Unapata hisia gani ukifikiria kuhusu Umri wako?

Jana bi mkubwa kwa mara ya kwanza kaniuliza umri(sio kwamba haujui) baada ya kumjibu akauliza kuhusu ishu ya mke/kuoa. Nilishtuka sikutegemea kabisa hayo maneno, network ikashake tukawa hatusikilizani kwenye simu nikakata, akapiga akasema nasingizia network(kweli sikuwa namsikia), akaniambia umri umesogea nikabaki kumsikiliza tu.

Nmewaza umri ushasogea kiasi cha kuanza kusukumwa na wazazi kufanya jambo ambalo natakiwa nilifanye kwa msukumo wangu binafsi, au ndio kaona kijana wake nna itikadi za kataa ndoa? Hata sielewi ila hili la jana limechukua nafasi kubwa sana ndani ya mawazo yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom