Hii dhana kwamba walimu hawazeeki ina ukweli wowote?

Hii dhana kwamba walimu hawazeeki ina ukweli wowote?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
61,664
Reaction score
126,410
Habari wanajukwaa.
Nimekuwa nikisikia hii kauli mara nyingi kuwa walimu hawazeeki tena wanasema hasa wa shule ya msingi, kwa sehemu mimi pia nilikuwa naiamini ila nadhani haina ukweli. Nitaelezea kwa mtazamo wangu na uzoefu wangu kwa nini nafikiria hivyo.

Ipo hivi, mtoto mdogo hasa wa shule ya msingi hawezi kuwatofautisha watu wazima kwa umri - kwake mtu mzima ni mtu mzima tu bila kujali ana miaka 25, 35 au 45 wote wapo kundi moja tu. Tulipokuwa shule tulifundishwa na walimu wenye umri tofauti ila sisi tuliwaweka kundi moja tu.

Let's say mwalimu alikufundisha akiwa na miaka 25, ukikutana naye baada ya miaka 20 atakuwa na miaka 45 na wewe utaona kama yuko vilevile kwa sababu huko nyuma tayari ulishamweka kwenye kundi moja na watu wenye miaka 45.

Nitatoa mfano mmoja, nina ndugu yangu mwalimu alianza kazi akiwa na miaka 20 mwaka 1989, ukikutana na wanafunzi wake utasikia hivi yule si alishastaafu eeh? Ukiwaambia bado wanashangaa inawezekana vipi 😁😁... Kwa sababu walikuwa wadogo walishindwa kung'amua kuwa alikuwa binti mdogo tu ambaye wengine pengine walikuwa wanamkaribia kiumri.

Mimi pia niliwahi kufundisha mahali fulani (of course sio wafundishwaji wote waliojua kuwa nilikuwa mwalimu wa mchongo). Imepita miaka kama kumi na tano nimekutana na mmojawapo wa watu niliowafundisha anaanza kuleta stori za walimu hawazeeki 😁😁 girl, I was literally 21 kipindi na kufundisha, baada ya miaka 15 ulitegemea kunikuta nimeshika mkongojo ama namna gani?

Ukitaka kujua kuwa ninachosema ni ukweli angalia walimu ambao wapo kwenye rika lako , wanafanana kabisa na umri wao na tunazeeka nao sambamba tu 😁

Yapi maoni yako mdau
 
Labda mazoezi wanayofanya walimu kila siku yanawapa uimara na kuwafanya wasichoke mapema.

kusimama zaidi ya saa 2 kwa siku 5 mpaka uku wakitembea tembea darasani wakati wanafundisha,kuongea kwa zaidi ya masaa mawili kwa siku 5 mpaka 6 sio mchezo ni mazoezi tosha.
 
Wiki iliyoisha nilikua na hekaheka ofisi za TRA karibia wiki Nzima niko pale nilichogundua ni kwamba wale watu wanaonekana wanaishi maisha ya anasa miili Yao imekaa ovyoovyo haswa wanaume hawa magonjwa hayawaachi salama
Kwa walimu hawanaga maisha ya Anasa kwa mshahara ule wanaishi kwa adabu sana na ukiangalia wastaafu walimu na wanajeshi wapo ngangari
 
Back
Top Bottom