalimbali za kuashiria upendo, ila sasa kwa baadhi, Valentine sio tena kuonyesha upendo, bali kuonyeshea!

Kabla sijazama ndani ya makala hii kwa kuzungumzia upendo wa siku hii ya Valentine, naomba kuchukua fursa hii, kuipongeza Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies Tanzania, kwa kipindi cha miaka 5 mfulululizo, imekuwa ikiiadhimisha siku hii ya Valentine kwa kwa konyesha upendo wa kweli kwa kuwapa zawadi mbalimbali Watanzania, badala ya kuonyeshea. Pongezi hizi kwa TotalEnergies sio tuu ni kwa sababu inaadhimisha siku hii kwa kutoa zawadi mbalimbali, bali Valentine kwa TotalEnergies sio maadhimisho ya siku moja, kama Valentine inavyoadhimishwa tarehe 14 February tuu, bali Valentine kwa TotalEnergies ni msimu na inaadhimishwa kwa siku 14 mfulululizo!

Hivi ninavyoandika hapa leo, japo Valentine yenyewe imeadhimishwa siku ya February 14, na baada ya siku hiyo, maisha yanaendelea, kwa TotalEnergies, maadhimisho yanaendelea na kutoa zawadi za Valentine hadi Tarehe 27 ya mwezi huu. Ukienda kituo chochote cha TotalEnergies kuweka mafuta, au kununua chochote katika maduka ya Bonjour yaliyopo kwenye kila kituo cha TotalEnergies, lazima utaondoka na zawadi yako ya upendo.

Sasa turudi kwenye maana halisi ya Valentine, kama nilivyoeleza ni sikukuu ya kuonyesha upendo halisi wa kweli wa kutoka moyoni, na sio kuonyeshea upendo ili watu waone kuwa unapenda!.. Kuna tofauti kati ya kuonyesha upendo, na kuonyeshea upendo. Konyesha upendo ni ile hali ya kumuonyesha umpendao, upendo halisi wa kweli kwake ulio ndani moyoni mwako, na upendo wa kuonyeshea ni ule upendo wa kufanya vitu ili watu waone jinsi wewe unavyopenda. Upendo halisi wa kweli wa kutoka moyoni, upendo huu hukaa moyoni mwa mtu na ndio upendo halisi wa ukweli, ambao hukaa ndani ya mtu. Upendo huu sio lazima uonekane maana mahali pa upendo huu ni ndani ya moyo wa mtu ambapo hakuna anayeweza kuuona.

Upendo wa kuonyeshea, ni vile vitendo vya mtu kufanya jambo au kuonyesha ishara fulani kuonyeshea kuwa unao huo upendo ili watu waone. Tatizo la kuonyeshea ishara ya upendo, na ni sometimes ni ishara tuu ya mapenzi, kupeana zawadi za upendo, maua, chocolates au zawadi zozote za upendo, ili anayependwa aone kuwa anapendwa kwa vitu vya kuonekanika, lakini sio lazima awe anapendwa kweli.

Kwa kadri siku zinavyokwenda, mapenzi kati ya wapenzi wapendanao, yamekuwa ni mambo ya maonyesho zaidi ili watu waone na sio mapenzi, ya dhati. Mapenzi ya sasa ni mapenzi ya kupenda vitu kuliko utu, hivyo mtu kujiona unapendwa ni lazima upewe vitu vya kuonekanika, pesa, zawadi, mtoko, ili tuu kuonyeshea kuliko ukweli halisi. Naomba kutumia maneno ya lugha ya Kiingereza, “life and love is more materialistic than realistic”.

Sisi binadamu tumejaaliwa uwezo tofauti tofauti wa kujieleza kwenye mapenzi, yaani “expressing yourself”, nakumbuka enzi za ujana, nikiwa nasoma shule ya sekondari ya wavulana ya bweni ya Ilboru, huko Arusha, ni kawaida shule za wavulana kuwa na mahusiano ya kutembeleana na shule za wasichana watupu. Ikatokea kwa wakati huo, mkoa wa Arusha hakukuwa na shule za wasichana, hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule yetu wa enzi hizo, Mwalimu Mushi, (tukimuita kwa jina la utani Bino). akaamua wavulana wa Ilboru, watacheza muziki na wasichama wa shule za Weruweru, Machame na Kibosho Girls pekee, za Moshi, ndizo shule zenye hadhi na nidhamu ya kuchanganyika na Ilboru.

