Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,764
Reaction score
71,793
Wasalaam,
Jana tarehe 8 kikao cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa kimeshindwa kupitisha Azimio la kuvamia nchi ya Syria kijeshi lililoletwa na nchi ya Ufaransa.
Aidha ilitegemewa kikao hicho kiruhusu uvamizi wa kijeshi nchini Syria ambapo ndege za mataifa ya nje zingeruhusiwa kuingia nchini Syria na kufunga anga lake ili ndege za kivita za serikali ya Bashar Al Asad zisiruke na kuendelea kuua raia wake.

Nchi ya Urusi kupitia balozi wake wa kudumu wa Umoja wa mataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza hilo la Ulinzi na Usalama wamepinga Azimio la Mfaransa na Hispania kuhusu kuacha kulipua maeneo ya jiji la Aleppo ili warudi kwenye mazungumzo ya mezani.
Pingamizi hili imeambatana na kura ya Hapana (VETO) kutoka Urusi, hivyo kutupilia mbali kabisa Azimio hilo la Baraza la Ulinzi na Usalama.

Na kibaya zaidi ni kwamba Mrusi naye alileta Azimio lake kuhusu nchi ya Syria lakini nalo likapingwa kwa kutumia kura ya VETO kutoka nchi za Magharibi. Serikali ya Uchina imeamua kutofungamana na upande wowote na kuamua kutopiga kura kabisa.

Ikumbukwe mwaka 2011 Azimio namba 1973 la Umoja wa Mataifa ndilo lilirohusu mataifa ya Magharibi yakiongozwa na NATO kwenda kufunga anga la nchi ya Libya na mwisho wake wote tunajua ni nini kilitokea. Mataifa ya Magharibi yalivuka mipaka na kuanza kulipua hadi chini kitu ambacho ni kinyume kabisa na Azimio.

Kinachoniogopesha ni kauli zisizo za Kidiplomasia ambazo zimetolewa na Mabalozi husika katika kikao hicho. Mfano tu, Balozi wa Uingereza bwana Matthew Rycroft amesema "Normally I begin my statement with, ‘Thank you Mr President’, cannot do this today. his council cannot stand by while such misery is meted out on the people of Aleppo. And yet, thanks to you, Mr President, that is exactly what we are doing. Thanks to your actions today, Syrians will continue to lose their lives in Aleppo and beyond to Russian and Syrian bombing. Please stop now."

Balozi wa Marekani naye kasema "One of us, perversely the president of council, is determined for the killing to continue, and is helping carry it out"
Kilichonishangaza zaidi ni pale ambapo wajumbe wa mataifa ya Marekani, Ufaransa, Uingereza na mengine kuamua kutoka wakati balozi wa nchi ya Syria alipoanza kuzungumza kuhusu huu mgogoro.

Kama hawataki kuwasikiliza wahusika, je watamsikiliza nani kwa sasa?
Ikumbukwe kwamba Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa ndilo pekee lenye uwezo wa kuidhinisha uvamizi wa nchi yoyote ile kama linahisi kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Uvamizi kama ule wa George Bush wa mwaka 2003 hauruhusiwi na ndiyo umechangia kuleta mambo kama ISIS, AL-NUSRA na Wimbi la Wakimbizi barani Ulaya.

Najiuliza tu,

  1. Kwanini haya mataifa ya Magharibi hayajifunzi tu?
  2. Wakivamia Syria hawataongeza Wakimbizi na Ugaidi kweli?
  3. Kwanini wahusika wakuu kama Israel, Iran na Syria wanaachwa kwenye vikao muhimu kama hivi?
  4. Je mataifa ya Magharibi yanaweza kuvamia Syria bila ruhusa ya Baraza la Ulinzi?
CC: Richard , Dotworld , Bukyanagandi
 
asietakiwa hapo ni Al Asad, operation ya ISIS waliotumwa inafeli mrusi kikwazo wanataka walete no fly zone kama Libya ili wampige vizuri

Wamefeli kivipi mkuu?
Na akina nani?
 
Kama sio Putin, hivi Bashar angekuwa marehemu kama Gaddafi. Russia alishasema, Historia ya Libya haitajirudia kwa Syria. Na itatumia njia yoyote kuondoa ISIS. Mataifa ya magharibi yakivamia hivyo vitakuwa ni vita kabisa.

This is very stupid. Kwanini Marekani na wapambe wake waamulie kufanya watakavyo Syria? Kwanini watoe support kwa ISIS? Yaani wanawapa terrorists na mercenaries support kwa kuwalipa na kuwapa silaha? Halafu hawataki hata kusikiliza serikali ya Syria na wanaidharau.

