Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

RT ina uhuru wa kutangaza bila kuwa influenced na marekani. Haitangazi kwa maslahi ya Uncle SAM.

Pia hiyo kauli ya China kuunga mkono Russia ni habari ya leo saa sita usiku. Hiyo kauli ya ABC ni habari ya kabla ya mazungumzo ya Li Baodong kuzungumza leo. Na bado channels za US hazijasema hilo.

3dc1a24a978b3d396427383587f0c258.jpg
Kwa iyo RT haitangazi kwa influence ya Russia?...Unazi huu shida san
 
Kwani katiba ya Urusi inamruhusu Jemedari Putin akae ikulu kwa miaka mingapi?
 
Russia ataomba poo tuu kwenye hii movie,, wenzake wanaangalia uchumi wake zaidi, wanataka migogoro isiishe mikononi mwake kwa kipindi kirefu, huoni kwa sasa ana ulinzi wa nchi mbili, kwa hio anga la Damascus ni la kwake na Moscow as well,, sasa swali nikwamba kiherehere cha west mnavyokijua kamwe they will not stand down, and russia ata sustain namna hio kwa muda gani,, remember kwa watu wenye mipango ya muda mrefu ni wamarekan, si ajabu hio issue iko planned for 15yrs to come,,,niambie kwa kipindi hicho jamaa kapoteza ngap kwa muundo huu
 
Kwa iyo RT haitangazi kwa influence ya Russia?...Unazi huu shida san

The issue sio kutangaza kwa influence, ni kutangaza bila influence ya western propaganda. Propaganda in a media its common but isizidi to the extent. If you want to get a clear picture, don't rely sehemu moja ya informations iwe RT, ABC or any channel. Mfano kikao cha Leo cha China kuzungumza mpango wake, media za US hazijasema kwa sababu juzi zilikuwa zinasema something different. Dont you want to say kuwa hawajui hicho kikao, why its taking time?

Whats my concern sio propaganda ya mmoja, its a balance of power.
 
Jana Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Taifa ndiye aliwapasha vizuri Waingereza alisema tatizo lao bado wana Colonial Mentality - binafsi naona tatizo hilo hata Wafaransa wanalo sana.

Tukumbuke Syria iliwahi kuwa koloni la Ufaransa hawampendi Asaad lakini anaye vuta strings na Amerika, wanatumia Ufaransa kujaribu kumzuga Putin kumbe mwenzao kesha wasoma siku nyingi ndio maana mjumbe wa Ufaransa aliye kwenda Klemlin kuonana na,Putin na kumpa mapendekezo ya Ufaransa ya kusitisha mapigano, Putin hakumpa Mfaransa huyo jibu la moja kwa moja Urusi ilisubiri kutumia kura yake ya trufu kuzima njama za Ufaransa na Merikani.

Mimi kinacho nidhangaza kuhudu nchi hizi za magharibi specifically Ufaransa,Uingereza na kinara wao Uncle SAM ni kule kupuuzia hatari zinazo letwa/sababishwa na Ugaidi Duniani wanajali maslahi zaidi kuliko usalama wa raia wzo na mali zao

pengine kitu wasichokijua ni kuwa hawa magaidi wakuchonga siku wakikosa zile dolari kutoka kwao ndio utakuwa mwanzo wa nchi zao kutendewa ugaidi daily kwani watazamia huko kwao na kuanza kufanya fujo coz wakibaki huku kwa waarabu wenzao watalimwa vichwa kama mapapai
 
Kama sio Putin, hivi Bashar angekuwa marehemu kama Gaddafi. Russia alishasema, Historia ya Libya haitajirudia kwa Syria. Na itatumia njia yoyote kuondoa ISIS. Mataifa ya magharibi yakivamia hivyo vitakuwa ni vita kabisa.

