Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Haijanitokea kwa mtu mmoja au wawili. Ni watu wengi sana. Wengine ni watu wangu wa karibu. Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni.

Mwingine labda ni mtu ambae hamjawahi kuwasiliana na ndiyo kwa mara ya kwanza labda umepata namba yake. Nayeye hana namba yako na una shida ungependa kuongea nae. Unapiga simu hapokei. Baadae atakuja kukwambia namba ngeni hapokei.

Nini siri ya kutopokea namba ngeni? Faida zake ni zipi au hata nyinyi mnafanya bila kujua faida na hasara zake?
 
Hao watu ni waoga au matapeli

Ni hawajiamini kupokea namba ngeni kwa sababu kuna mtu ambaye hawapokei simu yake wanahofia ametumia namba ngeni kuwapigia

Watu hawa mara nyingi ni watu wanaodaiwa hawalipi au malaya

Ukiwa na mwanamke au mwanaume ambaye anaogopa kupokea namba ngeni, jua utapigwa siku sio nyingi. Pia usikopeshe mtu kama huyo, utajuta
 
Kwa uzoefu wangu,katika kupokea namba ngeni nimekutana na mengi haya;

1. Mtu anaomba Hela.

2. Anasalimia.

3. Amekosea namba.

4. Anakuliza wewe ni nani (wakati kapiga yeye).

5. Ukipokea haongei ila anasikiliza sauti.

Faida ya namba ngeni ni kupigiwa na watu wazito. Mara nyingi watu wa kwenye mfumo hutumia namba ngeni kwenye mambo yasiyo ya ofisi.
 
Y
Muwe mnatuma sms za kujitambulisha kwanza ili hata asipopokea ujue kafanya makusudi.

Wengi wanaogopa matapeli wa ile pesa tuma namba hii
Yes, mtazamo wako unaweza kuwa sahihi. Lakini mtu kama tapeli si unamsikiliza unampuuza au unamkatia simu baada ya kumsikiliza. Sasa hii ya kupuuzia namba ngeni, what if ni shida ya dharura au ni mchongo wa maana ambao watu wanakusogezea?
 
Unaweza ukamblock mchepuko halafu akatumia namba nyingine kukutafuta utaishia kupata aibu ni
Kama utapiga na namba isipokelew ni jambo dogo tu kujitambulisha kwa sms wewe ni nani
Sio kila utakutana na situation za namna hiyo.
 
Back
Top Bottom