Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,399
Kaka ulitumia hapa juu maneno 88.Kiswahili ni Kibantu at large percent na kilikwepo hata kabla ya kuja kwa Arabs.
Percent ya Waarabu katika lugha sio kubwa kuzidi percent ya Bantu languages katika kiswahili. Pili kilikwepo kabla ya Arabs kuja na hata wao wamesema katika documents zai kuwa Azania ilikuwa na Lugha moja kutoka katika branches za tribal languages.
Hatuwezi kusema kiswahili ni kiarabu kwa sababu ya uwepo wa maneno ya kiarabu. Kila lugha ina words kutoka lugha nyingine especially when a new item or object is new to another language au popularity yake.
Kati ya maneno haya uliona vema kuingiza maneno 26 ya Kiingereza (sijui kama ni dalili ya ubora au uhaba wa elimu?).
Maneno 62 ni Kiswahili. Kati ya hayo ni maneno 48 yenye asili ya Kibantu, na 14 yenye asili ya Kiarabu.
Hakuna aliyesema Kiswahili ni Kiarabu ila tu Kiswahili kwa bahati nzuri ni kati ya lugha zilizotokea kwa kuathiriwa na lugha ya nje (yaaniKiarabu) na hivyo hadi leo zenye uwezo wa kupokea maneno ya nje kirahisi. Hapo kinafanana na Kiingereza kilichanza pia kama lugha ya Kigermanik (kama Kiholanzi, Kijerumani) kilichopokea maneno mengi sana kutoka Kifaransa / Kilatini. Mimi naona lugha za aina hii zinakua kwa upesi kushinda lugha nyingine ambako wasemaji wanavutana zaidi kuhusu "usafi" wa lugha.