Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

Kama sio Putin, hivi Bashar angekuwa marehemu kama Gaddafi. Russia alishasema, Historia ya Libya haitajirudia kwa Syria. Na itatumia njia yoyote kuondoa ISIS. Mataifa ya magharibi yakivamia hivyo vitakuwa ni vita kabisa.

This is very stupid. Kwanini Marekani na wapambe wake waamulie kufanya watakavyo Syria? Kwanini watoe support kwa ISIS? Yaani wanawapa terrorists na mercenaries support kwa kuwalipa na kuwapa silaha? Halafu hawataki hata kusikiliza serikali ya Syria na wanaidharau.

Hivi sasa anga la Syria lipo chini ya Russia. Na Urusi imefutilia mkataba wa kutumia Nuclear kwa amani wiki iliyopita hivi sasa inafanya itakavyo. Kinachofuata sio Peace. Western waamue moja, vita au wakubali kuachia Syria ifanye maamuzi yake na sio kuleta kama walichofanya Libya na Iraq.
Putin amewashtukia hawa watu wa magharibi wanataka wamtawale na kumwamulia wanachokihisi kina maslahi kwao ndio maana ule mkataba ameuvunja na kuwataka Marekani na umoja wa Ulaya kumlipa kwa muda wote aliutumikia ule mkataba.

Ni wapumbavu sana hawa jamaa wanapotumia njia ya pembezoni kuchochea vurugu katika nchi mbalimbali
 
Then wakimbizi wakianza kwenda nchini mwao wanawawekea vikwazo huku wakisahau kuwa wao ndio chanzo cha arise mapigano sehem mbalimbali duniani
Kwakwe haijalishi bhanaaaaaa, ila anataka kuwaonyesha hao makulumbembe kuwa wababe wenzie wapo......
 
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ni chombo cha mabeberu cha kufanikisha mambo yao. Kinachowaumiza siyo taabu za Wasyria Bali ni kwa sababu malengo yao ya kumg'oa Assad hayakutimia. Na kikwazo ni Urusi na Iran. Ni Yale Yale ya Iraq na Libya.
Hawajui kuwa wameshtukiwa na Russia na Iran ambao hawataki kuona wengine wakiendelea kuonewa.
 
Jana Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Taifa ndiye aliwapasha vizuri Waingereza alisema tatizo lao bado wana Colonial Mentality - binafsi naona tatizo hilo hata Wafaransa wanalo sana.

Tukumbuke Syria iliwahi kuwa koloni la Ufaransa hawampendi Asaad lakini anaye vuta strings na Amerika, wanatumia Ufaransa kujaribu kumzuga Putin kumbe mwenzao kesha wasoma siku nyingi ndio maana mjumbe wa Ufaransa aliye kwenda Klemlin kuonana na,Putin na kumpa mapendekezo ya Ufaransa ya kusitisha mapigano, Putin hakumpa Mfaransa huyo jibu la moja kwa moja Urusi ilisubiri kutumia kura yake ya trufu kuzima njama za Ufaransa na Merikani.

Mimi kinacho nidhangaza kuhudu nchi hizi za magharibi specifically Ufaransa,Uingereza na kinara wao Uncle SAM ni kule kupuuzia hatari zinazo letwa/sababishwa na Ugaidi Duniani wanajali maslahi zaidi kuliko usalama wa raia wzo na mali zao
Hii nakubaliana na wewe kuwa mataifa mengi ya magharibi yana hyo mentality nikirejea juzi tu hapa Belgium ilivyolizungumzia suala la mgogoro wa Congo kuhusu masuala ya kusogeza mbele uchaguzi kana kwamba hawa watu hawana mamlaka yao inayowaongoza. Hili pia kwa Ufaransa nao nimeliona katika mgogoro huu pia
 
China na yeye huwaga ni snitch tu, sijui mpk aje awekewe no fly zone kwake ndo ataelewa umuhimu wa kua na msimamo
china kawekeza pesa nyingi sana marekani,kwahiyo ana maslahi nao na hataki kuonekana wazi kuwa anampinga marekani,lakini ukweli ni huo kuwa wako pamoja na Russia,kama kikinuka makombora ya mchina yataelekea newyork.

Mrussia yeye keshaweka wazi,HIT ASSAD,HIT RUSSIA....
 
getty-putin-obama.jpg

"Smooth operator" raisi Putin akijaribu kutoa mkono wa salamu kwa raisi Barak Obama.

Mkuu Malcom Lumumba heshima yako.

Hii haitakuwa "Cuban Missile Crisis" ingine maana ile ni historia nzuri sana.

Jambo la msingi kabisa kufahamu ni kwamba sasa hivi Russia wanawazidi nguvu waasi walipo mashariki mwa mji wa Aleppo ambao wanasaidiwa na Marekani na nchi za magharibi ambao lengo lao ni kumtoa raisi Assad.

