Mshana Jr dah hili andiko lako linahuzunisha sana ila linatia morali kwa vijana hasa kuamka na kuwaza ni kipi sasa kifanyike ikiwa ajira haijapatikana , umezungumza ukweli mtupu
Mara moja nilipata nafasi ya kufika mpaka wa Tanzania na Uganda yaani Mutukula , nilifika usiku sana kutokea bukoba mjini
Punde baada ya kufika ile nashuka kwenye gari nililokuwemo nilipata kushuhudia watu wengi wakiwa wamemzingira kijana wa makamo yangu , huku mwenye jiwe , mwenye fimbo na kila silaha waliyoweza kuwa nayo wakimpiga kijana yule ...
Huku wakisema wezi wamezidi mahali pale ila zaidi nikamsikia kijana mmoja akisema kwa leo nahisi huyu jamaa kapitiwa tu mpaka kuiba hiyo chupa ya mama ntiliye uwa si tabia yake , maana yeye uwa anapiga debe ,kwenye gari ziendazo Bukoba mjini na hela yake uishia kwenye pombe basi hiyo ndiyo furaha ya kijana yule.
Punde polisi wa Tanzania na wale askari wa upande wa pili walifika pale nakumchukua pale yule kijana ingali afya yake ikiwa imekatishwa tayari kwa kile kipigo .
Nilijikuta nalia usiku mzima punde baada ya kutajiwa jina la muhusika na kugundua ni jamaa tulikuwa wote chuo those years na pia alikuwa vizuri ila frustrations za ukosefu wa ajira zimempeleka akhera .
Hivyo hatuna budi kuendelea kuombewa hasa vijana kwa hali ya sasa ni ngumu na vijana tumekata tamaa .
Ila wengine tuliobahatika kuwepo mahali fulani kwa muda fulani embu tupaheshimu na kuwa na maono endelevu .
Bravo
Mshana Jr