Unaikumbuka hii movie???

Unaikumbuka hii movie???

This was one of the best movie series ambayo niliipenda, ninaipenda na nitaendelea kuipenda hadi mwisho wa uhai wangu. Yaani ilikuwa niko radhi nisile ili mradi niangalie hii movie na ilikuwa ukitaka kugombana na mimi tu wewe nikataze kuangalia hii movie utaona mziki wake. Sio siri hii movie iliuteka sana moyo wangu. Sijui kwako wewe mdau, unaichukuliaje movie hii??




U137P200T1D195925F10DT20081103021921.jpg

Tuweke habari zilizokamilika.kusema tu unaikumbuka hii picha bila kuweka jina la movie si uandishi mzuri.Anyway,nami nilikuwa mdau wa hii movie na niliwahi kutuma thread ya kuomba kujua cd zake nitazipata wapi.kuna wadau walinielekeza posta na ubungo.Bahati nzuri niliipata hiyo cd!asante kwa walionielekeza.Picha ina visa vizuri sana na uigizaji uliobobea wa shivo(master),wukong,bajie,wuneng,nk
 
nakumbuka kuwapa madogo kampani kuingalia

na mimi nikajikuta nikiifurahia
 
haha, bongo tulikua tunasema shivo, mi baada ya kwenda china ndio nikagundua kua ni shifu(师傅)maana yake ni mwalimu au mtu yeyote mwenye ujuzi au utade wa kitu flani, shifu kwa sasa sio common China kwa vijana ila limebaki kumaanisha dereva, na katika movie nyingi na tv za zamani au vijijini pia bado unaweza kulisikia neno shifu, ukija China ukitaka kuchukua taxi, we mwambie shifu unataka unaenda wapi tuu shwari:lol:
 
This was one of the best movie series ambayo niliipenda, ninaipenda na nitaendelea kuipenda hadi mwisho wa uhai wangu. Yaani ilikuwa niko radhi nisile ili mradi niangalie hii movie na ilikuwa ukitaka kugombana na mimi tu wewe nikataze kuangalia hii movie utaona mziki wake. Sio siri hii movie iliuteka sana moyo wangu. Sijui kwako wewe mdau, unaichukuliaje movie hii??

U137P200T1D195925F10DT20081103021921.jpg

Mh umenikumbusha mbali kweli, by then nami nilikuwa napenda kweli, kina wukong, shivooo na yule mwingine mzembe mzembe me nilikuwa namuitwa mapua lol!
 
Kumbe vikojozi wengi humu ndani, sisi tumekulia enzi za kuangalia mtambo wa ZnZ and KBC, that time bongo kiza kabisa kwenye hii mtambo. Tulikuwa tunasikiliza mzee jongo na pwagu na pwaguzi
 
Nakumbuka niliwahi kusoma kitabu chake miaka mingi iliyopita.
 
Kumbe vikojozi wengi humu ndani, sisi tumekulia enzi za kuangalia mtambo wa ZnZ and KBC, that time bongo kiza kabisa kwenye hii mtambo. Tulikuwa tunasikiliza mzee jongo na pwagu na pwaguzi

Ua jekundu na Debora Mwenda katika Mama na mwana
 
dah!mkuu umenikumbusha mbali mno,hcho kipindi kilinifanya nikawa naenda misa ya jioni,ili nicheki monkey
 
"Safari ya Kwenda Magharibi".

"Safari ya Kwenda Magharibi" ni riwaya nzuri katika historia ya fasihi ya kale ya China. Riwaya hii ilitungwa kwa mujibu wa vituko vilivyomkuta sufii mkubwa wa dini ya Kibuda, Tang Zeng, alipokuwa katika safari yake ya kwenda India kuchukua msahafu katika karne ya 7 K.K. Katika riwaya hiyo Wu Chengen alibuni wafuasi watatu kufuatana na sufii huyo. Mmoja wa wafuasi wake alikuwa mfalme kima Sun Wukong. Sun Wukong alikuwa na nguvu za kudura ya mungu, anaweza kujigeuza sura 72 na fimbo yake ya kupambana na mashetani yaweza kurefushwa kuwa ndefu hadi mbinguni na kufupishwa kuwa ndogo hadi kama sindano ya kutia sikioni. Mfalme kima Sun Wukong ndiye aliyethibitisha matumaini ya mwandishi kwamba mambo yote maovu yatatokomeza kabisa katika jamii.