This is very stupid. Kwanini Marekani na wapambe wake waamulie kufanya watakavyo Syria? Kwanini watoe support kwa ISIS? Yaani wanawapa terrorists na mercenaries support kwa kuwalipa na kuwapa silaha? Halafu hawataki hata kusikiliza serikali ya Syria na wanaidharau.

Hivi sasa anga la Syria lipo chini ya Russia. Na Urusi imefutilia mkataba wa kutumia Nuclear kwa amani wiki iliyopita hivi sasa inafanya itakavyo. Kinachofuata sio Peace. Western waamue moja, vita au wakubali kuachia Syria ifanye maamuzi yake na sio kuleta kama walichofanya Libya na Iraq.

Tuko karibu kabisa na VITA YA TATU YA DUNIA
 
Russia ataomba poo tuu kwenye hii movie,, wenzake wanaangalia uchumi wake zaidi, wanataka migogoro isiishe mikononi mwake kwa kipindi kirefu, huoni kwa sasa ana ulinzi wa nchi mbili, kwa hio anga la Damascus ni la kwake na Moscow as well,, sasa swali nikwamba kiherehere cha west mnavyokijua kamwe they will not stand down, and russia ata sustain namna hio kwa muda gani,, remember kwa watu wenye mipango ya muda mrefu ni wamarekan, si ajabu hio issue iko planned for 15yrs to come,,,niambie kwa kipindi hicho jamaa kapoteza ngap kwa muundo huu
Mafuta,uranium kutoka Syria mahusiano mazuri kati ya asad na Putin...

Russia hawezi kupoteza
 
Kwa mtizamo wako unaona Bashar Al Asad ni bora kuliko watu wote mchini Syria si ndio?
Assad yuko upande mmoja na wasyria, dhidi ya uvamizi wa kigeni wakishirikiana magaidi.
 
The issue sio kutangaza kwa influence, ni kutangaza bila influence ya western propaganda. Propaganda in a media its common but isizidi to the extent. If you want to get a clear picture, don't rely sehemu moja ya informations iwe RT, ABC or any channel. Mfano kikao cha Leo cha China kuzungumza mpango wake, media za US hazijasema kwa sababu juzi zilikuwa zinasema something different. Dont you want to say kuwa hawajui hicho kikao, why its taking time?

Whats my concern sio propaganda ya mmoja, its a balance of power.
Unaposema media za US hazijatangaza unamaanisha nini ndugu/..wewe una access na media zaid ya mamia za US?..usiku wa kuamkia Leo nmeangalia CNN mbona wametangaza huo uamuzi wa china?..Mnaposema western propaganda mda mwingine nakua siwaelewi kabisa,alafu epuka sana generalization,ku genaralize mambo kunafifisha uwezo wa kufikiri vizuri.
Pili nachofahamu mimi ni bora private western media za marekani na ulaya ziko challengable kwa serikali zake na muda mwingine zinaweza kuendesha mijadala mikali kwa hali ya uhuru na watu wakajadili mambo kwa uwazi,kuliko kuniaminisha kwamba media kama RT ambayo kutwa ki kuendesha mijadala iliyo againsh US na kuisifia russia hata kwa mambo ya kipuuzi..Kwa mfano hii misimamo ya US dhidi ya syria ni vyombo vingi sana vyua habari vimekuwa vikianzisha mijadala kuusu huu uamuzi wa US kwa nchi ya Syria na watu wamekuwa waki condem vikali sana na kila mtu akiona.Sasa leo mtu unatoka huko unakuja na kusema eti propaganda za US.Ni lini ulishaona media kama RT au any private media ya Russia akifanya mijadala kama hii katika mambo yanayohusu maamuzi ya serikali m oja kwa moja hadharani?..
Acheni unazi wa kijinga.
 
getty-putin-obama.jpg

"Smooth operator" raisi Putin akijaribu kutoa mkono wa salamu kwa raisi Barak Obama.

Mkuu Malcom Lumumba heshima yako.

Hii haitakuwa "Cuban Missile Crisis" ingine maana ile ni historia nzuri sana.

