Eti mwanga hauna spidi????Mwangaza ni kitu ambacho kinaisha mwishoni mwa uwezo wa chanzo kilichoanzisha mwangaza na hauna speed wala hausafiri,kama mwangaza unasafiri ungekuwa unasafiri milele bila ya kuwa na kikomo.kwa mfano ukiwasha taa mwangaza wake hausafiri ukaenda milele unaisha mwishoni mwa uwezo wa ile bulb,kama bulb ni watt 40 uwezo na duara la mwangaza litakuwa dogo,tafauti na kama bulb litakuwa 100 watt duara na uwezo itakuwa mkubwa na hapa hio safari ya mwangaza itaonekana kama ni kubwa lakini sababu ni nguvu ya chanzo cha mwangaza tu na sio usafiri wa mwangaza.
Kwa mfano Kama mwangaza unasafiri basi hata bulb ya watt 20 mwangaza ungekuwa sawa kutoka kwenye bulb na sehemu zote zingefikiwa na mwangaza hata kama chumba kina ukubwa wa mita 50x50 mwangaza ungefika kila pahala na nguvu ile ile kama ilivyo mita mbili kutoka kwenye bulb.
Fikra vile vile hazisafiri fikra ni kitu kimefungwa ndani ya uwezo wa akili na uwezo wa akili ni information iliyo ndani ya akili tu,fikra haziwezi kufikiria vitu ambavyo havijawekwa ndani ya akili,kama fikra zinasafiri na zina speed yeyote zingekuwa zinakuja na mambo makubwa sana kwa muda mchache tu,yaani haya maendeleo yote ya dunia yangewezekana kwa pengine miaka mitano tu na sio miaka zaidi ya 5000 kama inavyosema historia,kama tukianza kupima speed ya fikrakiuhalisia basi fikra ni katika vitu vilivyo slow sana yaani slow kupita maelezo, ndio innovation yote duniani inachukua milele kukamilika,kila siku kunakuja mambo mapya ya kuongeza kwenye kila uvumbuzi duniani,kama fikra zina speed kila kitu kingekuwa kishatokea masaa machache baada ya uvumbuzi.
Chukulia mfano wa uvumbuzi wa simu,ilivumbuliwa zaidi ya miaka mia aliyopita na mpaka sasa bado tunafikiria kuongeza mabadiliko kwenye tasnia ya simu,kama fikra zina speed yote angekwisha julikana masaa tu baada ya uvumbuzi.