Unadhani Mwanga ndio kitu chenye spidi ya juu kushinda kila kitu? Vipi kuhusu hili jambo?

(Unahisi kipi kina spidi zaidi, Mwanga au Fikra

  • Total voters
    50
  • Poll closed .
Mwangaza ni kitu ambacho kinaisha mwishoni mwa uwezo wa chanzo kilichoanzisha mwangaza na hauna speed wala hausafiri,kama mwangaza unasafiri ungekuwa unasafiri milele bila ya kuwa na kikomo.kwa mfano ukiwasha taa mwangaza wake hausafiri ukaenda milele unaisha mwishoni mwa uwezo wa ile bulb,kama bulb ni watt 40 uwezo na duara la mwangaza litakuwa dogo,tafauti na kama bulb litakuwa 100 watt duara na uwezo itakuwa mkubwa na hapa hio safari ya mwangaza itaonekana kama ni kubwa lakini sababu ni nguvu ya chanzo cha mwangaza tu na sio usafiri wa mwangaza.

Kwa mfano Kama mwangaza unasafiri basi hata bulb ya watt 20 mwangaza ungekuwa sawa kutoka kwenye bulb na sehemu zote zingefikiwa na mwangaza hata kama chumba kina ukubwa wa mita 50x50 mwangaza ungefika kila pahala na nguvu ile ile kama ilivyo mita mbili kutoka kwenye bulb.

Fikra vile vile hazisafiri fikra ni kitu kimefungwa ndani ya uwezo wa akili na uwezo wa akili ni information iliyo ndani ya akili tu,fikra haziwezi kufikiria vitu ambavyo havijawekwa ndani ya akili,kama fikra zinasafiri na zina speed yeyote zingekuwa zinakuja na mambo makubwa sana kwa muda mchache tu,yaani haya maendeleo yote ya dunia yangewezekana kwa pengine miaka mitano tu na sio miaka zaidi ya 5000 kama inavyosema historia,kama tukianza kupima speed ya fikrakiuhalisia basi fikra ni katika vitu vilivyo slow sana yaani slow kupita maelezo, ndio innovation yote duniani inachukua milele kukamilika,kila siku kunakuja mambo mapya ya kuongeza kwenye kila uvumbuzi duniani,kama fikra zina speed kila kitu kingekuwa kishatokea masaa machache baada ya uvumbuzi.
Chukulia mfano wa uvumbuzi wa simu,ilivumbuliwa zaidi ya miaka mia aliyopita na mpaka sasa bado tunafikiria kuongeza mabadiliko kwenye tasnia ya simu,kama fikra zina speed yote angekwisha julikana masaa tu baada ya uvumbuzi.
Eti mwanga hauna spidi????
 
Me naona speed kali iko kwenye ubongo kutafsiri kitu.. Maana chochote unachokiona hapo hapo kwenye ubongo kinatambua hicho nn.. Ndio maana hata ukiangalia maandishi tuh utashangaa umeyasoma bila hata kutaka kuyasoma
 
Na unaweza ona vitu 100 kwa pamoja na vyote ukavijua bila hata kua na habar navyo... Kwa hio speed ya kuona na kutambua kitu... Ni kubwa zaid yaan haipimiki
 
Hapana.. Kitu chenye speed zaidi ni Gravity mkuu.
Gravity ina speed kuliko mwanga..ndio maana mwanga hua haukatizi kwenye black holes/wormhole. Mwanga ukifika kwenye black holes hua unamezwa maana pale kuna gravity kubwa

Time is just a speed, So ukiwa na speed kubwa unaweza kuBend muda. So scientist wengi wanajaribu kutengeneza wormhole zenye garvity kubwa kama zilizopo kwenye spaces.

Regarding Your example naamini nervous system ndio kitu chenye speed zaidi. (Stimulus----->>>Response)

Mchakato wake upo chini ya nano second, imagine sauti inavyopita kwenye vipengele vyote ndani ya sikio la nje hadi la ndani kisha kwenda kwenye ubongo kutafsiriwa na kurudisha majibu kua ulichosikia kinamaanisha kitu fulani. Its matter of nano second
Hapa ntakuuliza swali Gravity ipi Ulikua unamaanisha??