"Safari ya Kwenda Magharibi" Iliingizwa katika filamu ya mwendelezo mwaka 1982 mpaka mwaka 1986, ilikuwa mara ya kwanza kuonyeshwa kwenye Runinga na ilikuwa na sehemu 11. Simulizi za hii tamthilia ulimalizika Februari ya mwaka 1988. Tamthilia hii kwa ujumla ina sehemu au matukio 25.

Moja ya simulizi ambayo wengi wanaipenda, na hata iliwahi kutafsiriwa kwa Kiswahili ni ile ya Mfalme Kima Am'bumunda Shetani Mfupa Mweupe (Monkey King and the White Bone Devil)

"Safari ya Kwenda Magharibi" iliandikwa na Wu Chengen katika miaka yake ya uzeeni, lakini matayarisho ya riwaya hiyo yalimgharimu maisha yake yote. Alipokuwa mtoto mara kwa mara alifuatana na baba yake kwenda kwenye misitu minene na mahekalu, na baba yake humweleza hadithi za ajabu zilizotokea huko. Hamu yake ya kusikiliza hadithi utotoni mwake haikupungua hata baada ya yeye kuwa mtu mzima. Baada ya kutimiza miaka 30 alikuwa amekusanya hadithi nyingi za ajabu akanuia kuandika riwaya. Alipofikia umri wa miaka 50 hivi alikuwa amemaliza sura 10 za mwanzo za riwaya yake ya "Safari ya Kwenda Magharibi", lakini baadaye kwa sababu fulani aliacha kwa miaka mingi hadi baada ya kujiuzulu kazi na kuwa nyumbani.

"Safari ya Kwenda Magharibi" iliandikwa hadithi moja moja, lakini kila hadithi pia ni sehemu ya riwaya nzima. Ndani ya riwaya hiyo walitokea mashetani na miungu mingi ambao wanawakilisha haki na uovu. Kasri ya mbinguni ilionekana adhama sana lakini kwa kweli mungu aliyekuweko ndani ya kasri hiyo alikuwa mbabaishaji wa watu wema na wabaya, akilenga mfalme duniani; na kasri ya dunia ya pili ingawa ilionekana ukakamavu, lakini maofisa wanasaidiana katika hatia, walikuwa hawajali sheria na wadhulumiwa hawakuweza kupata haki. Hayo alilenga katika hali ya utawala wa kifalme. Mashetani walikula na kuwaua watu huku wakiwa wachoyo wa mali na kupenda warembo na kufanya uovu watakavyo. Katika hayo mwandishi alifananisha madhalimu na maofisa wa kifalme. Kwa upande mwingine Wu Chengen alifanikiwa shujaa kima Sun Wukong, ambaye alikuwa mtetezi wa haki, alikuwa na nguvu za kudura ya mungu na mwenye msimamo bayana kati ya watu wema na wabaya, fimbo yake ina nguvu za ajabu. Hii inaonyesha tarajio la Wu Chengen la kukomesha maovu yote katika jamii aliyoishi.

Riwaya ya "Safari ya Kwenda Magharibi" inajulikana sana kutoka kizazi hadi kizazi na katika miaka mia kadhaa iliyopita riwaya hii ni kama chimbuko la kutunga hadithi kwa watoto na michezo ya filamu na televisheni.
 
Mh umenikumbusha mbali kweli, by then nami nilikuwa napenda kweli, kina wukong, shivooo na yule mwingine mzembe mzembe me nilikuwa namuitwa mapua lol!

Lile zembezembe linaitwa Bajie a.k.a Kula kulala au nguruwe
 
dah!mkuu umenikumbusha mbali mno,hcho kipindi kilinifanya nikawa naenda misa ya jioni,ili nicheki monkey

Kumbe na wewe ulikuwa kama mimi. Ila mimi nilikuwa najitahidi naenda misa ya kwanza.
 
Back
Top Bottom