Hivi sasa anga la Syria lipo chini ya Russia. Na Urusi imefutilia mkataba wa kutumia Nuclear kwa amani wiki iliyopita hivi sasa inafanya itakavyo. Kinachofuata sio Peace. Western waamue moja, vita au wakubali kuachia Syria ifanye maamuzi yake na sio kuleta kama walichofanya Libya na Iraq.
 
Wakiivamia baadae watatuletea zile story za Obama kuhusu libya kwamba walifanya makosa kuivamia.... nakumbuka mwalimu wangu aliniambia kua "wale ambao hawakumbuki historia, ndio ambao kimakosa hurudia makosa ya kihistoria". sasa sijui wenzetu hua hawakumbuki historia au ndio business as usual
 
asietakiwa hapo ni Al Asad, operation ya ISIS waliotumwa inafeli mrusi kikwazo wanataka walete no fly zone kama Libya ili wampige vizuri

Well said

Sasa hivi anga la Syria lipo chini ya Russia. Sasa ISIS inakosa support ya misaada kwa wapambe waliowatuma. Naona wanaanza kulalamika ili watafute namna ya kuwasaidia ISIS ili waendelee na style kama Libya.
 
Wakiivamia baadae watatuletea zile story za Obama kuhusu libya kwamba walifanya makosa kuivamia.... nakumbuka mwalimu wangu aliniambia kua "wale ambao hawakumbuki historia, ndio ambao kimakosa hurudia makosa ya kihistoria". sasa sijui wenzetu hua hawakumbuki historia au ndio business as usual

True mkuu.

Kila siku wanalalamika kuwa ilikuwa mistake kuvamia Libya, angalia maisha ya Libyans hivi sasa. Halafu wanarudia vile vile na kwa formula ile ile nchini Syria. Its insanity.

Serious. These guys wana jambo. Sio bure.
 
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ni chombo cha mabeberu cha kufanikisha mambo yao. Kinachowaumiza siyo taabu za Wasyria Bali ni kwa sababu malengo yao ya kumg'oa Assad hayakutimia. Na kikwazo ni Urusi na Iran. Ni Yale Yale ya Iraq na Libya.
 
Libya juzi tenki za mafuta zimesafirishwa mpk nikahuzunika ase japo cyo mwananchi wa huko

Juzi us walipiga camp ya jeshi la Syria na kuua wanajeshi 60+ halafu wanasema bahat mby na shambulio hyo iliwapa upenyo Isis wachukue hyo ngome

Kwa miaka 5 us alikuwa anampa sapoti Isis kisha baadae anampiga ,ili tu Syria ichafuke muda wote mafuta ajichotee

Well done putin
 
Kama sio Putin, hivi Bashar angekuwa marehemu kama Gaddafi. Russia alishasema, Historia ya Libya haitajirudia kwa Syria. Na itatumia njia yoyote kuondoa ISIS. Mataifa ya magharibi yakivamia hivyo vitakuwa ni vita kabisa.

Mkuu,
Hakuna wa kuivamia Syria,
Kama wangekuwa na huo ubavu sidhani kama wangeenda kuomba ruhusa Umoja wa Mataifa.
Ingekuwa kama Iraq.
 
Yaani ndugu kama sio Putin? Hii dunia ingekuwa ya mtu mmoja.

Tunahitaji balance of power kama ilivyo hivi sasa, sio kuwepo na nchi inayotaka kufanya itakavyo kwa sababu inajiona ni super power.
 
Kwa mtizamo wako unaona Bashar Al Asad ni bora kuliko watu wote mchini Syria si ndio?
Wasalaam,
Jana tarehe 8 kikao cha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa kimeshindwa kupitisha Azimio la kuvamia nchi ya Syria kijeshi lililoletwa na nchi ya Ufaransa.
Aidha ilitegemewa kikao hicho kiruhusu uvamizi wa kijeshi nchini Syria ambapo ndege za mataifa ya nje zingeruhusiwa kuingia nchini Syria na kufunga anga lake ili ndege za kivita za serikali ya Bashar Al Asad zisiruke na kuendelea kuua raia wake.

Nchi ya Urusi kupitia balozi wake wa kudumu wa Umoja wa mataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza hilo la Ulinzi na Usalama wamepinga Azimio la Mfaransa na Hispania kuhusu kuacha kulipua maeneo ya jiji la Aleppo ili warudi kwenye mazungumzo ya mezani.
Pingamizi hili imeambatana na kura ya Hapana (VETO) kutoka Urusi, hivyo kutupilia mbali kabisa Azimio hilo la Baraza la Ulinzi na Usalama.

