Unadhani Mwanga ndio kitu chenye spidi ya juu kushinda kila kitu? Vipi kuhusu hili jambo?

(Unahisi kipi kina spidi zaidi, Mwanga au Fikra

  • Total voters
    50
  • Poll closed .
Hii napingana nayo.

Ili upate speed ya kitu lazima utahitaji starting point na destination.
Kitu ambacho kwa mwanga kinawezekana ila kwa fikra ni ngumu kidogo.
Hivyo ili tuweze kumeasure thought speed itabidi tutumie speed ya fikra kuchakata taarifa mpaka pale utakapopata jibu.

Mwanga always uko na speed constant isiyobadilika.

Lakini fikra haziwezi kuwa na speed constant na sidhani kama kuna uwezekano wa kufikia light speed.

ili kujaribu kuprove hilo kwamba speed ya fikra sio constant.
Na sometimes inaweza kuwa slow zaidi ya bando la Airtel au gari lisilo na engine.

Mfano mdogo huu hapa

Unaweza ukaniambia

2,424,697,415,356 x 7,786,326,964,664= sawasawa ni ngapi?

Sidhani hata kama umesoma hizo namba, zisome kwanza.

Je fikra zako zitaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 Bila ya msaada wowote?

Bila shaka hakuna binadamu duniani anaweza kuchakata hiyo taarifa chini au ndani ya sekunde 1 kwa mara ya kwanza na ukapata jibu bila msaada wowote.

Lakini wakati huohuo ukisema 1+1= ngapi?
Bila shaka asilimia kubwa ya watu wote duniani wanaweza kujua jibu ya hiyo taarifa chini au ndani ya seconds.
Baada ya kuona tu hiyo taarifa tayari fikra zako zimeshachakata hiyo taarifa ndani ya some milliseconds.

Hivyo mpaka hapo tayari speed ya fikra sio constant.

Kuna mengi hapo katikati ila kitendo cha light kuwa na speed constant isiyobadilika under any circumstances tayari speed of light ni almost untouchable at everything.

So in my opinion speed of light wins.

Kingine ni kwamba
technically black hole haimezi mwanga.
Bali massive gravity ya blackhole inabend space.
Na mwanga unafuatisha na kuexist kwenye space hivyo black hole ikibend space then mwanga nao utabend in ili kufuata au kuendana na hiyo space curvature.

Anayeweza kuniprove wrong, kunikosoa au kunichallenge Aje.
Yap,always time changes with respect to velocity,kadri kitu kinavosafiri sawa sawa na spidi ya mwanga urefu lazima upungue to nothing,time slows down to a stop na uzito unakuwa infinite kitu ambacho ni illogical.Mpaka sasa nothing goes fast than speed of light.@Andrew Tate
 
Ona

Oneni

Fikra zipo nje ya muda, kwa hiyo hata kupima spidi yake ni absurd.

Niwaambie kitu kimoja kwa ambao bado mnataka kulinganisha spidi mazee? Ipo hivi;

Fikra katika spidi hatutaipa namba, tutaipa u 'instantaneous' ambayo kama ni namba basi ni infinity ambayo pia ni sawa tu na ziro.

Yas, spidi ni ziro kwa sababu kiukweli fikra hata haisafiri kamwe. Yaani fikra ikishawazwa mahala A ni muda huohuo hilo wazo lipo mahala B hadi mahala XYZ! Kwa hiyo fikra huwepo ulimwengu mzima mara baada tu ya kuwepo.

Kama fikra hiyo ina athari kwa mazingira iliyofikiriwa basi tutakachokiona ni kuanza, kuendelea na kuchelewa kwa mchakato wa matokeo ya fikra hiyo. Lakini fikra yenyewe imeshafika pote na katika yote.

