Ujasusi ni funguo waliyoipoteza vijana wengi. Sio ajabu wakahangaika

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
UJASUSI NI FUNGUO WALIYOIPOTEZA VIJANA WENGI. SIO AJABU WAKAHANGAIKA.

Anaandika, Robert Heriel
Jasusi

Huwezi ukafanikiwa kwenye Jambo lolote bila ya kuwa Jasusi. Never ever! Ujasusi ni maarifa na uwezo wa kutafuta na kukusanya taarifa kisha kuzichakata, kuzichambua na kuziweka katika mafungu yake(Categorization) Kwa ajili ya kuzitumia katika mipango na malengo Fulani. Ujasusi ni sehemu ya mkakati muhimu katika kutimiza Jambo Fulani au lolote lile. Wahenga walisema "Informations is power"

Ujasusi ni muhimu Kwa sababu maisha ya mwanadamu yanaongozwa Kwa patterns, codes, na passwords.
Jambo lolote ambalo Kwa sasa unalichukulia la kawaida basi tambua zamani lilikuwa sio lakawaida, lilikuwa linasumbua watu, lakini baada ya watu kuhangaika kutafuta Patterns za kulifungua na wakafanikiwa ndio maana leo hii unaliona ni Jambo la kawaida.

Mambo mengi yanayosumbua watu Zama za leo, ni Kwa sababu bado codes na patterns zake hazijajulikana, hivyo zitakapojulikana kizazi kinachokuja halitawasumbua.

Ujasusi unaanza Kwa kujitambua wewe inside, kisha kutambua wanaokuzunguka na mazingira yako kisha baadaye ujitambue wewe Kwa upande wa nje.

Wanasema kabla hujajitambua wewe WA nje basi watu watakutambua, yaani mtu hawezi kujiona yeye mwenyewe pasipo KIOO au kitu kinachosharabu taswira yake lakini watu wanaweza kumuona. Unaweza kujiuliza hapo bila ya kioo ungeweza kujijua unasura gani? Jibu ni hapana, lakini watu wangekujua unasura gani. Hii inamaanisha Jambo gani? Kwa nini viumbe wameumbwa Kwa namna ya kushindwa kujiona wenyewe labda mpaka watumie kioo au maji au Mada yoyote inayosharabu Taswira.

Watu wamepewa uwezo wa kukuona Kwa nje unaweza ukafanya nini Kwa vile wanavyokuona. Lakini wewe Kwa ndani ndio unajua unaweza kufanya nini. Hata hivyo vipo vitu ukivifanya vinaweza kuwafanya watu wakujue wewe WA Ndani ukoje. Ujasusi ni Connectivity hiyo wake akilini. Kwenye mwili kuna kitu inaitwa Coordination yaani uwezo wa viungo vya Mwili kuwasiliana na kutumia taarifa kisha kuzifanyia kazi. Huo ni ujasusi katika mwili wa binadamu.

Vijana wengi wa siku hizi wamepoteza au kupuuza funguo nyeti ambayo ndio yenye uwezo wa kufunga milango karibu yote. Ujasusi ni funguo Malaya ambayo inafungua milango mingi Sana katika maisha ya mwanadamu.

1. Ujasusi katika Biashara na Taaluma
Biashara sio mtaji tuu. Biashara ni zaidi ya mtaji. Lazima ujue unataka kufanya biashara gani na Kwa nini. Mtu yeyote anayetaka kuanzisha biashara lazima awe na Lengo/shabaha ya Kwa nini anafanya biashara hiyo.
Lengo ndio litaibua mipango na mikakati. Kwenye mikakati ndipo ujasusi lazima uhusike.

Lazima ujue mambo haya katika biashara;

i. Umri wa Biashara
Kila kitu kina umri. Kuzaliwa, kukua na Kufa. Unapoanzisha biashara lazima ujue biashara hiyo umeikuta inaumri wa miaka mingapi tangu izinduliwe, na hapo ilipo imebakiza miaka mingapi Ife. Zingatia Hakuna kitu kinachodumu Milele. Pia zingatia katika biashara zipo biashara za kudumu kama vile biashara ya vyakula, maji, nguo n.k. ambazo ni basic needs za wanadamu.