Dunia ina yakwake

Mwezi una yakwake

Na hivyo tunategemea bodies mbalimbali kwenye universe kuwa na gravity yakwake tofauti tofauti

Ni ipi sasa ambayo ina spidi kuliko mwanga
 
Point of view yangu ni hivi
Mfano ukivuta picha unatembea kwenye ngazi za great wall of china,hyo imagination ni byproduct tu ya neural activity ndani ya brain yako(literally) na kuipata hyo byproduct kuna inputs ulikuw nazo mfano picha/video ulizowah kuziona za great wall hii ni imagination tu na ukienda mbal zaid inakuw fantansy tu lakn kwenye normal sense wew upo stationary,ubongo wako upo stationary na hizo fikra zipo stationary
Sipingani kabisa na kile unachosema wewe kwa sababu ni fact, isipokuwa najaribu kukufanulia kile ninachomaanisha mimi ambacho in essence nacho pia hakipingani na kile unachosema wewe hapa. Labda ujaribu kurejea kidogo post yangu hii hapa #81 halafu baada ya pale, labda ndiyo tuweze kuendelea tena kama kutakuwa bado kuna chochote kutoka kwako
 
Mmoja azungumzie blachole na warmhole n vitu gan?
Kama Einstein alivyopenda kusema 'Imagination is more powerful than knowledge',tutumie thought experiment kupata picha black hole ni kitu gani

kila massive body ina ukanda ambao gravitational field yake inaishia,mfano gravitational field ya jua inaishia kwenye ukanda unaoitwa Oort cloud,vuta picha kitu chochote kinachojaribu kutoka nje ya huu ukanda kitavutwa na Jua,Unless kiwe na speed inayowez kuikimbia gravitational field ya Jua ambayo ni 615000 m/sec,hii speed inaitwa Escape Velocity
Formula ya Escape velocity ni ve=(2GM/r)½
ambapo G ni gravitationa constant,M ni mass ya hicho kitu(nyota/sayari) na r ni radius kutoka kwenye centre of gravity ya hicho kitu
ukiangalia formula utagundua kadri mass ya nyota au sayari inavyokuw kubwa escape velocity yake inakuw kubwa zaid
Kumbuka speed ya light ni 299 792 458 m / s kwa hyo mwanga wa jua unawez kutoka nje ya ukanda wa jua bila ya shida yoyote...Sasa vuta picha una kitu chenye mass mara 50 ya jua maana yake escape velocity yake itakuw kubwa kuliko speed ya mwanga,kwa hyo ata mwanga wa hicho kitu utashindw kuikimbia gravitational field yake

Black hole ni region kwenye universe ambayo ina gravitational force kubwa kiasi ambacho hata mwanga hauwezi kuescape,black hole nying inaaminika zimeundwa baada ya kufa kwa nyota kubwa sana,baada ya kifo cha nyota,mabaki ya nyota hyo yatakuw compressed na gravity yake yenyew na matokeo yake ndio hii region inayoitwa Black hole

Kwenye mfano wa jua tuliona jua ina ukanda wake unaoitwa Oort Cloud,hii black hole pia inakuwa na ukanda wake unaoitwa Event horizon,mwanga unapoingia kwenye hii horizon hauwez kuescape kwa hiyo kama utafanikiw kuingia kwenye event horizon utakutana na library kubwa ya kila mwanga uliowah kuwepo kwenye universe,kuanzia big bang kwa hiyo black hole ni kama kitabu cha kumbukumbu cha historia ya Universe

Ukishavuka event horizon hutokutana na kitu chengine chochote cha hyo black hole kwa sababu ya strong gravitational force,kila kitu kilichokuw kwenye ile nyota iliyokufa kimekuw compressed kwenye particle moja inaypoitwa singularity na hata wew utakuw compressed kwend kweny ile singularity lakini huu ni upande mmoja wa imagination
Upande mwengine wa imagination ni kitu kinaitwa rotating black hole,ambapo badala ya black hole ku compress to singularity ina collapse kuwa rapidly spinning ring,ikitokea umeanguka kwenye hii ring utawez kutokea upande wa pili wa hii ring ambapo kimahesabu huu upande wa pili utakao tokea inaweza kuwa universe nyengine tofaut na hii ya kwetu,kwa hyo unawez kutengeneza hole inayo act kama daraja kati ya universe moja na nyengine kupitia hii rotating black hole,hii hole ndio inaitwa wormhole
Kama wanasayansi wataweza kutengeneza kitu kama hiki laboratory maana yake mtu anaingia kwenye hiki kitu ataweza kusafir kwenda universe nyengine,atawez kurudi nyuma au kwenda mbela ya muda
 
Hii napingana nayo.