Jambo la msingi kabisa kufahamu ni kwamba sasa hivi Russia wanawazidi nguvu waasi walipo mashariki mwa mji wa Aleppo ambao wanasaidiwa na Marekani na nchi za magharibi ambao lengo lao ni kumtoa raisi Assad.

Pia ndiyo umesikia John Kerry anaanza kudai kwamba Russia watashtakiwa kwa war crimes yaani wameua watu wengi waso na hatia huku ikieleweka wazi kwamba magaidi wanakuwa imbedded na wananchi wa kawaida hivyo kufanya kazi ya majeshi ya Syria na Russia kuwa hawana choice bali ni kutungua tu, hiyo moja.

Mbili, ni kwamba Marekani inaisaidia Saudi Arabia kupiga mabomu nchini Yemen na tumesikia watu karibu 10,000 wamefariki na UN aimeionya Marekani kwa kuwasaidia Saudi Arabia kwa ndege zake za kivita.

Hii pia inawafanya Marekani pia kuweza kushtakiwa kwa war crimes vilevile kwa kuwasaidia wasaudi kuua watu waso na hatia huko Yemen.

Sasa nikirudi kwenye masuali yako manne:

1. Mataifa ya magharibi hayawezi kujifunza na hayako tayari kufanya hivyo kwasababu hii ni vita ya kuhusu nani ana eneo lake la ushawishi katika mashariki ya kati na rasilimali zilizoko hapo khasa mafuta na gesi.

Hii inaenda sambamba na uhalisia kwamba tayari watu wa Syria ambao wanataka kuongoza nchi hiyo wakiwa vibaraka wa Marekani na nchi za magharibi nao sasa hivi wapo desperate kuona kwamba mpango wa kumwondoa Assad unakamilishwa haraka iwezekanavyo na hii inafanana kabisa na hali ilvyokuwa kule Libya.

2. Wakivamia Syria wataongeza magaidi kwani wale walipo tu wanatosha kuleta matatizo kwa nchi zote za mashariki ya kati. Ikumbukwe si tu ISIS bali pia kuna Al-Nusra na ALqaeda ambao wamesambaa hadi huko Yemen.

3. Kuna mada moja nimechangia nikitaja "nchi ya tatu" kwamba ndiyo iliyo nyuma ya Marekani katika mpango wake wa kujizatiti kwenye ubeberu wao katika eneo la Mashariki ya Kati, hivyo tunamweka Israel pamoja na Marekani na nchi za magharibi.

Iran wao wapo nyuma ya Russian kwani wakiwa wao ni washia hawatapenda kuona kabila la sunni ndilo linatawala Syria kama wanavyotaka kumwondoa Assad.

4. Mataifa ya magharibi hayawezi kuivamia Syria kama walivyofanya Libya kwani Russia tayari ametoa onyo la kutoshambulia majeshi ya Syria ambayo yapo kwenye vituo vya kijeshi ambavyo vimejengwa na Russia.

Hivyo inaonekana itaitwa round ingine UN kupitisha azimio bila kura ya Russia ambapo jambo hilo pia ni gumu kulitekeleza.
Nimecheka hiyo picha hapo juu,inaonyesha Putin alivyo na machale,hata mkono wa presida mwenzie anautilia mashaka.
 
Trump is a cure to all this horrible diseases in the world
 
Wasalaam,
Jana tarehe 8 kikao cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa kimeshindwa kupitisha Azimio la kuvamia nchi ya Syria kijeshi lililoletwa na nchi ya Ufaransa.
Aidha ilitegemewa kikao hicho kiruhusu uvamizi wa kijeshi nchini Syria ambapo ndege za mataifa ya nje zingeruhusiwa kuingia nchini Syria na kufunga anga lake ili ndege za kivita za serikali ya Bashar Al Asad zisiruke na kuendelea kuua raia wake.

