Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

Umoja wa mataifa: Syria haitavamiwa kijeshi

Bila Russia Assad angekuwa anaishi London maana mkewe ni muingereza na yeye ni daktari wa meno.

Angekuwa anaishi kama dokta wa meno UK wangemvusha.

Hiyo ya mkewe Assad kuwa ni mwingereza inawasumbua sana hawa jamaa.

Hahaha.

Si unajua huwa wana style yao ya kuwanyima uraia ili wawapige vizuri. Hapo huwa inawauma sana kuona lazima apate nationality ya UK kwa sababu ya mke wake, for real.
 
China na yeye huwaga ni snitch tu, sijui mpk aje awekewe no fly zone kwake ndo ataelewa umuhimu wa kua na msimamo
China ni mfanyabiashara yy anataka auze kila mahala ndio maana licha ya kushinikizwa amwekee vikwazo north Korea amekataa,anampelekea mafuta,chakula

China yupo kimaslah sana kila upande yupo japo ni mpinzani wa usa
 
China na yeye huwaga ni snitch tu, sijui mpk aje awekewe no fly zone kwake ndo ataelewa umuhimu wa kua na msimamo

Hatufahamu makubaliano kati ya Russia na China kwenye hili na ukimya wa China na inaweza kuleta matatizo makubwa kwa Marekani.

Pili, Marekani pia hafahamu ni makubaliano gani Russia na China wamefikia khasa baada ya kitendo cha China kutoshiriki kwenye mkutano wa baraza la Usalama la UN juzi.

Lakini tunaweza kuondoa wasiwasi kwani China nao ni taifa kubwa sasa hivi kiuchumi na kijeshi, hivyo yeye angoja zamu yake.
 
China ni mfanyabiashara yy anataka auze kila mahala ndio maana licha ya kushinikizwa amwekee vikwazo north Korea amekataa,anampelekea mafuta,chakula

China yupo kimaslah sana kila upande yupo japo ni mpinzani wa usa
Wafanyabiashara wapi jamaa waoga tu, kipindi kile Tanzania ina anza kuzinguana na Malawi ile issue ya Ziwa, China ikatoa bonge la statement ooh Tanzania ni rafiki yetu wa Kihistoria na tutahakikisha yuko salama na hakuna atakeye mgusa leo Huko Syria ameona mziki mkubwa wa Usa+Nato kabidi ajifiche nyuma ya UFANYABIASHARA
 
Hatufahamu makubaliano kati ya Russia na China kwenye hili na ukimya wa China na inaweza kuleta matatizo makubwa kwa Marekani.

Pili, Marekani pia hafahamu ni makubaliano gani Russia na China wamefikia khasa baada ya kitendo cha China kutoshiriki kwenye mkutano wa baraza la Usalama la UN juzi.

Lakini tunaweza kuondoa wasiwasi kwani China nao ni taifa kubwa sasa hivi kiuchumi na kijeshi, hivyo yeye angoja zamu yake.
Mkuu kuna makubaliano yangekua ya maana kama ya China kupiga kura ya Veto, kuwe na Veto ya Russia na China. Huoni ingeleta uzito kuliko hizi kona kona za mchina
 
Mkuu kuna makubaliano yangekua ya maana kama ya China kupiga kura ya Veto, kuwe na Veto ya Russia na China. Huoni ingeleta uzito kuliko hizi kona kona za mchina

Wanafahamu kwamba kura moja ya Veto inatosha kwa mjumbe mmoja na ndiyo alotumia Russia.

Wachina wao wanapiga mahesbau yao hawana haraka.
 
Yaani ndugu kama sio Putin? Hii dunia ingekuwa ya mtu mmoja.

Tunahitaji balance of power kama ilivyo hivi sasa, sio kuwepo na nchi inayotaka kufanya itakavyo kwa sababu inajiona ni super power.
Yani hapo umenena Mkuu,

Tuna wahitaji watu wa aina ya Putin kipindi hiki bhanaaaaa
 
Well said mkuu.

Ndio maana wanakimbilia umoja wa mataifa, ambao ndio uwanja wao wa nyumbani wa kujitetea.
Na hata wakikimbilia huko kwenye kipanda chao wanacho kiita UN mrusi atamchapa na kura ya Veto.

Na wakigaidi hapo sasa ndio singeli itakavyo chezwa wakubwa kwa wakubwa
 
True mkuu.