Baada ya kucheza muziki, wiki zinazofuatia ni mvua ya barua za mapenzi, kumiminika toka kwa wasichana wa shule hizo, kuja shuleni kweli, ikatokea tuu ni mimi ni mmoja wa vijana tuliofahamika kuwa ni wepesi wa kujieleza, hivyo barua hizo za mapenzi kuletwa na mimi kuzisoma na ku draft majibu ya barua hizo la ustadi mkubwa, kiasi kwamba barua hiyo ikifika inakokwenda, yule binti hawezi kabisa kuchomoa, ananaswa na maneno matamu kama samaki kwenye ndoana!. Hivyo kujikuta nina pile ya barua za watu, hivyo tukajikuta tumetenganeza mahusiano ya kudumu na kiukweli baadhi ya mahusiano hayo yaliishia kwenye ndoa, mimi mwenyewe nikiwa ni mmoja wao!

Barua zile hazikuwa ni barua za maneno ya mapenzi ya kweli kutoka moyoni kwa aliyeandika, kwasababu anakuwa ameandikiwa, lakini kwa msomaji, alikuwa anajisikia raha ya kweli kwasababu aliamini hayo ni maneno ni ya kutoka moyoni kwa mwandishi, kumbe alikuwa anadanganywa tuu, hivyo mapenzi ya sikuhizi kudanganyana ni kwingi kuliko mapenzi halisi. Wadada zetu wa kisasa nao ndio kabisa, badala ya kupenda pendo la kweli, wanapenda vitu, pesa, offer, gari, na starehe kuliko mapenzi halisi ya kweli.

Moja ya mifano mizuri ya upendo wa kweli wiki hii ni nchini Tanzania ni ule upendo wa picha ya pamoja ya wale Watanzania wawili waliokutana jijini Brussels nchini Ubelgiji kwa mazungumzo mafupi. Ule ndio upendo wa kweli ambao unatibu na kuliponya taifa!. Hongera Mama kwa upendo huu!.

Kufuatia uzungu mwingi wa upendo wa kuonyeshea siku ya Valentine, wake zetu, wapenzi wetu, wadada zetu, mabinti zetu, wamepoteza uwezo wa kubaini upendo wa kweli wa kutoka moyoni, sasa they are crazy na upendo wa vitu vya kuonekanika!, this is madness!. Mmoja wa mabinti zetu wa Kitanzania ame trend duniani kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuweka bango kubwa la barabarani lililogharimu shilingi milioni 6 likionyeshea picha ya mpenzi wake na kujieleza hivyo ndivyo anavyompenda mpenzi wake, hivyo bango hilo kusababisha kizaa zaa kwa kila anayependwa, kutaka awekwe kwenye Bango!. Bado najiuliza kwa sisi wanaume wa Kiafrika, ile kumposti tuu mpenzi mmoja kwenye status, ni issue, hii ya kuweka bango itakuwaje?.

Upendo ndio amri kuu kuliko zote Mungu aliotupa “mpendane”, ila upendo wa kweli ni ule upendo ukaao moyoni na sio upendo wa kuonyeshea!. Kuna wanaopendwa kwa kupewa maua, zawadi, kutolewa out na kufanyiwa kila kitu, lakini ikawa ni upendo wa maonyesho tuu, lakini sio upendo wa kweli, halafu kuna wale ambao, hata kuambiwa Happy Valentine hawakuambiwa, hawakupewa ua, au zawadi yoyote, lakini ndio wanaopendwa kweli. Pendo la kweli ni la moyoni na sio la kuonekanika.

Hii ni faraja kwa wale wote ambao hamkuambiwa Happy Valentine, hamkupewa kadi wala zawadi yoyote ya Valentine, furahini ndani ya mioyo yenu kwasababu nyie ndio mnaopendwa pendo la kweli la mayoni ambayo halionyesheki.

Hongera TotalEnergies kuwapenda Watanzania kwa kuonyesha upendo wa kweli na sio upendo wa kuonyeshea, lakini hongera kubwa zaidi kwa wote wanaopendwa kwa upendo mkubwa zaidi wa kweli ulioko moyoni usioonekanika kuliko wale wanaopendwa kwa kuonyeshea la sio upendo wa kweli.

Happy Valentine wasomaji wangu.

Nawapenda!.
 
Back
Top Bottom