Pia ndiyo umesikia John Kerry anaanza kudai kwamba Russia watashtakiwa kwa war crimes yaani wameua watu wengi waso na hatia huku ikieleweka wazi kwamba magaidi wanakuwa imbedded na wananchi wa kawaida hivyo kufanya kazi ya majeshi ya Syria na Russia kuwa hawana choice bali ni kutungua tu, hiyo moja.

Mbili, ni kwamba Marekani inaisaidia Saudi Arabia kupiga mabomu nchini Yemen na tumesikia watu karibu 10,000 wamefariki na UN aimeionya Marekani kwa kuwasaidia Saudi Arabia kwa ndege zake za kivita.

Hii pia inawafanya Marekani pia kuweza kushtakiwa kwa war crimes vilevile kwa kuwasaidia wasaudi kuua watu waso na hatia huko Yemen.

Sasa nikirudi kwenye masuali yako manne:

1. Mataifa ya magharibi hayawezi kujifunza na hayako tayari kufanya hivyo kwasababu hii ni vita ya kuhusu nani ana eneo lake la ushawishi katika mashariki ya kati na rasilimali zilizoko hapo khasa mafuta na gesi.

Hii inaenda sambamba na uhalisia kwamba tayari watu wa Syria ambao wanataka kuongoza nchi hiyo wakiwa vibaraka wa Marekani na nchi za magharibi nao sasa hivi wapo desperate kuona kwamba mpango wa kumwondoa Assad unakamilishwa haraka iwezekanavyo na hii inafanana kabisa na hali ilvyokuwa kule Libya.

2. Wakivamia Syria wataongeza magaidi kwani wale walipo tu wanatosha kuleta matatizo kwa nchi zote za mashariki ya kati. Ikumbukwe si tu ISIS bali pia kuna Al-Nusra na ALqaeda ambao wamesambaa hadi huko Yemen.

3. Kuna mada moja nimechangia nikitaja "nchi ya tatu" kwamba ndiyo iliyo nyuma ya Marekani katika mpango wake wa kujizatiti kwenye ubeberu wao katika eneo la Mashariki ya Kati, hivyo tunamweka Israel pamoja na Marekani na nchi za magharibi.

Iran wao wapo nyuma ya Russian kwani wakiwa wao ni washia hawatapenda kuona kabila la sunni ndilo linatawala Syria kama wanavyotaka kumwondoa Assad.

4. Mataifa ya magharibi hayawezi kuivamia Syria kama walivyofanya Libya kwani Russia tayari ametoa onyo la kutoshambulia majeshi ya Syria ambayo yapo kwenye vituo vya kijeshi ambavyo vimejengwa na Russia.

Hivyo inaonekana itaitwa round ingine UN kupitisha azimio bila kura ya Russia ambapo jambo hilo pia ni gumu kulitekeleza.
Umeeleza vzur lakin napenda usahihishe kidogo,hakuna kabila la washia wala sunni.hayo ni madhehebu ndan ya dini ya kiislam.
Kinachoendelea syria sio cha kufurahia,unaweza ukawa ndio mwanzo wa ww3.mvutano uliopo sio wa bahati mbaya ni planned ili ww3 izuke na ipiganwe ndani muda mfupi ila yenye madhala kiasi cha kuangamiza karibu robo 3 ya wakazi wa dunia hii US na washirika wake washinde then NWO.mmoja wa waandaji wa namna ya kufikia malengo ya mpango wa Nwo wa mpango huo Albert pike alishatabiri vita hii.tusishabikie ulimwengu upo kwenye kiwango cha juu chs hatari kuliko wakati wowote tangu kwisha kwa vita barid.wataangamia wengi.
 
China na yeye huwaga ni snitch tu, sijui mpk aje awekewe no fly zone kwake ndo ataelewa umuhimu wa kua na msimamo

Si hawa hawa ndiyo hao hao mnaosemaga watawakingieni kifua pindi mvamiwapo?...😀😀😀.mmeingia cha kike!
 