Kila siku wanalalamika kuwa ilikuwa mistake kuvamia Libya, angalia maisha ya Libyans hivi sasa. Halafu wanarudia vile vile na kwa formula ile ile nchini Syria. Its insanity.

Serious. These guys wana jambo. Sio bure.

Mkuu, Jana Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa maTaifa ndiye aliwapasha vizuri Waingereza, alisema tatizo lao bado wana Colonial Mentality - binafsi naona tatizo hilo hata Wafaransa wanalo sana.

Tukumbuke Syria iliwahi kuwa koloni la Ufaransa, hawampendi Asaad lakini anaye vuta strings pale ni Amerika, walitumia Ufaransa kujaribu kumzuga Putin kumbe mwenzao kesha wasoma siku nyingi ndio maana mjumbe wa Ufaransa aliye kwenda kuonana na Putin na kumpa mapendekezo ya Ufaransa ya kusitisha mapigano, Putin hakumpa Mfaransa huyo jibu la moja kwa moja, Urusi ilisubiri kutumia kura yake ya trufu kuzima njama za Ufaransa na Merikani, sijui kwa nini nchi hizi azishitukii uwezo mkubwa wa kijasusi wa Urusi, hata incident ya kula njama za kutaka kushambulia kwa kushitukiza viwanja vya ndege vinavyo tumiwa na jeshi la Syria, Urusi ilipewa taarifa za kijasusi mapema kuhusu njama hizo, jeshi la Merikani liliona aliwezi ku risk ndege na marubani wake hivyo walipanga kutumia njia mbadala ya kuvurumisha Subsonic Tomahawk Cruise missiles kuhujumu viwanja vya ndege la jeshi la Syria.

Kitu kinacho shangaza kidogo ni kuhusu Merikani ni kwa nini aikushitukia kwa kujiuliza nani anawapa Warusi taarifa in advance - iweje taarifa za siri kuhusu mipango ya operations za jeshi la Merikani dhidi ya Syria/Urusi zijulikane mapema? Yaani Merikani awajiulizi kama kuna moles ndani ya Serikali/washirika wao ambao ndio chanzo cha kuvujisha siri na kuwapatia Warusi.

Narudia kusema kwamba Weakness tajwa hapo juu - zinadhilisha kwamba ndani ya Serikali ya Merikani au Washirika wake kuna baadhi ya watu wenye morals zao ambao wanakerwa na siasa hatarishi za Merikani, ndio maana wako radhi kuwasaliti kwa kutoa taarifa mapema na kuwapatia Warusi ili wajihami mapema zaidi - sasa hii si habari nzuri kwa the USA, ina maana wakipanga kuishambulia Urusi kwa kuishtukiza na mabom ya thermonuclear, Urusi itapata taarifa mapema na ku unleash a pre emptive strikes kwenye major cities na Military bases kubwa kubwa kwa kutumia makombola yenye payload ya ma TERATONNE ya TNT, Warusi makombola ya type hiyo wanayo sana mfano RS-28 Sarmat ICBM iliyo sheheni na MIRVs zaidi ya kumi na tano zikiwemo decoys!!!

Umahili wa ujasusi wa Taifa la Urusi inanikumbusha tukio/kisanga kilicho wahi kutokea wakati wa uhundwaji wa bom la Nuclear in mid 1940s, wanasayansi/Engineers walijua kwamba Amerika ikimiliki bom peke yao Dunia aitakuwa salama ,Wamerika watatumia bom hilo ku blackmail Warusi na nchi nyingine zinazo inukia, ndio maana baadhi ya wanasayansi majasusi kwenye Project ya Manhattan aliyo kuwa inasimamiwa na Robert Oppenheimer walifanikiwa kuwapatia Warusi designs za capacitors zinazo tumika kulipua high explosive lenses za ku initiate chain reaction (atomic fission), watu wengi hawajui kwamba Urusi nayo ilikuwa inafanya tafiti katika masuala ya uhundaji bom la Nuclear, Dunia inapashwa kuwashukuru wanasayansi majasusi walio jitolea kuwapa msaada Warusi, bila kufanya hivyo Wamerika wangenyanyasa sana Dunia. Hapo natoa angalizo la kuonyesha kwamba hapa Duniani bado kuna watu ambao wana morals zao hata kwenye Administration ya Obama wapo sana.