Ili upate speed ya kitu lazima utahitaji starting point na destination.
Kitu ambacho kwa mwanga kinawezekana ila kwa fikra ni ngumu kidogo.
Hivyo ili tuweze kumeasure thought speed itabidi tutumie speed ya fikra kuchakata taarifa mpaka pale utakapopata jibu.

Mwanga always uko na speed constant isiyobadilika.

Lakini fikra haziwezi kuwa na speed constant na sidhani kama kuna uwezekano wa kufikia light speed.

ili kujaribu kuprove hilo kwamba speed ya fikra sio constant.
Na sometimes inaweza kuwa slow zaidi ya bando la Airtel au gari lisilo na engine.

Mfano mdogo huu hapa

Unaweza ukaniambia

2,424,697,415,356 x 7,786,326,964,664= sawasawa ni ngapi?

Sidhani hata kama umesoma hizo namba, zisome kwanza.

Je fikra zako zitaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 Bila ya msaada wowote?

Bila shaka hakuna binadamu duniani anaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 kwa mara ya kwanza na ukapata jibu bila msaada wowote.

Lakini wakati huohuo ukisema 1+1= ngapi?
Bila shaka asilimia kubwa ya watu wote duniani wanaweza kujua jibu ya hiyo taarifa chini au ndani ya seconds.
Baada ya kuona tu hiyo taarifa tayari fikra zako zimeshachakata hiyo taarifa ndani ya some milliseconds.

Hivyo mpaka hapo tayari speed ya fikra sio constant.

Kuna mengi hapo katikati ila kitendo cha light kuwa na speed constant isiyobadilika under any circumstances tayari speed of light ni almost untouchable at everything.

So in my opinion speed of light wins.

Kingine ni kwamba
technically black hole haimezi mwanga.
Bali massive gravity ya blackhole inabend space.
Na mwanga unafuatisha na kuexist kwenye space hivyo black hole ikibend space then mwanga nao utabend in ili kufuata au kuendana na hiyo space curvature.

Anayeweza kuniprove wrong, kunikosoa au kunichallenge Aje.
General relativity
 
Unaposema elimu ya outer space and time sio uhalisia una maanisha nini? Au hauna macho ya kuona kwamba "jua liko pale na linatuangaza"? Au hauoni sayari hii uliyopo inayoitwa dunia? Au hauzioni nyota zilizopo angani? Au hauwezi kunote jinsi mwanga ulivyo na kasi ya kustaajabisha? (300,000km/s).Uhalisia huo unaouzungumzia ni upi?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Nnaposema elimu ya outer space and time na dunia haiendani na uhalisi nakusudi hivyo,kuwa haviendani na hali halisi hata kidogo,yaani ni vitu tafauti kabisa,hivi vitu sio rahisi kufahamu hasa baada ya kupata elimu si rahisi kuona uhalisi hata kama uhalisi upo mbele ya macho.

Jua naliona kama sote tunavyoliona na kama nlivyosema kuwa jua haliko mbali wala halipo outer space na kama jua lipo 53 million miles away tusingeliona hata liwe kubwa kiasi gani, macho yetu yana mwisho wa uwezo wa kuona,hayawezi kuona infinity kwa sababu tu kitu ni kikubwa sana au kina mwangaza mkali, kwa macho yetu 1 million miles ni zaidi ya infinity achilia mbali 53 million miles,hivi vitu sio uhalisi hata kidogo tufungue akili.

jua,mwezi,sayari, nyota vyote havipo outer space vipo karibu sana na ardhi na wala dunia siyo sayari, hayo mafunzo yote ya skuli sio uhalisi,dunia kuelea angani na gravity na vitu vyote hivyo sio uhalisi,wala sayari zote hakuna yenye ardhi au udongo kama ilivyo ardhi ya dunia, mkuu sitakwenda mbali sana ila kama nlivyosema kuwa hivi vitu si rahisi kufahamu hasa ukiwa na elimu ya skuli pekee na ufahari wa elimu ndio adui mkubwa wa ufahamu.
 