Dunia imegawanywa kiitikadi sehemu kuu mbili japo zipi 3,yaan nchi za kijamaa na nchi za kipepari,mgawanyiko huu ulijitokeza zaidi baada ya WW1 na mapinduzi ya Urusi(bolshevic revolution)ambapo V.Lenin alichukua uongozi na kufutilia mbali uongozi wa emperor/Tsar Nicolas II na kuunda serikali ya kikomunisti wakufuata mawazo ya kimax.itikadi hii ilikumbatiwa na vyama vingi vya kimapinduzi na wana mapinduzi wengi ktk nchi nyingi hasa zilizokuwa zinabinywa na mataifa makubwa ,baada ya WW2 makoloni mengi yalipata uhuru kuanzia bara la Africa mpaka Asia mfano China (mao),vietnam chini ya (Ho chi minh)na Angola.Hapo ndipo dunia inagawika mapande mawili makubwa kiitikadi magharibi wakiongozwa na marekan mashariki wakiongozwa na Ussr.kambi ya magharibia inadhindana na kambi ya mashariki chini ya viranja USA na mjomba mwingereza wakiongoza kambi ya magharibi kule Urusi na china.ndipo mwanzo wa vita barid katka harakati za kila kambi kujitanua na kijirinda dhidi ya kuhujumiwa na kambi pinzan,mwisho ilionekana kama Kambi ya Magharibi imeshinda pale ukuta wa berlin ulipoanguka ukitoa taswira mwisho wa utengano kusambaratika kwa USSR lkn vita imeanza upya.Hawa master wao ni mmoja uku kupishana, kupingana na kupingana ni utekelezaji wa mipango ili kufikia marengo ya master wao.lengo moja
 
The issue sio kutangaza kwa influence, ni kutangaza bila influence ya western propaganda. Propaganda in a media its common but isizidi to the extent. If you want to get a clear picture, don't rely sehemu moja ya informations iwe RT, ABC or any channel. Mfano kikao cha Leo cha China kuzungumza mpango wake, media za US hazijasema kwa sababu juzi zilikuwa zinasema something different. Dont you want to say kuwa hawajui hicho kikao, why its taking time?

Whats my concern sio propaganda ya mmoja, its a balance of power.

Pantheon Apollo,
Never argue with a fool, he will take you down to his level and beat you with experience.
 
Russia hawezi kukubali kuchezewa tena na mmarekani,Marekani alizoea vya kunyonga.
Baba wa dunia amerudi ( peace maker) RUSSIA.
Hajawahi kufanya nchi yoyote koloni lake duniani
Hajawahi unga mkono ushoga
Hajawahi chonganisha mataifa ya wenzie.
Hajawahi wachokoza wamarekani ( mwenyewe ndo humchokoza)
Analinda amani ya kweli ya dunia.
RUSSIA NDO FATHER
RUSSIA BABY
RUSSIA BABY.
 
kwenye huu uzi Urusi imeutumia vizuri udhaifu wa Obama tulijadili hii ishu kutokea.
upload_2016-10-11_0-50-59.png

lakini kwanini nchi za magharibi walete mswada wanaojua Urusi wataukataa kwa VETO? wanakusanya ushahidi ili waje kusema walifanya yote wawezayo? au kuna kitu wanataka huko mbele hivyo wanajenga mazingira ya kutokataliwa na Urusi wakiamini ni vigumu kukataliwa mara nyingi (gambler's fallacy)
 
Wafanyabiashara wapi jamaa waoga tu, kipindi kile Tanzania ina anza kuzinguana na Malawi ile issue ya Ziwa, China ikatoa bonge la statement ooh Tanzania ni rafiki yetu wa Kihistoria na tutahakikisha yuko salama na hakuna atakeye mgusa leo Huko Syria ameona mziki mkubwa wa Usa+Nato kabidi ajifiche nyuma ya UFANYABIASHARA
anasubili kura za baraza la usalama ambapo zitaijadili urusi ndio aseme hapana.mrusi amechanga karata amemuweka mchina km mtaji wa dharula.pale baraza litakapoitaji kumjadili mrusi. kistratejia anawapa mtihani marekani na wenzake kuhusu msimamo wa china
 
Hakuna watu wanafiki kama hawa wazungu.Hivi majeshi ya nchi za magharibi yameua raia wangapi katika maeneo mbalimbali dunia hii?drone attacks zimeua watu maelfu ila nafsi haziwaumi alafu ishu za assadi ndio wanaona zinawakera.Unafiki mtupu
 
anasubili kura za baraza la usalama ambapo zitaijadili urusi ndio aseme hapana.mrusi amechanga karata amemuweka mchina km mtaji wa dharula.pale baraza litakapoitaji kumjadili mrusi. kistratejia anawapa mtihani marekani na wenzake kuhusu msimamo wa china
Mbona juzi Alfajiri china walisema kwamba kutojumuika ktk kikao hicho huko UN sio kwamba hafungamani na upande wowote ule.....
Bali maadhimio na mapendekezo waliyo toa Urusi ndio waliyo kubalina Wao.....
 
Bunge la Seneti la Urusi limepitisha sheria ya kuruhusu ndege za jeshi za nchi hiyo kuruka na kufanya ulinzi kwenye anga la Syria hadi pale watakopoyatimiza malengo yaliyowapeleka pale.
Hili linamaanisha Urusi amejiingiza kabisa nchini Syria na hivyo basi kuongeza zaidi vikosi vya kijeshi vya anga nchini humo; hili limekuja baada ya ule mpango wa kufunga anga la nchi ya Syria kukataliwa.
Mrusi akiwa anatumia anga hilo kwa masaa 24 ina maana ni lazima apeleke vikosi vikubwa vya rada na makombora (Anti-Aircraft Shield) kwa ajili ya kudungulia ndege za mahasimu wao.