Tukirudi kwenye mada kuhusu yanayo jili nchini Syria - Mimi kinacho nishangaza kuhusu akili za Viongozi wa nchi za magharibi specifically Ufaransa,Uingereza na kinara wao Uncle SAM ni kule kupuuzia hatari zinazo letwa/sababishwa na Ugaidi Duniani, wanajali maslahi zaidi kuliko usalama wa Nchi zao i.e raia na mali zao, chukulia Ufaransa kwa mfano: Taifa lao ndilo ushambuliwa mara kwa mara na magaidi, wamepoteza raia wengi kutokana na Ugaidi, mapema mwaka huu Ufaransa ilipo kumbwa na Ugaidi Putin aliwahi kumpa pendekezo Hollande kwamba washirikiane huko Syria ili watokomeze kundi hatarishi la ISIS/Daesh/Al-Nusra, mwanzo Hollande alijitia kukubali pendekezo la Putin lakini hakushiriki, baadae akageuza kibao na kuanza kumlahumu Asaad na Serikali yake - watu hawa akili zao matope kabisa - yaani wameshikwa na makucha ya Wamerikani kila sehemu hawafurukuti kabisa, awawezi kufanya mahamuzi yoyote bila ya kupata kibali cha Serikali ya Merikani kwanza, unaweza kufikiri Serikali zao zimekwenda likizo!!!

Sasa, hasa hasa ni nini kinagomba kuhusu Asaad, kwa nini Mataifa ya magharibi yamepania kuhakikisha Asaad anaondolewa madarakani - jibu ni kwamba kuna sababu kuu mbili:

Ya kwanza: Ni ile inayo husu mpango wa Merikani, Qatar na Saudi Arabia kujenga bomba la gesi kupitia Syria kwenda Ulaya, zamani Marekani walijaribu kumuomba/shawishi Asaad wapitishe bomba hilo nchini mwake Asaad aliwakatalia for a reason, Asaad alitambua hizo ni njama za kutaka kudhoofisha Urusi kiuchumi na kwa kuwa Urusi ndiyo Taifa lililo kuwa linashirikiana sana na Syria tangu ya miaka ya hamsini/sitini, Asaad akaona kwa nini akubaliane na mapendekezo ya Project ya ujenzi wa bomba kupitia nchini mwake lenye lengo la kuhujumu Urusi kiuchumi, Merikani na washirika wake walikasirika sana - wakaona ili kuondoa kizingiti lazima Asaad aondoke madarakani i.e regime change, hilo la kwanza.

La pili: Linahusu Iran - Merikani na wenzake waliplan kwamba Asaad akisha ondolewa madarakani atakaye fuata katika crusade ya regime change litakuwa ni Taifa la Iran, njama hizi wapo pamoja na Saudi Arabia, Qatar na zamani Uturuki (tangu Serikali ya Uturuki inusurike kupinduliwa ,sijui kama wana hamu tena na siasa/mbinu hatarishi za Wamerikani).

Wamerikani walipanga kwamba wakisha fanikisha kuondoa Serikali za Syria na baadae Iran watayatumia Mataifa hayo ku recruit waasi wengi kwa kuwapa mafunzo, fedha na silaha ili wakamilishe Grand Plan yao ambayo ni ku unleash waasi wengi iwezekanavyo kuingia ndani ya Taifa la Urusi, baadae waanze kushambulia na kufanya hujuma katika miji na vitongoji vyake vile vile kuhujumu mihundo mbinu nchini Urusi na lengo la njama hizo ni kutaka kulifanya Taifa la Urusi lisitawalike - hizo ndizo zilikuwa plan za muda mrefu za utawala wa Merikani yaani wanatekeleza ushauri wa Dr. Zbigniew Kazimierz Brzezinski to the letter!!! - Someni vitabu vya kichaa huyu specifically kitabu kinacho julikana kwa title ya 'The Grand Chess Board' ndiyo mtajua kwamba kumbe yanayo tokea Africa Kasikazini, Mashariki ya kati na Ulaya yalipangwa na Merikani siku nyingi tangu baada ya vita ya pili ya Dunia, yanatekezwa kwa hatua moja baada ya nyingine hayatokei kwa bahati mbaya hata kidogo - kichaa huyu mwenye asili ya Poland anasukumwa na chuki zake binafsi kuhusu Taifa la Urusi na cha hatari zaidi bado ana wafuasi wengi kwenye Establishment including Pentagon Top Brass, kitabu chake wanakichukulia kama msaafu/Biblia!! Mawazo ya kichaa huyu hayana tofauti na ya Dikteita Adolf Hitler!! Merikani anakazania kug'ang'ania kanda/eneo la Kasikazini mwa Africa, Mashariki ya kati na Barani Ulaya hilo kutokana na factors zifuatazo:-
1) Zaidi ya robo tatu za natural resources nje na chini ya aridhi zinapatija,kabda hiyo
(2) Asilimia 75 % ya World population inaishi ndani ya kanda hiyo.
(3)Robo tatu za vyanzo vya nishati Duniani vinapatikana ndani ya kanda hiyo.
(4) Mbili ya tatu ya uchumi mkubwa na uzalishaji mkubwa viwandani unapatikana kanda hiyo.
Kati ya nchi ndani ya kanda hiyo Urusi ndiyo inaongoza katika utajiri wa mali asili Duniani.