Sasa mzee utatrace vipi hio sauti wakati unaweza kuta hio energy ilishaenda hadi kwenye mkaa na nikapikia makande.

Sound imeenda kwenye electrical impulses thru masikio yangu mimi nikareact na ngumi..ikaja kifuani kwako ikaleta heat na impulses tena yani it's practically impossible kutrace sauti ya sekunde 2 tu nyuma maana sio kwamba sauti yooote inageuka kua aina moja ya energy no..inageuka kua aina tofaut tofaut na inasambaa all over
... hiyo law nimekuwa nikii-mind sana! Kwamba, the amount of energy in the universe is constant; just the form changes! Now, sound is a form of energy; if so, sauti zote zilizowahi kutokea duniani hazijapotea, pengine zimebadilika form tu. I believe, one day, wenye brains zao kuna siku wataweza ku-reverse sauti (zilizo katika form nyingine ya energy) back to their original sounds/forms.

In that regard, kuna siku (watu/kizazi kingine) watasikia mahubiri ya Bwana Yesu Kristo (live) na manabii maana sauti zao ziko tu somewhere in another form ni suala la kuzirudisha kwenye original form tu! Hata uhalifu utaisha maana yaliyojadiliwa sirini yatawekwa wazi kwa re-wind mazungumzo! Very important law indeed!
 
Ni kweli fikra ya mwanadamu ina speed kuliko mwanga, unaweza kwenda nnje ya galaxy yetu kwa hio sekunde, labda tofauti ije kwamba mwanga ni KITU, cha kuonekana kwa macho, na fikra ni HALI, isiyoonekana kwa macho
Imethibitishwa kuwa mwanga unasafiri kwa spidi ya km laki tatu kwa sekunde moja tu(300,000km/s), Yani kwa sekunde tu mwanga unaizunguka dunia mara Nane(08)

kuna nadharia nyingine(Hii sio yangu mimi,Lakini nimetokea kuisapoti kishingo upande)

NI HIVI:- Pengine Fikra ya mwanadamu ndio kitu chenye spidi kali kushindwa hata hup mwanga(sema imeshindikana kuthibitisha kisayansi)

Hebu chukulia mfano huu mwepesi:-

Mfano getoni kwenu mpo watatu(03) tu, na tuchukulie nyie mna mashati yakuvaa matatu tu(yaani kila mmoja wenu ana shati moja) la kuvaa {Kauka nikuvae }
Sasa hapo geto kuna MTU A(shati jekundu) MTU B(Shati jeupe) MTU C(Shati la manjano)
MTU A mwenye shati jekundu akaenda kazini halafu mida mida mwenzake MTU B Mwenye shati jeupe akaja kumtembelea getto-mate mwezake:: yani ukimuona tu na shati jeupe MOJA KWA MOJA utajua getto-mate C amevaa shati la manjano

Hv mmeweza kupata picha hapo jinsi spidi ya fikra ilivyo??

Hoja mezani,(Unahisi kipi kina spidi zaidi, Mwanga(A) au Fikra(B) )
Na uzi tayar
Kama ni fikra iko slow kurko mwanga,
Unaesema unaenje nje ya galaxy, utaendaje kifikra angar hujawah kufika
Pili macho yakiona ilo shati, ni mwanga umesafir mpaka jichon kwako na mpaka kwenye retina ikabadrishwa ili uwe umeme then unapita kwenye optical nerve ndo unabadrishwa tena kwenda kwenye akili then process za kutambua zianze'
Process za mwil ziko slow, sema mazoea ndo yanafanya udhan yako fasta, ukitak kujua ni dista ce yako na huyo mtu, lets say 3meters mpaka umtambue mwanga ushasafiri mara milion100, ukigawanya kupata mda ni mdogo sana kuringanisha na fikra, ata computer na processor zake zote haikarbii ata kidogo, ata chembe ya robo ya speed ya mwanga, usiongelee kuzunguka dunia ukadhan dunia ni ndogo kaka
 
Hii napingana nayo.