Nchi ya Urusi kupitia balozi wake wa kudumu wa Umoja wa mataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza hilo la Ulinzi na Usalama wamepinga Azimio la Mfaransa na Hispania kuhusu kuacha kulipua maeneo ya jiji la Aleppo ili warudi kwenye mazungumzo ya mezani.
Pingamizi hili imeambatana na kura ya Hapana (VETO) kutoka Urusi, hivyo kutupilia mbali kabisa Azimio hilo la Baraza la Ulinzi na Usalama.

Na kibaya zaidi ni kwamba Mrusi naye alileta Azimio lake kuhusu nchi ya Syria lakini nalo likapingwa kwa kutumia kura ya VETO kutoka nchi za Magharibi. Serikali ya Uchina imeamua kutofungamana na upande wowote na kuamua kutopiga kura kabisa.

Ikumbukwe mwaka 2011 Azimio namba 1973 la Umoja wa Mataifa ndilo lilirohusu mataifa ya Magharibi yakiongozwa na NATO kwenda kufunga anga la nchi ya Libya na mwisho wake wote tunajua ni nini kilitokea. Mataifa ya Magharibi yalivuka mipaka na kuanza kulipua hadi chini kitu ambacho ni kinyume kabisa na Azimio.

Kinachoniogopesha ni kauli zisizo za Kidiplomasia ambazo zimetolewa na Mabalozi husika katika kikao hicho. Mfano tu, Balozi wa Uingereza bwana Matthew Rycroft amesema "Normally I begin my statement with, ‘Thank you Mr President’, cannot do this today. his council cannot stand by while such misery is meted out on the people of Aleppo. And yet, thanks to you, Mr President, that is exactly what we are doing. Thanks to your actions today, Syrians will continue to lose their lives in Aleppo and beyond to Russian and Syrian bombing. Please stop now."

Balozi wa Marekani naye kasema "One of us, perversely the president of council, is determined for the killing to continue, and is helping carry it out"
Kilichonishangaza zaidi ni pale ambapo wajumbe wa mataifa ya Marekani, Ufaransa, Uingereza na mengine kuamua kutoka wakati balozi wa nchi ya Syria alipoanza kuzungumza kuhusu huu mgogoro.

Kama hawataki kuwasikiliza wahusika, je watamsikiliza nani kwa sasa?
Ikumbukwe kwamba Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa ndilo pekee lenye uwezo wa kuidhinisha uvamizi wa nchi yoyote ile kama linahisi kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Uvamizi kama ule wa George Bush wa mwaka 2003 hauruhusiwi na ndiyo umechangia kuleta mambo kama ISIS, AL-NUSRA na Wimbi la Wakimbizi barani Ulaya.

Najiuliza tu,

  1. Kwanini haya mataifa ya Magharibi hayajifunzi tu?
  2. Wakivamia Syria hawataongeza Wakimbizi na Ugaidi kweli?
  3. Kwanini wahusika wakuu kama Israel, Iran na Syria wanaachwa kwenye vikao muhimu kama hivi?
  4. Je mataifa ya Magharibi yanaweza kuvamia Syria bila ruhusa ya Baraza la Ulinzi?
CC: Richard , Dotworld , Bukyanagandi
Waacheni nao wauane make kule Libya waluwaua sana watu
 
Mkuu Dotworld upo wapi bhanaaaa,
Njoo uchangamshe jamvi huku naona Best wako Putin anawakata ngebe waaimba taarabu .......
 
Then wakimbizi wakianza kwenda nchini mwao wanawawekea vikwazo huku wakisahau kuwa wao ndio chanzo cha arise mapigano sehem mbalimbali duniani
 
Hizi mbwembwe za mrusi na hashuo la mmarekani litaisha keshokutwa Trump akiingia madarakani, Besti wake Putin. Mrusi kavunja mkataba wa nuclear lakini akiingia trump ata renew ili image ya trump ikubalike..... na watakuwa na uhusiano mzuri sana tu kuliko mara zote.
 
Back
Top Bottom