Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Vita vinavyoendelea mpaka kufikia leo vimepitia hatua nyingi na za wazi.Kila mwenye kuelewa alielewa kilichopangwa kutokea.Hii ni kwa vile vita hivi kati ya Israel na wapalestina vimepiganwa katika namna za kisasa tofauti na vita vilivyotangulia vya mwaka 148 na vile vya Yom Kipur vya mwaka 1973.
Kipigo ilichopata Israel kutoka kwa Hamas oktoba 7 kilikuwa kiko wazi sambamba na hasira za Israel kama ilivyoonekana kupitia viongozi wao wa kisiasa.
Kingine kilichoonekana wazi ni makamio ya kulipiza kisasi na matayarisho yake.Kama ni umuhimu wa kutaka kuwatetea wapalestina basi ulionekana kwa mara nyengine kupitia uungwaji mkono wa makamio ya Israel kutoka kwa mataifa makubwa yenye mafungamano na taifa hilo.
Viongozi wa nchi kadhaa marafiki wa Israel walionekana kuhamanika kwa kwenda huku na huko kwa madhumuni mawili.Kwanz kuiunga mkono Israel kwa maneno na vitendo na upande wa pili kuwasisitiza waungaji mkono wa Palestina kwamba waiingilie katika vita hivyo kwa maelezo kuwa vita hivyo visije vikapanuka na kuwa vita vya eneo zima la mashariki ya kati.
Kwa mtu ambaye hana udhaifu wa kiakili na ambaye si mnafiki basi angekuwa makini kuweka masharti yake ya kujizuia kutoingilia kati huko kulikohimizwa na marafiki wa Israel.
Hayo yote yalikuwa ni maandalizi ya vita.Ilikuwa ni madogo kuliko yale yaliyoanza kuonekana mwanzoni mwa vita na mpaka kufikia leo.
Wakati waislamu wamehimizwa kuhurumiana na kujitolea kuwahami wale madhaifu wanaoonewa.Lakini inaonekana mafunzo hayo yanaingia sikio hili na kutokea sikio la pili.Watu wameuliwa kwa maelfu tena kwa njia mbaya ya kuporomoshewa majengo mazito au kuchomwa na moto wa mabomu.Hayo yote yamefanyika kwa watoto na wanawake zaidi na bado hakukuwatia huruma viongozi hao wa nchi za kiarabu.
Tukiangalia mifano na ukubwa wa unafiki huo tunauona kwa nchi tatu zaidi nazo ni Saudi Arabia,Misri na Jordan
Saudi Arabia : Ipo taarifa kuwa mwanmfalme Mohammed Suleiman mara baada ya kuchukua madaraka aliwahi kuwazodoa Hamas na wapalestina kwa jumla kuwa yanayowakuta ni shauri kwani wanatakiwa kukubaliana na mipango ya Israel
Tangu kuanza kwa vita hivi vya Oktoba 7 wamekuwa wako doro sana katika harakati zao za kuwaunga mkono Hamas katika nia ya kukomboa maeneo yao au angalau kuwakemea Israel wasitekeleze azma yao ya kupambana na Hamas
Katika kiwango cha juu cha unafiki wa Saudi Arabia ni kutungua kombora lililorushwa na Houth wa Yemen hapo juzi likielekea kusini ya Israel.
Jordan: Ni nchi yenye mafungamano ya kidugu zaidi na wapalestina kuliko nchi nyengine yoyote ile kwani 80% ya watu wake wana asili ya Palestina.Zaidi ni kuwa eneo la Jerusalem kwenye msikiti wa tatu kwa utakatifu wa Alaqsa,eneo hilo liliporwa kutoka kwao mwaka 1967.
Vita hivi ingekuwa ni fursa kwao kuwafungulia raia wake kuingia Jerusalem kwa namna yoyote wangeona inafaa.Wangefanya hivyo kama vile ambavyo wayahudi kwa kusaidiwa na jeshi la Israel limetumia fursa ya vita hivi vipya kuendelea kunyang'anya maeneo ya wapalesitna yaliyobaki huku wakiwauwa kwa visingizio mbali mbali na kuwaharibia mali zao.
Misri:Ndio nchi pekee ya kiarabu ambayo imepakana na Gaza.Watu huku wakiangamia kwa kuuliwa lakini pia wamekatiwa mahitajio muhimu ya kibinadamu kama chakula,maji na nishati za umeme na mafuta.
Katika hali hiyo huruma ya kibinadamu tu ingefanya nchi hiyo ifungue mpaka bila kushauriana na yoyote.
Kinyume chake viongozi wa nchi hiyo wamekuwa wakiilaumu Israel kwa kutokuingia kwa misaada iliyorundikana mpaka kama ndio sababu ya mahitaji hayo kutoingia Gaza.
Lawama hiyo imeonekana kama ni kula njama na Israel ili ifanikishe mipango yake kwani kituo cha mpaka wa Rafah hakiko Israel na upekuzi wa malori uliolalamikiwa hufanyika kilomita 62 ndani ya ardhi ya Misri.
Tukiendelea kupembua unafiki wa nchi hizo tunaweza kuwakuta Iran kwa kiasi kidogo na Syria. Mfano Pentagon ya Marekani imesema nchi hiyo iko mbioni kuwapelekea Hizbulah mifumo ya ulinzi wa anga. Kama ni kweli uamuzi huo utakuwa ni wa kushangaza kwani wenyewe wamekuwa wakipigwa na Israel wanavyopenda na bila kuwachokoza.Wangetumia mifumo hiyo kujilinda wenyewe kabla ya kufikiria kuipeleka Lebanon kwa Hizbulah.