Ili upate speed ya kitu lazima utahitaji starting point na destination.
Kitu ambacho kwa mwanga kinawezekana ila kwa fikra ni ngumu kidogo.
Hivyo ili tuweze kumeasure thought speed itabidi tutumie speed ya fikra kuchakata taarifa mpaka pale utakapopata jibu.

Mwanga always uko na speed constant isiyobadilika.

Lakini fikra haziwezi kuwa na speed constant na sidhani kama kuna uwezekano wa kufikia light speed.

ili kujaribu kuprove hilo kwamba speed ya fikra sio constant.
Na sometimes inaweza kuwa slow zaidi ya bando la Airtel au gari lisilo na engine.

Mfano mdogo huu hapa

Unaweza ukaniambia

2,424,697,415,356 x 7,786,326,964,664= sawasawa ni ngapi?

Sidhani hata kama umesoma hizo namba, zisome kwanza.

Je fikra zako zitaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 Bila ya msaada wowote?

Bila shaka hakuna binadamu duniani anaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 kwa mara ya kwanza na ukapata jibu bila msaada wowote.

Lakini wakati huohuo ukisema 1+1= ngapi?
Bila shaka asilimia kubwa ya watu wote duniani wanaweza kujua jibu ya hiyo taarifa chini au ndani ya seconds.
Baada ya kuona tu hiyo taarifa tayari fikra zako zimeshachakata hiyo taarifa ndani ya some milliseconds.

Hivyo mpaka hapo tayari speed ya fikra sio constant.

Kuna mengi hapo katikati ila kitendo cha light kuwa na speed constant isiyobadilika under any circumstances tayari speed of light ni almost untouchable at everything.

So in my opinion speed of light wins.

Kingine ni kwamba
technically black hole haimezi mwanga.
Bali massive gravity ya blackhole inabend space.
Na mwanga unafuatisha na kuexist kwenye space hivyo black hole ikibend space then mwanga nao utabend in ili kufuata au kuendana na hiyo space curvature.

Anayeweza kuniprove wrong, kunikosoa au kunichallenge Aje.
Mada ilitakiwa ifungwe na jibu hili
Kuendeleza mada ni ukosefu wa adabu na ni dhuluma ya wazi ya mawazo kuntu ya mtoa jibu!
Binafsi hii mada imefika mwisho kwa jibu lako
Mwanga mwanga ndio baba lao
 
Imethibitishwa kuwa mwanga unasafiri kwa spidi ya km laki tatu kwa sekunde moja tu(300,000km/s), Yani kwa sekunde tu mwanga unaizunguka dunia mara Nane(08)

kuna nadharia nyingine(Hii sio yangu mimi,Lakini nimetokea kuisapoti kishingo upande)

NI HIVI:- Pengine Fikra ya mwanadamu ndio kitu chenye spidi kali kushindwa hata hup mwanga(sema imeshindikana kuthibitisha kisayansi)

Hebu chukulia mfano huu mwepesi:-

Mfano getoni kwenu mpo watatu(03) tu, na tuchukulie nyie mna mashati yakuvaa matatu tu(yaani kila mmoja wenu ana shati moja) la kuvaa {Kauka nikuvae }
Sasa hapo geto kuna MTU A(shati jekundu) MTU B(Shati jeupe) MTU C(Shati la manjano)
MTU A mwenye shati jekundu akaenda kazini halafu mida mida mwenzake MTU B Mwenye shati jeupe akaja kumtembelea getto-mate mwezake:: yani ukimuona tu na shati jeupe MOJA KWA MOJA utajua getto-mate C amevaa shati la manjano

Hv mmeweza kupata picha hapo jinsi spidi ya fikra ilivyo??

Hoja mezani,(Unahisi kipi kina spidi zaidi, Mwanga(A) au Fikra(B) )
Na uzi tayar
Speed ya Nerve impulse ni ndogo kuliko ya Mwanga yani ya Mwanga ni 300,000Km/s huku ya Nerve Impulse ikiwa ni 342Km/s..

Umetolea mfano wa shati na Mimi naomba nikutolee huu mfano..

*Kiwango ambacho huona ambavyo huona video inacheza kwenye Tv ni matokeo ya macho kushindwa kutofautisha picha zilizofuatana kuanzia kiwango cha speed ya picha 24 kwa sekunde yani 24fps..

Mpaka hapo utakuwa umeona vile kunatofauti kubwa Kati ya speed ya kuona ya macho na Mwanga..
 