Ndiyo maana FIKRA iliweka wazo la 'UWEPO MWANGA!' Pale palipokuwa na giza na kilichotokea ndio hicho mwanga ukawepo, sema kwa kuchelewa kwa spidi ya mwanga ndiyo maana hadi leo huo mwanga unasafiri katika duara (ever expanding cycle) katika mchakato wa kulibadili giza.

Mwanga una kasi ndogo kuliko FIKRA/WAZO na ninao uthibitisho wa hili🤔. Uthibitisho upo hukohuko katika kosmolojia na nadharia na majaribio kiasi sikiliza; Inafahamika kwamba hata leo ukianza kukimbia kwa spidi ya mwanga kujaribu kuukamata 'mwanga' wa kwanza katika pembe ya ulimwengu HAUTAKAA UUPATE!....... Tena hata ukifanikiwa kuukimbiza kwa kasi mara kadhaa ya mwanga bado hutaupata! Kwa nini? Ni kwa sababu mwanga huo unakimbia kwa spidi zaidi ya spidi ya mwanga na spidi hiyo inaongezeka (it is accelerating!).

Kitendo cha sayansi kusema spidi ya mwanga ni X, kisha hapohapo kusema tena kwamba kuna 'mwanga' una spidi zaidi ya mwanga na inaonesha inajiongezeka. Ni sawa na kusema kuna 'kitu' kingine kina spidi zaidi ya mwanga huko kwenye ncha ya ulimwengu (ambayo ni sawa na kusema kwenye mwanzo wa ulimwengu🤨. It is the same thing).

Hicho 'kitu' ndugu zangu wala sio mwanga tena. Hiyo ndiyo fikra ya mwanzo na ya mwisho na ya hata sasa. Yaani ya pote. NIKO (kule) ambaye NIKO (hapa pia). Fikra/wazo/idea ambayo imewakilishwa kwa NENO 'LET THERE BE LIGHT'.....

Fikra inayo kasi kuliko mwanga. Na kasi yake ni ukipenda sema infinity, ukipenda sema ziro/sifuri. Maana fikra ikishawazwa katika pointi yoyote ya ulimwengu basi inakuwepo ishafika pote.
NB: Kama nyongeza basi someni Quantum Entanglement. Quantum entanglement inawasiliana kati ya pointi tofauti kwa 'kasi' ya fikra yaani ziro/infinity. Zote hizi ni uthibitisho kiwa kuna 'vitu' vina kasi zaidi ya mwanga.

Nawaita wote;
Mufti kuku The Infinity
Andrew Tate dudus ZENJIBARIA Nibiru Abraham Lincolnn Pendaelli Kiranga Allency Waterbender Kapumpuli Fund man Makanyaga utali Samcezar Mjomba Fujo zous hypothalamus Watery Mawimba Amigoh uncle virus carnage21
 
Inaonekana haujui ukubwa wa spidi ya mwanga.... huo mda utakaotumia kufikiria kuhusu mshkaji wako ghetto, mwanga utakuwa umeshaizunguka Dunia zaidi ya mara 8
 
Ona

Oneni

Fikra zipo nje ya muda, kwa hiyo hata kupima spidi yake ni absurd.
Kwanini? Fikra ni nini? Nadhani tungeaza by definitions, utanipa yako ila yangu ni hii:
Fikra ni mawazo kuhusu jambo Fulani yanayotokea akilini baada ya kitendo Cha kufikiri.
Sasa, Kwasababu fikra ni wazo(idea) tu, basi Haliwezi kuwa na spidi maana wazo(idea) haliexist kwenye physical world Bali lipo kwenye mental/conscious space. ili kitu kiwe na spidi lazima kisafiri kwenye nafasi Fulani (ndani ya physical world) kwa muda Fulani.
Lakini Kwasababu wazo halichukui nafasi yoyote wala halitumii muda wowote basi haliwezi kuwa na spidi yoyote. (Ni sawa na kuuliza huzuni Ina spidi gani? Huzuni IPO kichwani tu haipo duniani physically, haionekani haishikiki)

Lakini Sasa usichanganye fikra na kufikiri... kufikiri kunatumia muda. Kufikiri ni kitendo Cha kutumia ubongo (mental gymnastics, neuronal coordination ,synapses,etc.) Kutengeneza fikra/wazo.