Establishment ndani ya Taifa la Merikani inajua vizuri utajili mkubwa unao patikani katika Ukanda huo, yaani: Africa Kasikazini, Mashariki ya kati na Ulaya ikiwemo Urusi, wao kanda yote hiyo inajulikana kama EURASIA, Wamerikani wana amini kwa moyo wao wote kwamba Taifa lolote likifanikiwa kutawala au tuseme kuwateka akili viongozi wote wa kanda hiyo, basi Taifa hilo litakuwa limefanikiwa kuitawala Dunia - ndio maana Marekani katika harakati zake za kuteka akili viongozi wa Ulaya waliazisha NATO wakati hapakuwepo ulazima wowote baada ya vita ya 2 ya Duniani na kuanzishwa Umoja wa Mataifa, Marekani walikwenda mbali zaidi kuanzisha EU behind the scene watu awawezi kuamini, lakini the brains behind uanzishwaji wa EU ni Merikani yenyewe - ndiyo maana Uingereza ilipo jitoa EU Amerika/Obama ilikasirika sana na kufikia hatua ya kutaka kuhujumu Benki za Uingereza - we fikiria watu hawa walivyo na akili za ajabu wanawahujumu hata wajomba zao!

Kikwazo kikubwa cha kinacho zuia Grand Plan za Merikani kuitawala kikamirifu Eurasia ni URUSI, ndiyo maana Viongozi wa Merikani uisema sema Urusi, kuisingizia vitu chungu nzima, kufanya fitina nchi za Ulaya zisielewane na Urusi, kuwatisha tisha raia wa Ulaya kwamba Warusi wana mpango wa kuwavamia - vyombo vya habari karibu vyote Barani Ulaya vimenunuliwa na Merikani kusambaza propaganda za Uongo tu, zote hizo ni mbinu za Amerika kutafuta mbinu za kuendelea kug'ang'ania Barani Ulaya na kusifanya Serikali za Barani Ulaya ziamini kwamba bila ya Amerika kuendelea kubaki Barani Ulaya nchi hizo zitavamiwa na Urusi, Viongozi wa Ulaya wanakuwa mazezeta sijui kwa nini hata Rais wa Filipino kawazidi akili.

Merikani haitaki mshindani katika masuala ya Geopolitics wanaona adui wao mkubwa anaye zima ndoto zao za kuitawala Dunia kwa kuikalia Eurasia ni Warusi - Marekani wako tayari Dunia yote ihangamie kwa vita kutoka na uchu wao wa kutaka kug'ang'ania kanda ya Eurasia wakifanikiwa kuisambaratisha Urusi hizo ndizo ndoto zao za Alinacha - wanataka wao ndio wawe alfa na omega, for a starter mnaona kinacho endelea ndani ya Umoja wa Mataifa, juzi juzi hapa bila aibu Merikani iliwahi kutoa pendekezo eti Urusi iondolewa Umoja wa Mataifa, je mtu mwenye akili timamu unaweza kuamini kauli za kishenzi kama hizo, wasisahau kwamba Urusi is not a banana Republic, Marekani ikitaka kipigana nayo vita Urusi hiko tayari we can guess the outcome and Uncle SAM knows it, ndiyo maana anakusanya kusanya vijinchi chungu mzima vimsaidie just in case, hiyo ni kawaida/hulka za wadhalimu na watu woga Duniani ndiyo walivyo, Marekani haitaki kufa/angamia peka yake inataka nchi za Ulaya zi go down with her - wala sishangai watu/Taifa lisilo jiamini ukimbilia kutafuta coalition of the so called WILLING - haya ni mambo ya kisaikoloji yaani kujaribu kujenga impression kwamba wako wengi kwa hiyo wanaweza kufanya lolote.

Nimalizie kwa kusema kwamba kwa bahati mbaya Taifa la Merikani kutokana na viburi vyao ilijifunzi kitu miaka nenda rudi masaa yote wana behave like a spoilt Brat, hawajui hata jinsi ya ku address binadamu wenzao, jaribu kulinganisha majibu ya yule mama Balozi wa Merikani Umoja wa Mataifa, hana lugha ya kidiplomasia hata kidogo unaweza kufikiri aliokotwa barabarani na kupachikwa cheo - uwezi kulinganisha yeye na Maria Zhakarova kwa mfano, Maria yuko cultured kabisa, tufauti za behaviour za nama huyo na Maria ni kama kulinganisha Mbingu na Dunia.

Balozi wa Merikani ni jeuri, majivuno na kujiona Taifa lao ni exceptional na ujinga huu ndio utawamaliza wao na Taifa lao wasipo jirudi, wakumbuke hata Pharao aliamini yeye ni Mungu.

Binafsi nilipo ona sura ya Balozi wa Merikani Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza nilifikiri labda ni transgender - behaviour zake zina walakini mkubwa, I hope Administration inayo kuja itasitisha utehuzi wake Umoja wa Mataifa.

Cc: Malcom Lumumba, Appolo,DotWorld,Moh, LeeVancleef, Richard,Elungata.p
 
Hatufahamu makubaliano kati ya Russia na China kwenye hili na ukimya wa China na inaweza kuleta matatizo makubwa kwa Marekani.

Pili, Marekani pia hafahamu ni makubaliano gani Russia na China wamefikia khasa baada ya kitendo cha China kutoshiriki kwenye mkutano wa baraza la Usalama la UN juzi.

Lakini tunaweza kuondoa wasiwasi kwani China nao ni taifa kubwa sasa hivi kiuchumi na kijeshi, hivyo yeye angoja zamu yake.

Habari mpya zinasema kuwa Wizara ya mambo ya nje ya Uchina kupitia naibu waziri wake,
imesema hata kama Uchina hawakupiga kura bado wanakubaliana na msimamo wa Urusi kuhusu Syria na Afghanistan. Hivyo Beijing itaendelea kuwepo upande wa Urusi kwenye masuala muhimu ya Ulinzi na Usalama kikanda na Kidunia.
Na ikumbukwe mchina hakupiga kura ya Kwenye Azimio la Mfaransa, lile Azimio la Urusi kuhusu Syria alilipigia kura.

Jana mashirikia ya habari ya Marekani kama ABC na The Guardian waliandika kwamba kitendo cha kutopiga kura Uchina ni dalili ya Mrusi kutengwa na dunia kwenye masuala ya Mashariki ya kati haswa haswa Syria.
Sasa ukitaka ujue kwamba mashrika ya kimarekani ni propaganda tupu, hebu soma hiyo link ya ABC na RT uone tofauti mkubwa. Wazungu wamesema Uchina kamtenga Urusi wakati hakuna kitu kama hicho.

Chanzo:Russia vetoes UN resolution to stop bombing of Aleppo (Theguardian)
Chanzo: China supports Russian position on Syria & Afghanistan – Beijing (RT)
Chanzo: Rival Syria Resolutions by West and Russia Defeated at UN (ABC)

CC: mng'ato , Apollo
 
Kwa iyo kwa akili zako wewe,RT wakiandika un aamini moja kwa moja sio propagonda ila ABC wakiandika wewe kwako ni propaganda..Alafu hapo hapo unatumia Google search engine za marekani kupata link zako.
 
Jana Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Taifa ndiye aliwapasha vizuri Waingereza alisema tatizo lao bado wana Colonial Mentality - binafsi naona tatizo hilo hata Wafaransa wanalo sana.

Tukumbuke Syria iliwahi kuwa koloni la Ufaransa hawampendi Asaad lakini anaye vuta strings na Amerika, wanatumia Ufaransa kujaribu kumzuga Putin kumbe mwenzao kesha wasoma siku nyingi ndio maana mjumbe wa Ufaransa aliye kwenda Klemlin kuonana na,Putin na kumpa mapendekezo ya Ufaransa ya kusitisha mapigano, Putin hakumpa Mfaransa huyo jibu la moja kwa moja Urusi ilisubiri kutumia kura yake ya trufu kuzima njama za Ufaransa na Merikani.

Mimi kinacho nidhangaza kuhudu nchi hizi za magharibi specifically Ufaransa,Uingereza na kinara wao Uncle SAM ni kule kupuuzia hatari zinazo letwa/sababishwa na Ugaidi Duniani wanajali maslahi zaidi kuliko usalama wa raia wzo na mali zao

Kumbe lilikuwa koloni la Ufaransa. Hapo pia ni sawa wanalipiza kisasi kwa ndugu Asaad kama walivyomfanyia Gaddafi na Sadam. Also kwenye huo mkutano Misri imeamua kuunga mkono Russia?

Uncle SAM na members wake wana tricks sana.
 
Russia ana option mbili tu,achague moja
1.Akubali no fly zone na kuacha ku bomb aleppo kuruhusu misaada ya kibinadamu,Sababu ameonekana ki crazy hadi anaenda ku bomb malory ya midaada akati alishapewa taarifa ya kila kitu na route hayo malori yatapopita.
2.Au ashuhudie misaada ya silaha nzito iki flow kwa waasi ili ashuhudie vita isiyoisha nchini syria.
My take.Kwa maono yangu sioni hata mmoja mwenye huruma na watu wa syria sio russia wala US.Wote wanaangalia maslahi tuu.Ingekuwa russia ana huruma na watu wa syria angepeleka ground forces kuwafukuza waasi na IS.Ground troops ndio wenye uwezo wa kuchagua kati ya raia mwema na muasi,sio ku bomb na midege eneo lote kisa tuu linashikiliwa na waasi.Watu wataendelea kufa na ku flow kwenda ulaya kwa ukimbizi.Bahati mbaya sana hawaendi urusi,wanaenda ulaya so russia hawezi hisi pain yoyote ku handle maelfu ya wakimbizi thats y anakuwa reluctant.
 
Kwa iyo kwa akili zako wewe,RT wakiandika un aamini moja kwa moja sio propagonda ila ABC wakiandika wewe kwako ni propaganda..Alafu hapo hapo unatumia Google search engine za marekani kupata link zako.

RT ina uhuru wa kutangaza bila kuwa influenced na marekani. Haitangazi kwa maslahi ya Uncle SAM.

Pia hiyo kauli ya China kuunga mkono Russia ni habari ya leo saa sita usiku. Hiyo kauli ya ABC ni habari ya kabla ya mazungumzo ya Li Baodong kuzungumza leo. Na bado channels za US hazijasema hilo.

3dc1a24a978b3d396427383587f0c258.jpg
 
Habari mpya zinasema kuwa Wizara ya mambo ya nje ya Uchina kupitia naibu waziri wake,
imesema hata kama Uchina hawakupiga kura bado wanakubaliana na msimamo wa Urusi kuhusu Syria na Afghanistan. Hivyo Beijing itaendelea kuwepo upande wa Urusi kwenye masuala muhimu ya Ulinzi na Usalama kikanda na Kidunia.
Na ikumbukwe mchina hakupiga kura ya Kwenye Azimio la Mfaransa, lile Azimio la Urusi kuhusu Syria alilipigia kura.

Jana mashirikia ya habari ya Marekani kama ABC na The Guardian waliandika kwamba kitendo cha kutopiga kura Uchina ni dalili ya Mrusi kutengwa na dunia kwenye masuala ya Mashariki ya kati haswa haswa Syria.
Sasa ukitaka ujue kwamba mashrika ya kimarekani ni propaganda tupu, hebu soma hiyo link ya ABC na RT uone tofauti mkubwa. Wazungu wamesema Uchina kamtenga Urusi wakati hakuna kitu kama hicho.

Chanzo:Russia vetoes UN resolution to stop bombing of Aleppo (Theguardian)
Chanzo: China supports Russian position on Syria & Afghanistan – Beijing (RT)
Chanzo: Rival Syria Resolutions by West and Russia Defeated at UN (ABC)

CC: mng'ato , Apollo

Thanks for the info.
 
Back
Top Bottom