Pia zipo biashara za msimu hizi mara nyingi zinatokana na Uvumbuzi wa Teknolojia. Lazima ujue umri wa Biashara au Taaluma Fulani. Kwenye biashara tunazungumzia kitu kinaitwa Rasilimali/Resources, na katika Resources kuna Renewable resources and Non-renewable resources. Hivyo lazima upate taarifa ya umri wa kike utakachokukifanya.

Kasi ya dunia Kwa sasa ni kubwa Sana. Vitu vingi ni rahisi kupitwa na wakati, hivyo lazima uangalie angalau kitu ambacho kitadumu Kwa angalau Nusu Karne au Karne moja.

ii. Washindani wako
Chunguza washindani wako katika biashara au Taaluma, wakoje kiakili, ki-exposure, mipango na malengo Yao, mikakati yao ikiwemo namna wafanyavyo promotion, propaganda, Fitna n.k. Angalia mitaji Yao, ubora wa Huduma zao, bei n.k

iii. Angalia Soko
Bidhaa unayoitaka inapatikana wapi Kwa gharama nafuu kabisa, hakikisha ujue Washindani wako wao chimbo Lao ni wapi. Hakikisha usiwe na chimbo moja unalolitegemea pekee. Hii itakusaidia kuwa na Sustainability ya muda mrefu bila kupata shambulizi la kushtukiza na kuanguka mara moja. Kisha tafuta wapi utakapouzia biashara yako. Kamwe usipende kuuliza wafanyabiashara wenzako biashara wanayoifanya hutapata taarifa za kweli au uhakika.

Lazima uwe na bidhaa za kujaribu soko lako. Mwisho usitegemee bidhaa moja kuwa sokoni. Tengeneza bidhaa mbili zenye Majina tofauti utakazo zishindanisha moja iwe Bora kuliko nyingine. Yaani hiyo tunaiita jitengenezee adui bandia katika bidhaa zako mwenyewe. Nilishaeleza katika andiko langu moja" Nadharia za Taikon;UTAWIWISHAJI"

iv. Pandikiza vibaraka
Hakikisha una vibaraka kwenye Mamlaka na tawala, kisha usiwe mtu wa maneno mengi Sana. Hiyo sio kazi yako. Hao watakusaidia Kwa sehemu ndogo zinazohusu ulinzi na migogoro pale inapozuka katika biashara yako.

v. Fitna na Propaganda
Tumia Watu wenye ushawishi na Wataalamu kutangaza Huduma au biashara yako.
Utawagawa katika makundi mawili,
a) Direct Propagandists
b) indirect Propagandists
Direct Propagandists hawa wanaweza kuwa vyombo vya habari, machawa, wasanii, wanamichezo na waigizaji.

Indirect Propagandists hawa wawe Wataalamu kama Maprofesa, Wanasayansi, madaktari, n.k. Mfano, unauza bidhaa ya Vinywaji au Mkate au biskuti. Unaweza lipa Mtaalam au profesa au Daktari akawa anaongea mada Fulani labda ni ishu ya Nguvu za kiume au kuongeza siku za kuishi, lakini akataja Madini au nutrients Fulani inasaidia Kwa kiwango kikubwa, anaweza kutoa mfano wa bidhaa yako kuwa inahayo madini au nutrients.
Pia viongozi wa dini.

Hata hivyo unaweza kutumia vitu vilivyokatazwa na dini na kuwalipa Wachungaji au masheikhe waipige vita mara Kwa mara ili kuipa Promo, huku upande wa Wasanii au watu wengine mashuhuri ukiwafanya wawe mabalozi ya kitu hichohicho. Hiyo biashara lazima itembee.

Maisha yanahitaji uwe na taarifa zote mbili, taarifa sahihi na taarifa zisizo sahihi. Pia uwe na uwezo wa kuzitumia taarifa zote mbili ili kujinufaisha. Kuwa na taarifa pekeake haitoshi. Ila kuzitumia inamata Sana.

2. Ujasusi kwenye Ndoa/ Familia
Vijana wa sasa wengi wanapuuza vitu vikubwa Kwa kuviona vidogo kutokana akili kuwa ndogo. Na hapo ndipo Jamii ya watu weupe inapotupiga Bao. Ndoa ndio sehemu pekee ya kutengeneza taifa Bora.