Kwasababu ubongo unafanya kazi kwa kutumia umeme kwenye neurons, na kemikali kwenye synapses basi hiki kitendo Cha kufikiria kinatumia muda na nafasi. Nafasi ikiwa ni ule umbali kati ya neourones zote zinazohusika kutengeneza fikra Fulani, na muda ni ule muda ambao umeme (kwenye axons), na kemikali (kwenye synapses) vinatumia kufika katika hizo circuits ili kutengeneza wazo Fulani.

Hivyo kufikiria kuna spidi maana kunatumia nafasi na muda. Spidi yake roughly tunaweza kuestimate itakuwa chini kidogo tu ya spidi ya umeme Ndani ya free liquid electrolytes. Ambayo kwa udogo wa size ya kichwa chakona ubongo wako unaona ni kama inafika instantaneous. Lakini trust me ungekuwa na kichwa kikubwa kama Dunia lazima ungenotice lag katika kufikiria.

Niwaambie kitu kimoja kwa ambao bado mnataka kulinganisha spidi mazee? Ipo hivi;

Fikra katika spidi hatutaipa namba, tutaipa u 'instantaneous' ambayo kama ni namba basi ni infinity ambayo pia ni sawa tu na ziro.
Hili nmeelezea hapo juu

Yas, spidi ni ziro kwa sababu kiukweli fikra hata haisafiri kamwe. Yaani fikra ikishawazwa mahala A ni muda huohuo hilo wazo lipo mahala B hadi mahala XYZ! Kwa hiyo fikra huwepo ulimwengu mzima mara baada tu ya kuwepo.
Uko sahihi fikra haisafiri, lakini sio kwa sababu hizo. Ni Kwasababu haipo kwenye physical world. Unatakiwa utofautishe kuhusu kitu na fikra kuhusu hiko kitu. Unapofikiria kuhusu Ubungo kwa mfano, fikra hazisafiri kwenda Ubungo na wala hazitoki kichwani mwako, Bali inabaki kama wazo tu ndani ya kichwa chako linalojaribu kuigilizia picha ya real world Ubungo palivyo. Hata details za fikra Huwa ni chache sana (<0.0000000000......00001%) kuliko reality. Mfano jaribu kuwaza kuhusu picha ya tembo(pause kidogo uwaze kuhusu tembo) tayari?.....hapo tayari imekuja picha kichwani ya tembo, lakini najua hujawaza kuhusu mikunjo kwenye magoti yake, umewaza kuhusu weusi wa kucha zake?, umewaza kuhusu unene wa mkonga wake?, umewaza kuhusu ufupi wa mkia wake? Umewaza kuhusu jinsia ya huyo tembo? Umri wake je? Na vipi umewaza mazingira aliyopo? Ni zoo au porini?
Umeiona? Mwanzoni ulitengeneza wazo kuhusu tembo lakini hukuinclude vitu vyote hivyo nilivyotaja, ila ukaendelea kuviongeza kwenye fikra zako kadri nilivyokuwa navitaja.
Nimefanya hivyo kukuonesha tu kuwa fikra zipo tu ndani ya kichwa na wala haziwakilishi asilimia kubwa ya uhalisia. Ni kama rough representation ya ulimwengu ndani ya kichwa chako.
Kama fikra hiyo ina athari kwa mazingira iliyofikiriwa basi tutakachokiona ni kuanza, kuendelea na kuchelewa kwa mchakato wa matokeo ya fikra hiyo. Lakini fikra yenyewe imeshafika pote na katika yote.
Natumai umeelewa ni kweli Fikra haijafika popote Kwasababu haiendi popote. Lakini kitendo kufikiri Kuna Mwanzo, mwendelezo na kuchelewa. Ndiyo maana huwezi kufikiria vitu 8000 kwa wakati mmoja. Vinapeana muda ndani ya working memory yako. Kuna vitu vinatumia muda kufikiria kuliko vingine, mfano ukiulizwa 1+1 utatumia muda mchache kufikiri kuliko ukiulizwa mwaka Jana mwezi huu ilikuwa wapi.
Ndiyo maana FIKRA iliweka wazo la 'UWEPO MWANGA!' Pale palipokuwa na giza na kilichotokea ndio hicho mwanga ukawepo, sema kwa kuchelewa kwa spidi ya mwanga ndiyo maana hadi leo huo mwanga unasafiri katika duara (ever expanding cycle) katika mchakato wa kulibadili giza.
Hapa umeenda kiimani zaidi na Mimi sitacomment, lakini utambue kuwa fikra zako Wewe binaadamu pekee haziwezi kutengeneza kitu chochote kwenye material world. Lakini unaweza kutumia mikono Yako physical kutengeneza kitu kwa kufuata direction ya Ile image kwenye fikra zako.
Mwanga una kasi ndogo kuliko FIKRA/WAZO na ninao uthibitisho wa hili🤔. Uthibitisho upo hukohuko katika kosmolojia na nadharia na majaribio kiasi sikiliza; Inafahamika kwamba hata leo ukianza kukimbia kwa spidi ya mwanga kujaribu kuukamata 'mwanga' wa kwanza katika pembe ya ulimwengu HAUTAKAA UUPATE!....... Tena hata ukifanikiwa kuukimbiza kwa kasi mara kadhaa ya mwanga bado hutaupata! Kwa nini? Ni kwa sababu mwanga huo unakimbia kwa spidi zaidi ya spidi ya mwanga na spidi hiyo inaongezeka (it is accelerating!).

