Unajua ni kwanini zamani inasemekana kulikuwa na watu wengi wenye akili?unajua kwanini vijana maisha ni magumu?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,546
2,989
Kila zama na nabii wake,walikuwepo wakina adamu,nuh na akina ibrahimu wote walikuja wakati ambao dunia haimtambui mungu na ujio wao ulikuwa ni wenye lengo la kutambulika kwa nguvu kuu yenye mamlaka dhidi ya nguvu zote,katika zama hizi habari zilikuwa hazina ukubwa kiasi cha kusambaa kila eneo kwa haraka anga na barabara zilishambuliwa na kwako za wanyama na bado mazingira yalikuwa magumu kufikika.

Watu wengi wenye uwezo huenda walikutumia nguvu na imani kutawala {uchawi na dini} hivyo ilikuwa ni rahisi kutawala kutumia hizi vitu 2 kutawala lakini wengi wao walikuwa ni free minded kwakuwa hawakuwa ni wenye kupokea mabadiliko ya akili na akili zao zilikuwa active kutokana na kwamba ukuwaji wa teknolojia ulikuwa bado si wa kuridhisha,wapo waliopata maafa sababu ya kuhoji na wengi wao walikuwa ni famous kutokana na kuhoji kwao mpaka kufikia hadi leo.

Vijana wa kileo tumebakia katika maendeleo makubwa ambayo yanatunyima uwezo wa akili zetu kufunguka na hata zikifunguka unakuta tayari umeshatengeneza mazingira magumu ya wewe kubadilika,waliofanikiwa wachache bado wanataka kutawala kupitia wewe imagine kijana siku nzima anaishi kuangalia kwenye TV akili huadapt na kuhgitaji kama ilivyooneshwa end of the day tumebakiwa na picha za kutuaminisha kuwa life gonna change kumbe umri unazidi kusogea.

Wengi teknolojia inatuendesha inavyotaka na hivyo kutufanya kuwa ni addicted na japo hatujioni,akili inawaza akina diamond & alikiba,haji na zay na hakuna jambo la msingi tunalolifanya zaidi ya mitandao,wengi wetu tunatumia fursa ya kusambaza umbea matokeo yake tunajikita kwenye media tunasahau uzalishaji wa msingi.


NAWAKUMBUSHA MBELENI KUNA NJAAA,FUNGUA UBONGO.
 
Back
Top Bottom