Lazima ufanye upelelezi wa mambo haya kabla hujaoa au kuolewa

i. Unayemuoa au kuolewa Naye ni Nani, chimbuko lake, akili yake, Afya yake, kizazi chao kikoje, Wanasema Embe halianguki mbali na mti wake, na maji hufuata Mkondo. Asijekukudanganya mtu ni nadra Sana kushinda asili yake. Ukimuona mtu ni Malaya elewa sio Kwa bahati Mbaya. Jua ni Asili Yao. Hata wajitetee vipi elewa hivyo. Ukiona mtu mwizi au mchoyo au vyovyote vile jua kwao ndio wako hivyo.

Ingawaje wapo watu exceptional ambao ni wachache Sana.

ii. Mitazamo, ndoto na maono yake na waliomlea.
Hawezi kuwa mbali na hayo.
iii. Chunguza life expectancy ya ukoo wao.
Chunguza umri wa kuishi katika koo unayotaka kuoa au kuolewa.
Usije sema unamkosi utakapoachwa mjane au mgane watoto wangali wadogo.
iv. Mambo mengine ya Dini, na tamaduni.
v. Uchapakazi na uzalishaji n.k.

Hata kama umeoa lazima umchunguze Mkeo, kamwe usikubali kuishi na mtu usiyemjua au ambaye hujui anafanya nini behind You. Hata kama unamajukumu mengi kiasi gani, hiyo haikuzuii kuweka mifumo ya kujua nini kinaendelea katika nyumba yako. Kwenye maisha hakuna Jambo la kushtukiza au linalotokea kama Ajali au bahati mbaya. Kila kitu kinaanzaga Kwa mchakato.

Ni utoto kuendekeza Hisia kuliko Akili. Ukisikia mtu anasema kuwa moyo wake ndio umeamua ujue hapo hakuna kitu. Bado anaakili changa. Mtu ambaye yupo tayari kuanzisha kizazi bora kamwe hawezi tumia Moyo kupokea Oda za hatma ya maisha yake. Wengi wanaotumia moyo hujikuta wakifanya maamuzi mabaya. Lakini kama ni kijana Mdogo WA miaka 14-20 huyo akitumia moyo usimlaumu jua ni kupevuka na kubalehe kunakomsambua.

Lakini kama jitu linamiaka 25+ na anatumia moyo jua huyo ni Mpumbavu.

3. Ujasusi kwenye Makazi
Elewa eneo unapoishi na wakazi wake vizuri Kabisa. Usipende watu wakujue Sana na wakuzoee Sana. Nawe usiwazoee Sana Ila jitahidi uwajue Kwa namna ya Akili. Zingatia adui WA Mtu hatoki Mbali. Hivyo vyovyote utakavyofanya jua kuwa adui wako yupo katika mzunguko wako. Hivyo usiwe mtu wa kuji-expose Kwa watu.
Shida zako au mafanikio yako. Jua nani ni mke wa Mtu Nani siye kama bado haujaoa. Kamwe usiingize Demu WA hapo mtaani chumbani kwako. Kama utaweza usidate na warembo wa mtaani ulipopangisha,

Hakikisha unajua wahuni wote wa mtaa. Hii itakusaidia kiusalama. Kama ni kijana hakikisha hata kama unauwezo na unafanya kazi yenye kipato cha Kati. Hakikisha unajua vichochoro vyote vya mtaa wenu, siku za wikiend toka zurura Kwa mguu unanyoosha miguu ukipita kwenye njia na vichochoro vyote vya mtaa. Sio kwa siku moja. Bali wikiend hii unapita kichochoro Hilo, wikiendi hii kichochoro kile. Ujue vinatokea wapi.

Elewa jina la mtaa na majina ya watu maarufu

Usipende kuomba omba vitu, wala usipende watu wakusogelee kukuombaomba vitu. Mazoea mazoea Epuka Sana. Kama umepanga usipende vitoto vidogo vya jirani kuingia ingia chumbani au kwako. Usipende watu majirani kuingia ingia kwako. Acha uswahili Swahili. Halikadhalika usipende kuingia kwenye majumba ya watu.
Usipende kukopesha kopesha watu unaoishi nao. Kiufupi usipokuwa na mazoea Sana na watu ni ngumu watu kuja kuwakopa. Ila pia uwe mtu wa kutoa misaada Kwa wanaohitaji misaada.