Kitendo cha sayansi kusema spidi ya mwanga ni X, kisha hapohapo kusema tena kwamba kuna 'mwanga' una spidi zaidi ya mwanga na inaonesha inajiongezeka. Ni sawa na kusema kuna 'kitu' kingine kina spidi zaidi ya mwanga huko kwenye ncha ya ulimwengu (ambayo ni sawa na kusema kwenye mwanzo wa ulimwengu🤨. It is the same thing).

Hicho 'kitu' ndugu zangu wala sio mwanga tena. Hiyo ndiyo fikra ya mwanzo na ya mwisho na ya hata sasa. Yaani ya pote. NIKO (kule) ambaye NIKO (hapa pia). Fikra/wazo/idea ambayo imewakilishwa kwa NENO 'LET THERE BE LIGHT'.....

Fikra inayo kasi kuliko mwanga. Na kasi yake ni ukipenda sema infinity, ukipenda sema ziro/sifuri. Maana fikra ikishawazwa katika pointi yoyote ya ulimwengu basi inakuwepo ishafika pote.
NB: Kama nyongeza basi someni Quantum Entanglement. Quantum entanglement inawasiliana kati ya pointi tofauti kwa 'kasi' ya fikra yaani ziro/infinity. Zote hizi ni uthibitisho kiwa kuna 'vitu' vina kasi zaidi ya mwanga.
Okay hapa umeongelea mwanga. Ni kweli hakuna kitu kinaweza kusafiri through spacekwa spidi kuliko mwanga.
Hapo nimebold key words. Kitu na through space.
Kinachofanya mwanga uonekane unaaccelerate sio kwamba wenyewe ndiyo unaaccelerate Bali ni space unamosafiria ndiyo inaexpand kwa kuaccelerate.
Ni sawa muwe ndani ya basi pamoja na Usain bolt, ukasema kuwa humu kwenye basi hakuna mtu mwenye spidi kuliko Usain bolt. Hiyo sentesi itakuwa ni kweli. Lakini Hilo basi likianza kutembea kwa spidi kuliko Usain bolt, kwa mtu aliye nje atapona abiria wote mna spidi kuliko Usain bolt. Hata Usain bolt atakuwa na spidi kuliko Usain bolt.

