Hii comment murua kabisa kutoka kwa bwana denoo JG kukemea kinachoendea huko Zanzibar.
Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
Ameanza na ushauri
Anachohisi ni tatizo
Anashangaa jinsi hii jamii (Znz) ilivyo ya ajabu
Anakemea unafiki
Anatoa Elimu
Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
Ameanza na ushauri
Tatizo upeo tu, wale watu wanatakiwa kuwa wanapewa safari za boti bure kuja huku bara kujifunza watu wanavyoishi.
Anachohisi ni tatizo
Kukaa kwao sehemu moja muda mrefu kumewafanya kuwa kama wanakijiji wasiojua nini kinaendelea kijiji cha pili.
Anashangaa jinsi hii jamii (Znz) ilivyo ya ajabu
Wanawazuia wengine wasile kisa wao wamefunga, sasa badala ya kufunga kuendane na unyenyekevu, wao wanaleta ubabe, hiyo inakuwa funga ya sampuli gani?
Anakemea unafiki
Wanajidai kufunga huku wanawaza kula muda wote ndio sababu yao kupiga marufuku wengine wasile, kama wangekuwa wanafunga kweli wasingekuwa na muda wa kufikiria wengine wanafanya kitu gani.
Unamletea kisirani anayekula, kwani wewe nani alikulazimisha ushinde na njaa tena ikiwa umekula usiku kucha? hii kitu kumbe inaonesha hao wafungaji hawafungi kwa moyo, ni hizo sheria zao huko ndio zinawalazimisha kufunga.
Anatoa Elimu
Jambo la kiimani halitakiwi kusukumwa na kiboko, hiyo inakuwa sio imani tena, ni amri ya ulimwengu ambayo inakuwa lazima muifuate mtake au msitake.
Huwezi kumlazimisha mtu kwenda mbinguni kwa kiboko, atakuwa tu anakufurahisha machoni kwa kushinda na njaa, kumbe moyoni anatamani kupiga msosi, hiyo funga ya hao jamaa simply naona ni maigizo matupu.