Unadhani hawajisikii vibaya?

Unadhani hawajisikii vibaya?

Halaf hao wanaokwambia ujiajir wao wameng'ang'ania vyeoo wanastaaf ila bado wanataka waajiriwe kwenye vtengo tuuuu
Kuna wakati huwa naziona siasa ni kitu cha kipuuzi kabisa kisichoakisi ukweli wala uhalisia wa kile kimachohubiriwa majukwaani na kupigiwa makofi mengi
 
Nipo Kituo cha daladala hapa kuna tangazo la ajira na mshahara laki tatu sabini elfu kwa mwezi. Labda hii nayo inaweza kuwa fursa kwa we nye uhitaji wasting wakisubiria ajira ya ndoto yao!
 
Nipo Kituo cha daladala hapa kuna tangazo la ajira na mshahara laki tatu sabini elfu kwa mwezi. Labda hii nayo inaweza kuwa fursa kwa we nye uhitaji wasting wakisubiria ajira ya ndoto yao!
Hao jamaa ni matapeli na sijui kwanini serikali inawafumbia macho labda ni kwakuwa inawasadia kupunguza pressure ya ishu za ajira
 
Kuna mwaka nilienda kuomba field halmashauri moja hapa dar,kufika nkamkuta mama mtumzma akaambiwa na mwenzie akija bwana nanii mwaambie huyu dada apeleke barua yake..basi yule mama alinuna mpaka anakuja yule bwana hakunambia ikabidi nikisie ndo huyu nkaenda..Mpaka hapo nikaamini kweli waliokalia viti ndo wanafanya wenzao wengi wakose ili wao ambao elimu yao ya zaman waendelee kuwepo tena waweke na nduguzao wasio na vigezo.
 
Mkuu Drc kaskazini ni Rahisi kupitia Rwanda,na kusini ni Rahisi kupitia ,Zambia,kati ni kupitia kigoma
Utaona wazi kabisa hii ya Rwanda itarahisisha kubeba mizigo ya Goma na kivu ya kaskazini
Kwaio huoni kuwa janga la ajira litazidi kuongezeka kwa hy reli? Fikiria kuna magari makubwa mangapi yanayopeleka mizigo huko na watu wanaoziendesha kupata kipato cha kuendeleza familia zao? Naona watakuja mitaani.
 
Kaka mshana hata hiyo reli iliyopewa kipaumbele nayo ni janga kubwa sana kwa upande wa ajira. Kwa mtazamo wangu waliokuwa kwenye ajira za kuendesha magari makubwa ni wengi sana kuliko hata taasisi za serikali fikiria kuna maroli mangapi? Tanzania hii inapeleka mizigo huko nje? Je mizigo hiyo ikibebwa na treni hayo maroli yatabeba nini? Yatakuwa hayana kazi za transit kwaio madereva na matan boy wao nao wanakosa kazi watakuja mtaani
 
Umeniwazisha sana mkuu, mshana jr ! Mungu wewe mkuu sana, itazame kila nafsi ya mmoja wetu!
Tunapopita mitaani asubuhi kwenda kazini na tunaporudi jioni wale vijana walioko vijiweni yale macho yao yanayotuangalia ukiwa makini kuyaangalia yanaongea mengi sana na kwa sehemu kubwa yamejaa maumivu
 
Tuna shida kidogo kwenye vipaumbele vyetu kama kile cha kujenga reli kwenda Rwanda yenye watu milioni kumi badala ya kujenga reli kwenda DRC Congo yenye watu zaidi ya milioni mia moja
Ni wazi kuwa kila kimoja kina umuhimu wake lakini kwasasa nchi haina tatizo kubwa la usafiri wa anga! Pengine zile pesa za Bombardier zingetosha kujenga viwanda vidogo vidogo zaidi ya 20 na kuleta ajira zisizopungua 500...nina hakika ajira zitakazotokana na bombardier mbili haziwezi kuzidi miamoja nchi nzima
Vile vile ile project ya kuua upinzani nchini kupitia bwana yule na wengineo pesa yake ingetosha kujenga walau kiwanda kimoja cha matunda mkoani Tanga na kuzalisha ajira zisizopungua 100 kuanzia kukusanya kuuza kuprocess matangazo kutawanya na kuuza
Kwa njia hii tungewapunguzia vijana wengi stress za maisha bila ajira
 
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini

Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi

View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA

Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.

Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao

Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684

tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani

Mshana (doto)
Umetoa Maelezo ambayo yanaumiza sana fikra za watu sana hasa kwa watanzania. Gavana wa benki yetu ametoa report za kukua kwa uchumi kama ulivyoeleza.

Mie nina mtizamo tofauti wakifikra na wewe. Kwa maelezo yako inaonesha kwamba unategemea serekali ndio ilete maisha bora kwa watanzani, Viongozi wetu hawana utashi wa kweli kuwahudumia wananchi nia yao ni kwa ajili ya matumbo yao na familia zao, fikiria kidogo tu wewe unalipa payee kiongozi halipi,

Unakatwa Mafao leo wanaleta sheria ya kwamba mafao yako yakajenge viwanda hela utaipata ukifikisha miaka 65, wao hio sheri kwao haitumiki 5 years wakimaliza hela wanachukua bila makato. hivyo basi mfumo wa maisha kwa dunia nzima ni waudanganyifu na kukatisha tamaa sana.

Cha Msingi ni kubadili mtizamo tu, kufanya kazi kwa bidii na kwa malengo kwa wale walioajiriwa watambue hiyo kazi ni daraja la kumpleleka kwenye kazi za kujiajiri. kwa wale majasiriamali ni kujitahidi kwa bidii kufanya kazi sana ili uwe na maisha bora bila kuilalamikia serekali yetu sikivu..
 
Back
Top Bottom