Kwahyo kinachofanYa mwanga kwenye ncha za ulimwengu uoneakane una spidi kuliko mwanga sio kwamba kweli una spidi kuliko mwanga, Bali ni Ile space au nafasi ya huko kwenye ncha za ulimwengu inaexpand kwa spidi kubwa kuliko mwanga.
Ni kweli nothing can travel through space at a speed greater than light, but space itself can expand faster than the speed of light.
 
Fikra hands down, nipo New York right now lakini kila kitu nikifikiria hapo bongo nakiona live, lakini sina uhakika kama fikra zinapimwa kwa speed ya namna gani
Dar to New York ni km 12,000 tu,bado ipo chini sana
 
Speed inapimwa kwa Km per hour
Yaani how many distance covered per hour

Fikra unaipimaje sasa kuishindanisha na mwanga?

Fikra ni uwezo wa kupokea taarifa na kuzichakata....... hapa nadhani Chip za simu kompyuta zipo fasta kuliko fikra za binadamu
 
Kwasababu fikra ni wazo(idea) tu, basi Haliwezi kuwa na spidi maana wazo(idea) haliexist kwenye physical world Bali lipo kwenye mental/conscious space. ili kitu kiwe na spidi lazima kisafiri kwenye nafasi Fulani (ndani ya physical world) kwa muda Fulani.
Lakini Kwasababu wazo halichukui nafasi yoyote wala halitumii muda wowote basi haliwezi kuwa na spidi yoyote. (Ni sawa na kuuliza huzuni Ina spidi gani? Huzuni IPO kichwani tu haipo duniani physically, haionekani haishikiki)
Ndiyo.

Na katika maelezo yangu nilikubaliana na watakaoona kuwa huu mwendokasi wa fikra kuwa mkubwa sana (infinity) na watakaosema kuwa ni haupo (zero) wote wapo sahihi. Maana fikra iko na ridiculous speed ambayo mtu mwenye akili timamu akiikataa anakuwa hajayumba kinamna yoyote kiakili (sanity). Sahihi.

Hivyo kufikiria kuna spidi maana kunatumia nafasi na muda. Spidi yake roughly tunaweza kuestimate itakuwa chini kidogo tu ya spidi ya umeme Ndani ya free liquid electrolytes. Ambayo kwa udogo wa size ya kichwa chakona ubongo wako unaona ni kama inafika instantaneous. Lakini trust me ungekuwa na kichwa kikubwa kama Dunia lazima ungenotice lag katika kufikiria.
Kuhusu kufikiria, huo mchakato nnakubali ni wa polepole, una kasi inayoendana na miunganiko ya neva na mwendokasi wa kusafirisha taarifa katika neuroni na sinapsi hizo. Mchelewo upo sana tu hadi unafanya watu wajihisi kuwa na machale, hayo yapo sana tu

Kwahyo kinachofanYa mwanga kwenye ncha za ulimwengu uoneakane una spidi kuliko mwanga sio kwamba kweli una spidi kuliko mwanga, Bali ni Ile space au nafasi ya huko kwenye ncha za ulimwengu inaexpand kwa spidi kubwa kuliko mwanga.
Ni kweli nothing can travel through space at a speed greater than light, but space itself can expand faster than the speed of light.
So hayo ndiyo maelezo yako kuhusu huo mwanga uliopo nchani kuonekana unakimbia zaidi ya kasi ya mwanga sawa ahsante nimekusikia. Umekazia sana kwenye suala la nafasi ooookay🤔.