Hii napingana nayo.

Ili upate speed ya kitu lazima utahitaji starting point na destination.
Kitu ambacho kwa mwanga kinawezekana ila kwa fikra ni ngumu kidogo.
Hivyo ili tuweze kumeasure thought speed itabidi tutumie speed ya fikra kuchakata taarifa mpaka pale utakapopata jibu.

Mwanga always uko na speed constant isiyobadilika.

Lakini fikra haziwezi kuwa na speed constant na sidhani kama kuna uwezekano wa kufikia light speed.

ili kujaribu kuprove hilo kwamba speed ya fikra sio constant.
Na sometimes inaweza kuwa slow zaidi ya bando la Airtel au gari lisilo na engine.

Mfano mdogo huu hapa

Unaweza ukaniambia

2,424,697,415,356 x 7,786,326,964,664= sawasawa ni ngapi?

Sidhani hata kama umesoma hizo namba, zisome kwanza.

Je fikra zako zitaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 Bila ya msaada wowote?

Bila shaka hakuna binadamu duniani anaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 kwa mara ya kwanza na ukapata jibu bila msaada wowote.

Lakini wakati huohuo ukisema 1+1= ngapi?
Bila shaka asilimia kubwa ya watu wote duniani wanaweza kujua jibu ya hiyo taarifa chini au ndani ya seconds.
Baada ya kuona tu hiyo taarifa tayari fikra zako zimeshachakata hiyo taarifa ndani ya some milliseconds.

Hivyo mpaka hapo tayari speed ya fikra sio constant.

Kuna mengi hapo katikati ila kitendo cha light kuwa na speed constant isiyobadilika under any circumstances tayari speed of light ni almost untouchable at everything.

So in my opinion speed of light wins.

Kingine ni kwamba
technically black hole haimezi mwanga.
Bali massive gravity ya blackhole inabend space.
Na mwanga unafuatisha na kuexist kwenye space hivyo black hole ikibend space then mwanga nao utabend in ili kufuata au kuendana na hiyo space curvature.

Anayeweza kuniprove wrong, kunikosoa au kunichallenge Aje.
Naomba nitofautiane na ww kidg,

Kwa nnavyo elewa, unapoona kitu mfano shati la njano (kama mfano wa mdau), maanake mwanga umesafiri kutoka hilo shati au chanzo mpaka retina ya jicho. Then cell hubadilisha miale kuwa kuwa signal ambazo ubongo hutafsiri na kukupa maana kuwa Teenager umeona shati la njano.

Sasa mwanga umetoka kwenye shati mpaka kwenye jicho. Fikra zimeanza ubongo ulipopata signal na kutafsiri na kukupa maana. Kwa namna fulani yote yanahusisha kiungo cha kuchakata(kuprocess).

Ishu inakuja pale kiungo hiki kinaposhindwa kutoa jibu sahihi, basi inaweza kuathiri speed.
Mfano; kwa mfano wako mimi naona sio kwamba fikra zimesafiri muda mrefu, ila ni kwamba zimefika ila jibu halijawa tayar, hivyo ubongo umekosa mrejesho sahihi uliouhitaji(jibu la hiyo hesabu yako) na kukufanya uhisi fikra hazina speed ya kutosha. In real sense hata kutambua kuwa hesabu ni ngum kwa kupitisha macho tayari fikra zimefikisha ujumbe.
Mfano 2: Mfano wa shati la njano. Kama hyo mtu angekuwa sehem ambayo haonekani vzr either umbo au shati, mtoa hoja asingeweza kumtambua. Kwa namna fulani unaweza tafsiri mwanga umechelewa na kufikinya macho uone vzr illa kumbe ubongo ndo umeshindwa kutafsiri picha sahihi.

Swali fikirishi 1: Kama mwanga unazunguka dunia kwa muda mfupi hvyo, vipi fikra zinazoweza kunipeleka utotoni na kunirudisha palepale nnapoulizwa swali na nikamjibu bila delay? Vipi zinavyoweza kunipeleka kwenye imagination za maisha ya zaman au yajayo pale nnaposoma habari za kufikirika?

Swali fikirishi 2: Kuna utofauti gani wa nerve impulse na fikra?
 
Back
Top Bottom