Unapata shot ya stock kwenye biashara Yako? Nipe kazi niwe stock controller wako. Mungu ni mwema SITAKUANGUSHA

Tanki

JF-Expert Member
Apr 7, 2013
491
189
Nina uzoefu wa miaka miwili na nusu ambapo nilifanya katika moja ya depot ya kampuni ya Cocacola, hizi ambazo zinaitwa SSD. Nilikuwa chini ya kampuni Fulani ambayo mshahara wangu ulikuwa ukipitia kwenye hiyo kampuni. Nilifanya kazi Kwa miaka kadhaa na niliacha kazi Kwa amani kabisa pasipo changamoto yoyote ya kiutendaji.

Ok, kipindi kile Depot tulikuwa na magari zaidi ya 9 ya kwenda kuuza soda mitaani. Nikiwa kama stock controller chini ya Team Leader, niliwajibika kusimamia operation zote za depot kuhakikisha gari zinapakia mapema ili ziwahi kuingia sokoni. Nina uzoefu wa kuhesabu stock inayopakiwa kwenye magari, na nina uzoefu wa kuhesabu stock iliyopo depot, lakini pia nina uzoefu wa kuhesabu stock iliyorudi kutoka sokoni ( Returns ).

Stock ni vema ikawa inahesabiwa kila siku iitwayo leo. Nina uzoefu wa kufanya hivi. And siyo tu kuhesabu, bali ni pamoja na kuipima stock ili kujua Iko sawa? Ina shot? Ina over?. Kama Ina shot Je hiyo shot imetokea wapi? Kama ni over nayo imetokea wapi wakati depot hatuzalishi stock.

Nina uzoefu wa kufuatiria date code ( expire date ) ya kila stock inayoingia depot. Hapa tunatakiwa tupeleke sokoni stock iliyotangulia kuingia depot, ikiisha ndipo iende stock mpya. Hii ni Ili kuepuka stock ku expire ambapo haitafaa tena kuuzwa.

Nazijua janja janja na magumashi yote ya madereva na vijana wa mauzo wanaokwenda sokoni kuuza stock. Unajua nini?, ukipata shot ujue kuna sababu, maana shot nyingine zinaletwa na watu, na nyingine ni system, either kwenye ku-panch manifest, kwenye kucheck in returns n.k.

Mimi nahesabu soda as a stock, ila Kwa mtu wa mauzo yeye anahesabu as a PESA.

Naamini kwenye ushirikiano, uaminifu na kujituma. Unajua nini?, mwisho wa siku Mimi stock controller na mtu wa mauzo wote ni wauza soda. So, lazima tuwe kitu kimoja Ili tu yeye asipate shot ya hela na Mimi nisipate shot ya stock. Haonewi mtu, ila panapobidi kulipwa aisee LAZIMA ulipe kaka.

Umri: miaka 31.
Makazi : Dar es salaam (ila naweza kufanya kazi mkoa wowote. )
Kazi siyo lazima iwe kama niliyokuwa nikifanya. Naamini naweza kufanya kazi ya ku control chochote ambacho kinahitaji umakini kwenye mahesabu.

Naamini ninafaa. Naamini sitakuangusha.
Mungu akubariki pindi unapowaza kuja inbox hapa jamiiforums au tuwasiliane Kwa email yangu hii au Kwa simu

0676558714

zakariapetro337@gmail.com
 
Back
Top Bottom