Wajisiriamali eeh....Si mnaambiwa muwe wajasiriamali, kuweni wabunifu acheni kusubiri kuajiriwa
Tayari angalia post no#15 ila jaribu kumwelewa MKWEPA KODI kacheza tu na lugha ameongea kinyume nyumeWajisiriamali eeh....
Cc mshana jr naomba umjibu huyu mtu.
Hili swala linazidi kukua kwa Kasi. Sijajua tunaelekea wapiView attachment 411685Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini
Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA
Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.
Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao
Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANAView attachment 411684tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani
Takwimu za kukua kwa uchumi
Takwimu za kuongezeka pato la Taifa
Takwimu za kuanza kulipa deni la Taifa
Habari za kuhakiki watumishi hewa
Habari za kusitisha ajira nknk
Haya mambo yote haya ni kizungumkuti kwa kijana graduate asiye na ajira na mwenye kutegemewa na wazazi pale kijijini achilia mbali changamoto zake mwenyewe
Asante kwa kumjibu. hua wanadhani kwamba its an easy task to do kama kuteleza kwenye utelezi,![]()
![]()
nimecheza anga zote mbili..jaribu kuanzisha biashara yako leo hii ili ujikwamue kimaisha baada ya kukosa ajira uone mziki wake
Kupata tu nyaraka za kukutambua kama mjasiriamali unaweza kukata tamaa na kurudi kijiweni ukavute bangi
Michakato migumu kuanzia kupata mtaji mpaka kusimamisha biashara imewashinda wengi
Umenena lililo jema kabisa kwa siku ya leo munbu akubariki mkuu.Leo hii ukitangaza nafasi kumi za kazi turnover ya waombaji inaweza kukushangaza
Nakukumbuka ajira za uhamiaji kipindi kile waliojitokeza walikuwa elfu kumi wakati nafasi zilikuwa 70 tu
Kwa maisha haya ya sasa ukifanikiwa kupata ajira ipende ilinde na iheshimu
Kaka nlikuambia kua watakuja baadhi na kutoa kejeli zao kama huyo...ameshindwa kujibu hoja ya uliyoisema ameishia kusema vijana waisome namba...na ndio mawazo hayo hayo na serikali yao,
Mkuu Drc kaskazini ni Rahisi kupitia Rwanda,na kusini ni Rahisi kupitia ,Zambia,kati ni kupitia kigomaTuna shida kidogo kwenye vipaumbele vyetu kama kile cha kujenga reli kwenda Rwanda yenye watu milioni kumi badala ya kujenga reli kwenda DRC Congo yenye watu zaidi ya milioni mia moja
Ni wazi kuwa kila kimoja kina umuhimu wake lakini kwasasa nchi haina tatizo kubwa la usafiri wa anga! Pengine zile pesa za Bombardier zingetosha kujenga viwanda vidogo vidogo zaidi ya 20 na kuleta ajira zisizopungua 500...nina hakika ajira zitakazotokana na bombardier mbili haziwezi kuzidi miamoja nchi nzima
Vile vile ile project ya kuua upinzani nchini kupitia bwana yule na wengineo pesa yake ingetosha kujenga walau kiwanda kimoja cha matunda mkoani Tanga na kuzalisha ajira zisizopungua 100 kuanzia kukusanya kuuza kuprocess matangazo kutawanya na kuuza
Kwa njia hii tungewapunguzia vijana wengi stress za maisha bila ajira
Tuna shida kidogo kwenye vipaumbele vyetu kama kile cha kujenga reli kwenda Rwanda yenye watu milioni kumi badala ya kujenga reli kwenda DRC Congo yenye watu zaidi ya milioni mia moja
Ni wazi kuwa kila kimoja kina umuhimu wake lakini kwasasa nchi haina tatizo kubwa la usafiri wa anga! Pengine zile pesa za Bombardier zingetosha kujenga viwanda vidogo vidogo zaidi ya 20 na kuleta ajira zisizopungua 500...nina hakika ajira zitakazotokana na bombardier mbili haziwezi kuzidi miamoja nchi nzima
Vile vile ile project ya kuua upinzani nchini kupitia bwana yule na wengineo pesa yake ingetosha kujenga walau kiwanda kimoja cha matunda mkoani Tanga na kuzalisha ajira zisizopungua 100 kuanzia kukusanya kuuza kuprocess matangazo kutawanya na kuuza
Kwa njia hii tungewapunguzia vijana wengi stress za maisha bila ajira
Kujiajiri sio dhana rahisi kama inavyochukuliwa na wanasiasa...imagine wewe ni fresh graduate huna mbele huna nyuma huna chochote unaambiwa sio lazima kuajiriwa unaweza kujiajiriUtasikia mtu anasema mujiajiri sijui mtaji unaupata wapi? soko la mazao n.k
Naufahamu mkuu ngoja niutafute niuwekeDah umeandika kwa hisia sana.. Ungesindikiza na ule wimbo ameimba darasa na lina.. jina siujui ila ktk korasi Lina anaimba kila kunapokucha afadhali ya jana.... Au ule wa Bellah na Banana.
Wanadhan mkopo unatoka juu mbinguni ama kwenye miembe na michungwa kua unaenda tu kuchuma unabeba na safletUtasikia mtu anasema mujiajiri sijui mtaji unaupata wapi? soko la mazao n.k
Halaf hao wanaokwambia ujiajir wao wameng'ang'ania vyeoo wanastaaf ila bado wanataka waajiriwe kwenye vtengo tuuuuKujiajiri sio dhana rahisi kama inavyochukuliwa na wanasiasa...imagine wewe ni fresh graduate huna mbele huna nyuma huna chochote unaambiwa sio lazima kuajiriwa unaweza kujiajiri
Unapozungumzia kujiajiri unahitaji mtaji , nenda kakope bank uone