Sasa nnaomba 'uexplain away' issue yangu ya nyongeza. Issue ya quantum entanglement; ni kwamba ukichukua jozi moja ya 'kipande fulani' zilozoshikamana ukafanikiwa kuzigawanisha kisha ukazitenganisha kwa umbali wowote katika ulimwengu. Hapa weka nafasi kiasi chochote unachotaka. Na kitabakia 'fairly constant'. Ukifanya badiliko kwa kipande A hapohapo kipande B kitaitikia katika namna inayoendana na badiliko katika kipande A lililotokea. Na hakuonekani kuwepo na mchelewo (lag) wowote kati ya hayo matukio mawili!!

Na hakuna miale inayosafiri kwa kasi zaidi ya mwanga katika ulimwengu huu, achilia mbali kwa kasi ya kuwa mara moja (instantaneous). HAKUNA! Je hivyo vipande vimewasiliana vipi.

Mimi ndio nimeweka, hiyo ndiyo kasi ya fikra. HAPOHAPO, Infinity, Zero. Ipo hapa, na ndiyo iliyopo kule. Ova.

Again una haki ya kusema kuwa nimezungumza kiimani, kwamba mambo ya fikra hayapo katika physical reality eeeh. Lakini nikuonye kwamba; wakati huo wanasayansi wanajua kuwa atomu ndiyo mwisho wa maada, basi yeyote ambaye angezungumzia electroni na neutroni alikuwa 'out of the physical reality kwa muda! Achilia mbali huyo wa quaks na muons........... na sasa strings! Long long way down

........... Sasaa nikuache na swali la kujiuliza. Hivi unafikiri hicho wanachopima na kusema ni nafasi tupu (Majority of atom is empty space, majority of universe is space etc) unajuaje kama kesho keshokutwa ndio ukaambiwa hiyo ndiyo fikra, idea!!!!????? Stretch kidogo hapo. Pseudoscience anyone 🥴
 
Ndiyo.

Sasa nnaomba 'uexplain away' issue yangu ya nyongeza. Issue ya quantum entanglement;
Kwanza before sijajibu, nimeishia apa, hii statement imenifanya nicheke sana😂😂😂.
Anyways nkitulia ntareply 🤣🤣

But before Sija reply nilikuomba utoe definition ya fikra.
Maana huenda tukawa tunaongelea vitu viwili tofauti.
 
Ni kweli fikra ya mwanadamu ina speed kuliko mwanga, unaweza kwenda nnje ya galaxy yetu kwa hio sekunde, labda tofauti ije kwamba mwanga ni KITU, cha kuonekana kwa macho, na fikra ni HALI, isiyoonekana kwa macho
Bila utafiti na kuwekea dimensions analysis za fundamental quantities, basi ni heri useme hujui
 
But before Sija reply nilikuomba utoe definition ya fikra.
Maana huenda tukawa tunaongelea vitu viwili tofauti.
Maelezo yangu yanaenda na definition ya kwamba fikra ni wazo(idea) tu.

Ukitaka official definition ninayoenda nayo ni hii: fikra (wingi fikra) = wazo kuhusu jambo fulani. (TafsirihaririKiingereza: thought (en))

Wote hatuzungumzii mchakato wa kufikiri, bali ile bidhaa ya mwisho ya mchakato huo yaani lile wazo lililozaliwa, mfano 'Tembo mweupe' 'mwanga mzuri wa bluu'
 
Imo fikra is just an illusion....ndio maana hata einstein alikuwa na jeuri ya kusema kuwa time is illusion why ni kwasababu mwanadamu alifikiri anaweza akaenda beyond time I mean future au akarudi past but in real sense what we have is now....but mwanga ni kitu physical we can measure its distance and time taken in relative to its position...

kuna series inaitwa dark itakupa grasp kuhusu time ni ya kijerumani after ndio unaweza ukawekeza muda kwenye kuuelewa mwanga...I mean 4 dimensional space-time ambayo tunaipima kwa events
 
Back
Top Bottom