Na kibaya zaidi ni kwamba Mrusi naye alileta Azimio lake kuhusu nchi ya Syria lakini nalo likapingwa kwa kutumia kura ya VETO kutoka nchi za Magharibi. Serikali ya Uchina imeamua kutofungamana na upande wowote na kuamua kutopiga kura kabisa.

Ikumbukwe mwaka 2011 Azimio namba 1973 la Umoja wa Mataifa ndilo lilirohusu mataifa ya Magharibi yakiongozwa na NATO kwenda kufunga anga la nchi ya Libya na mwisho wake wote tunajua ni nini kilitokea. Mataifa ya Magharibi yalivuka mipaka na kuanza kulipua hadi chini kitu ambacho ni kinyume kabisa na Azimio.

Kinachoniogopesha ni kauli zisizo za Kidiplomasia ambazo zimetolewa na Mabalozi husika katika kikao hicho. Mfano tu, Balozi wa Uingereza bwana Matthew Rycroft amesema "Normally I begin my statement with, ‘Thank you Mr President’, cannot do this today. his council cannot stand by while such misery is meted out on the people of Aleppo. And yet, thanks to you, Mr President, that is exactly what we are doing. Thanks to your actions today, Syrians will continue to lose their lives in Aleppo and beyond to Russian and Syrian bombing. Please stop now."

Balozi wa Marekani naye kasema "One of us, perversely the president of council, is determined for the killing to continue, and is helping carry it out"
Kilichonishangaza zaidi ni pale ambapo wajumbe wa mataifa ya Marekani, Ufaransa, Uingereza na mengine kuamua kutoka wakati balozi wa nchi ya Syria alipoanza kuzungumza kuhusu huu mgogoro.

Kama hawataki kuwasikiliza wahusika, je watamsikiliza nani kwa sasa?
Ikumbukwe kwamba Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa ndilo pekee lenye uwezo wa kuidhinisha uvamizi wa nchi yoyote ile kama linahisi kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Uvamizi kama ule wa George Bush wa mwaka 2003 hauruhusiwi na ndiyo umechangia kuleta mambo kama ISIS, AL-NUSRA na Wimbi la Wakimbizi barani Ulaya.

Najiuliza tu,

  1. Kwanini haya mataifa ya Magharibi hayajifunzi tu?
  2. Wakivamia Syria hawataongeza Wakimbizi na Ugaidi kweli?
  3. Kwanini wahusika wakuu kama Israel, Iran na Syria wanaachwa kwenye vikao muhimu kama hivi?
  4. Je mataifa ya Magharibi yanaweza kuvamia Syria bila ruhusa ya Baraza la Ulinzi?
CC: Richard , Dotworld , Bukyanagandi
 
Mkuu,
Hakuna wa kuivamia Syria,
Kama wangekuwa na huo ubavu sidhani kama wangeenda kuomba ruhusa Umoja wa Mataifa.
Ingekuwa kama Iraq.

Well said mkuu.

Ndio maana wanakimbilia umoja wa mataifa, ambao ndio uwanja wao wa nyumbani wa kujitetea.
 
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ni chombo cha mabeberu cha kufanikisha mambo yao. Kinachowaumiza siyo taabu za Wasyria Bali ni kwa sababu malengo yao ya kumg'oa Assad hayakutimia. Na kikwazo ni Urusi na Iran. Ni Yale Yale ya Iraq na Libya.

Kweli,
Baraza lina matatizo makubwa haswa kimfumo.
Huwezi kuweka hatma ya dunia nzima kwenye mataifa matano tu, kisa tu yalishinda vita ya pili ya dunia.
Mfano kwa jinsi ilivyo sasa maslahi tofauti yamewagawa na mambo hayaendi kabisa.

Kuna siku moja nilisoma hotuba ya Mzee Mahiga,
Alizungumzia jinsi gani mataifa mengine kama India, Brazil na Ujerumani yangeweza kuhusishwa kwenye maamuzi. Waliwaza vizuri lakini tatizo siyo idadi ya wajumbe bali ni mfumo mbovu tu.
Kigezo cha ujumbe wa kudumu hakiwezi kuwa ni ushindi wa vita ya pili na Ushawishi wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi.

Tukitaka kufanikiwa ni lazima ushiriki wa kila taifa uangaliwe ili maslahi ya nchi zote yalindwe.
Hata kikanda tu inatosha, japo Mrusi na Marekani hawataki kabisa hili litokee.
 
getty-putin-obama.jpg

"Smooth operator" raisi Putin akijaribu kutoa mkono wa salamu kwa raisi Barak Obama.