4. Ujasusi Eneo la kazi
Hakikisha unajifunza Saikolojia ya binadamu, body language, maana ya sauti ya matamshi ya watu wanapozungumza. Ni rahisi mtu kujua utafukuzwa kazi lini kama utakuwa makini na mambo hayo. Ni nadra Sana mtu atukuzwe kazi ghafla kabla Boss au mkurugenzi hajaandaa mpango wa kumfukuza kazi. Nadra Sana.

Taarifa nyeti zinazohusu Future za Ofisi unazofanyia kazi ni muhimu kwako Kama mfanyakazi, Usiishi Kama Kuku asiyejua kesho kitatokea nini. Ingawaje tumia akili Sana kuzipata hizo taarifa. Na hata ukizipata usizitoe Kwa watu. Ujasusi Una kanuni muhimu ya usiri.

Mambo ya nyumbani usilete Ofisini. Na mambo ya Kazini usilete nyumbani. Wewe Kama ni Boss mahali unapofanyia kazi usilete Uboss wako Mtaani, utakwama. Sifa mojawapo ya ujasusi ni kuwa Normal, isipokuwa kama inawezekana kuwa Low-key.

Ukileta Uboss wako mahali unapoishi utakwama Maeneo mengi mno. Hasa kiuchumi, hautakuwa huru. Ukipata shida labda ya kutengenezewa kitu fulani sio ajabu ukalipishwa pesa nyingi kutokana na kuletaleta uboss wako wa kijinga. Ni Kheri utoe Pesa Kwa moyo mmoja lakini sio Kwa kupigwa. Ukileta uboss mtaani itakufanya usiwatambue wanaokuzunguka Kwa usahihi kabisa yaani kuna hatari ya kupata taarifa za uongo. Wengi watakuigizia au ku-pretend kama sio kuwa Wanafiki.

Ukileta Uboss au usomi wako mahali unapoishi utajikuta unakuwa mtumwa na haupo huru hata kuongea Pumba au mambo ya kipuuzi. Unajua sio muda wote unapaswa uongee mambo ya maana. Kuna Muda akili inahitaji uongee mambo ya utumbo utumbo, sasa ukileta usomi na uboss wako mtaani utajikuta unakuwa kauzu muda wote Kama Lofa au mbumbumbu Fulani hivi.

5. Ujasusi wa tabia ya nchi na Hali ya hewa
Lazima ujue mwenendo WA anga Kwa mwaka huo upoje na utakuwaje. Peleleza na kusanya taarifa zinazohusu tabia ya nchi na Hali ya hewa ikoje na itakuwaje. Hali ya hewa Kwa sehemu kubwa inaratibu. Maisha yetu Kwa sehemu kubwa. Walioweka Weather Forecast (Utabiri wa Hali ya hewa) hawakuwa wajinga

Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Sawa muzee..
 
Ujasusi mkubwa zaidi ni ujasusi binafsi, if you know your self, you will benefit to know others, shida ni kua watu wako busy kujasusi ya wengine wakati wao hawakajijasusi.
Unafatilia unafatilia mtoto wa jirani amesoma nini chuo na wewe usome kumbe mwenzio kashaandaliwa mazingira.

I think SWOT analysis is best piece of weapon, always know tha self first
 
Nimejifunza mengi, sijajutia kusoma hili bandiko.
Ngoja nilihifadhi kwa matumizi endelevu.

Hongera sana mkuu Robertooo
 
Haya madini hayafundishwi shuleni.

Nimeongeza kitu kikubwa sana leo
 
yani mtu anayenyanduana na kila demu kama daimondi anapata wapi muda wa kuchunguza jamaa akiona K tu anawaza kuloweka tu, haya mambo ni magumu sana usichukulie poa , kuna chawa pia wamejaa tele unadhani thinking capacity yao inaruhusu ku think positively, mambo ni mengi ila muda mchache
 
Back
Top Bottom