Unadhani hawajisikii vibaya?

Unadhani hawajisikii vibaya?

Takwimu za kukua kwa uchumi
Takwimu za kuongezeka pato la Taifa
Takwimu za kuanza kulipa deni la Taifa
Habari za kuhakiki watumishi hewa
Habari za kusitisha ajira nknk
Haya mambo yote haya ni kizungumkuti kwa kijana graduate asiye na ajira na mwenye kutegemewa na wazazi pale kijijini achilia mbali changamoto zake mwe
Dah
 
Afrika kuna shida kubwa sana, mwenye nacho haamini kama wengine hawana.
Hahahah sio Africa ila mwenye shibe huwa hamkumbukagi mwenye njaa hasa kwa sisi watu weusi!

Huwa majority wenye mafanikio huwa wanapenda kuoshea wengine ambao wako disadvantaged! Yani una struggle leo, siku ukitoboa unajisahau kuwa ulisotaga, basi umpe support ambaye anasotea mchongo aah wapi we unafurahia kuona anateseka na kumsindikiza na kejeli tu na kujiona umemaliza😅
 
Na nyie waajiri mnatumia sana loop hole hii kutunyanyasa sanaaa wafanya kazi kisa mmetupa vi ajira vyenu tunapata pesa ( na tunazipenda mno hela) ila mnatutesa sanaaa eti kwasababu kuna mamilion ya watu wana shida na kazi.
Kwakifupi hii kazi siipendi na kila siku nitagombana na bosi kwa kero zake akitaka kazi yake achukue tuu msitake kutuua kwa stress kisa mmetuajiri..
Pumbavu sana nyie
Yan inafika asubuh huna hata raha ya kwenda kazin.
Umefiw ila unaogopa hta kuomba ruhusa it is like u r commiting a crime.
Bosi akiingia ofis atmosphere yote ina change vicheko vinakata mnabaki kukimbia kimbia hata kama hamna kaz ya maana siku hiyo..unafik nafik tu na ubaguz mabos wana tengeneza makundi na ku force watu wawe machawa ili maisha yaende.
HELL NOO..
nalipwa 2.5m ila huu upumbavu na kazi wala siihitaji..kazi huna hata aman..It is kiliing the self esteem...confidence yote inaondoa kis boss..
 
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini

Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi

View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA

Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.

Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao

Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684

tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani
Chapisho hili ni la 2016, je 2021 hali ipoje
 
Bonge moja la dini lipo humu. Unasoma unaelewa unajionea huruma alafu unaacha.

Mi binafsi nmechagua kucheka tuu!!

Maana inaweza kufika mda unadhani umelogwa asiee.

Kumbe ni kipindi tuu ambacho ni laazma ukipitie.

Wacha tuendelee kula punje kama kuku huku tukiwa na matarajio makubwa kua kesho yetu haiwezi kua kama leo.

Marufuku kukata tamaa na kujifananisha na wengine.
 
Haya mambo yasikie kwa mwenzio tu, na mnyamapori anafurumukia sijui kichaka gani na mawenge yake anakuja kusema vijana wajiajiri mara siyo waaminifu wakati huo yeye kashikilia ofisi kwa miaka nenda rudi pumbavu kabisa.
 
Kuna kontena jingine linamwagwa ndani ya mwezi huu na ujao. Nawahurumia wadogo zangu wasio na anko kitengoni.
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827] May God prevail
 
Back
Top Bottom