Mkuu Malcom Lumumba heshima yako.

Hii haitakuwa "Cuban Missile Crisis" ingine maana ile ni historia nzuri sana.

Jambo la msingi kabisa kufahamu ni kwamba sasa hivi Russia wanawazidi nguvu waasi walipo mashariki mwa mji wa Aleppo ambao wanasaidiwa na Marekani na nchi za magharibi ambao lengo lao ni kumtoa raisi Assad.

Pia ndiyo umesikia John Kerry anaanza kudai kwamba Russia watashtakiwa kwa war crimes yaani wameua watu wengi waso na hatia huku ikieleweka wazi kwamba magaidi wanakuwa imbedded na wananchi wa kawaida hivyo kufanya kazi ya majeshi ya Syria na Russia kuwa hawana choice bali ni kutungua tu, hiyo moja.

Mbili, ni kwamba Marekani inaisaidia Saudi Arabia kupiga mabomu nchini Yemen na tumesikia watu karibu 10,000 wamefariki na UN aimeionya Marekani kwa kuwasaidia Saudi Arabia kwa ndege zake za kivita.

Hii pia inawafanya Marekani pia kuweza kushtakiwa kwa war crimes vilevile kwa kuwasaidia wasaudi kuua watu waso na hatia huko Yemen.

Sasa nikirudi kwenye masuali yako manne:

1. Mataifa ya magharibi hayawezi kujifunza na hayako tayari kufanya hivyo kwasababu hii ni vita ya kuhusu nani ana eneo lake la ushawishi katika mashariki ya kati na rasilimali zilizoko hapo khasa mafuta na gesi.

Hii inaenda sambamba na uhalisia kwamba tayari watu wa Syria ambao wanataka kuongoza nchi hiyo wakiwa vibaraka wa Marekani na nchi za magharibi nao sasa hivi wapo desperate kuona kwamba mpango wa kumwondoa Assad unakamilishwa haraka iwezekanavyo na hii inafanana kabisa na hali ilvyokuwa kule Libya.

2. Wakivamia Syria wataongeza magaidi kwani wale walipo tu wanatosha kuleta matatizo kwa nchi zote za mashariki ya kati. Ikumbukwe si tu ISIS bali pia kuna Al-Nusra na ALqaeda ambao wamesambaa hadi huko Yemen.

3. Kuna mada moja nimechangia nikitaja "nchi ya tatu" kwamba ndiyo iliyo nyuma ya Marekani katika mpango wake wa kujizatiti kwenye ubeberu wao katika eneo la Mashariki ya Kati, hivyo tunamweka Israel pamoja na Marekani na nchi za magharibi.

Iran wao wapo nyuma ya Russian kwani wakiwa wao ni washia hawatapenda kuona kabila la sunni ndilo linatawala Syria kama wanavyotaka kumwondoa Assad.

4. Mataifa ya magharibi hayawezi kuivamia Syria kama walivyofanya Libya kwani Russia tayari ametoa onyo la kutoshambulia majeshi ya Syria ambayo yapo kwenye vituo vya kijeshi ambavyo vimejengwa na Russia.

Hivyo inaonekana itaitwa round ingine UN kupitisha azimio bila kura ya Russia ambapo jambo hilo pia ni gumu kulitekeleza.
 
Kama sio Putin, hivi Bashar angekuwa marehemu kama Gaddafi. Russia alishasema, Historia ya Libya haitajirudia kwa Syria. Na itatumia njia yoyote kuondoa ISIS. Mataifa ya magharibi yakivamia hivyo vitakuwa ni vita kabisa.

This is very stupid. Kwanini Marekani na wapambe wake waamulie kufanya watakavyo Syria? Kwanini watoe support kwa ISIS? Yaani wanawapa terrorists na mercenaries support kwa kuwalipa na kuwapa silaha? Halafu hawataki hata kusikiliza serikali ya Syria na wanaidharau.

Hivi sasa anga la Syria lipo chini ya Russia. Na Urusi imefutilia mkataba wa kutumia Nuclear kwa amani wiki iliyopita hivi sasa inafanya itakavyo. Kinachofuata sio Peace. Western waamue moja, vita au wakubali kuachia Syria ifanye maamuzi yake na sio kuleta kama walichofanya Libya na Iraq.

Bila Russia Assad angekuwa anaishi London maana mkewe ni muingereza na yeye ni daktari wa meno.

Angekuwa anaishi kama dokta wa meno UK wangemvusha.

Hiyo ya mkewe Assad kuwa ni mwingereza inawasumbua sana hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom