mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,772
- 2,171
Kweli kabisa. Waache tabia za upinzani. Wawe kama TLP, UDP, nk hapo watachukua dola.Muda mrefu hofu ya watanzania ni nani mbadala wa CCM kama CCM ikiondolewa?
Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi niseme kweli nchi yetu bado haijashuhudia chama cha kuiondoa CCM hata kama CCM imechokwa sana bado wanaliona tumaini ndani ya CCM kuliko nje.
Kuna tabia fulani fulani zilizokuwa zinasababisha upinzania kudumaa na kushindwa kusonga mbele nazo zilipelekea kifo chao. Tabia hizo ni pamoja na:
i) Kuonesha kushindwa kwa CCM huku nao wameshindwa kuonesha umuhimu wao. Hili lilikuwa ni kosa kubwa
ii) Kutokuwa na agenda za kusimamia badala yake ikawa inasimamia madhaifu ya CCM na madhaifu hayo yaliporekebishwa ikapelekea kufeli kwao.
iii) Kushindwa kushirikiana na CCM hata kwa mazuri yanayoonekana na badala yake wakawa wanatafuta mabaya katika mazuri
iv) Hamu ya Upinzani kuingia ikulu kuliko kujiimarisha na kuaminisha watanzania wana uwezo wa kuwatumikia.
Naamini kama Umoja Party wakirekebisha madhaifu hayo na mengine watafika mbali kama mbadala wa CCM.