Kwa kawaida jeshi la anga haliwezi kufanya kazi bila msaada wa vikosi vya ardhini.
Kama vikosi vya angani vinaongezwa; nini kitazuia vikosi vya ardhini kuongezwa huko Syria?
Marekani na washirika wake hasa Israel na Saudi Arabia wamempa Mrusi sababu kubwa ya kutanua ushawishi wake huko Mashariki ya kati. Hili ndilo Mrusi alikuwa analitaka miaka nenda rudi.

Mambo ya kujiuliza,

  1. Hivi Mrusi akipeleka vikosi huko Syria hatalazimika kujenga kambi ya jeshi kweli?
  2. Ule mpango wa Israel kuvamia Iran utakuwepo bado? (Kwasababu ni raisi sana kwa vikosi vya Urusi kuingia Iran kutoka Syria, ukingatia umbali)
  3. Je, yale makundi kama Al-Nusra na ISIS yataweza kuwahimila Warusi peke yao? (Mataifa ya Magharibi yatafanya nini baada ya hili? ikumbukwe ndege zao ziatakuwa na ifunyu wa kutumia anga la Syria kutokana na uwepo wa vikosi vya Urusi)
  4. Sheria za kimataifa haziruhusu nchi kupeleka vikosi vya kijeshi mpaka nchi husika itoe mwaliko kama au baraza la ulinzi la Umoja wa taifa liruhusu. Hili la Umoja wa mataifa limeshindikana. Je, Marekani na Israel watakubali maslahi yao yakwamishwe kirahisi hivi? (Watatumije nguvu za kijeshi katika hali kama hii?)

CC: Richard , Bukyanagandi , Apollo , Dotworld , mshana jr , MOTOCHINI

 
Bunge la Seneti la Urusi limepitisha sheria ya kuruhusu ndege za jeshi za nchi hiyo kuruka na kufanya ulinzi kwenye anga la Syria hadi pale watakopoyatimiza malengo yaliyowapeleka pale.
Hili linamaanisha Urusi amejiingiza kabisa nchini Syria na hivyo basi kuongeza zaidi vikosi vya kijeshi vya anga nchini humo; hili limekuja baada ya ule mpango wa kufunga anga la nchi ya Syria kukataliwa.
Mrusi akiwa anatumia anga hilo kwa masaa 24 ina maana ni lazima apeleke vikosi vikubwa vya rada na makombora (Anti-Aircraft Shield) kwa ajili ya kudungulia ndege za mahasimu wao.

Kwa kawaida jeshi la anga haliwezi kufanya kazi bila msaada wa vikosi vya ardhini.
Kama vikosi vya angani vinaongezwa; nini kitazuia vikosi vya ardhini kuongezwa huko Syria?
Marekani na washirika wake hasa Israel na Saudi Arabia wamempa Mrusi sababu kubwa ya kutanua ushawishi wake huko Mashariki ya kati. Hili ndilo Mrusi alikuwa analitaka miaka nenda rudi.

Mambo ya kujiuliza,

  1. Hivi Mrusi akipeleka vikosi huko Syria hatalazimika kujenga kambi ya jeshi kweli?
  2. Ule mpango wa Israel kuvamia Iran utakuwepo bado? (Kwasababu ni raisi sana kwa vikosi vya Urusi kuingia Iran kutoka Syria, ukingatia umbali)
  3. Je, yale makundi kama Al-Nusra na ISIS yataweza kuwahimila Warusi peke yao? (Mataifa ya Magharibi yatafanya nini baada ya hili? ikumbukwe ndege zao ziatakuwa na ifunyu wa kutumia anga la Syria kutokana na uwepo wa vikosi vya Urusi)
  4. Sheria za kimataifa haziruhusu nchi kupeleka vikosi vya kijeshi mpaka nchi husika itoe mwaliko kama au baraza la ulinzi la Umoja wa taifa liruhusu. Hili la Umoja wa mataifa limeshindikana. Je, Marekani na Israel watakubali maslahi yao yakwamishwe kirahisi hivi? (Watatumije nguvu za kijeshi katika hali kama hii?)

CC: Richard , Bukyanagandi , Apollo , Dotworld , mshana jr , MOTOCHINI

[emoji635]
[emoji635]
[emoji635]
[emoji317] [emoji317] [emoji317] [emoji317] [emoji317] [emoji317] [emoji317] [emoji317]

Hao makulumbembe na kichaka Chao kinacho itwa NATO mbona wataisoma namba Mwaka huu....!!!
 
Back
Top Bottom