Kutoa penzi kwa mashart ni ujinga. Nilikuwa nimeajiriwa serikalini, huyu boss alinitesa ikawa kerooo, nikaamua kuandika barua niende masomoni nimkwepe huwezi amini hakuwai kupitisha barua yangu, nikienda halimashauri naambiwa mkuu wa kituo kwanza apitishe.
Alinifanyia visa vingi sana kazi za ziada napewa mm ili mradi tu nichelewe kutoka, ila kwa kuwa alikuwa MTU mzima alikuwa alazimishi, ananiambia kwa ustaarabu, anasisisitiza kha! Nilivyoona keroo nikaacha kazi kiroho safiii nikaenda shule. Sijutiii na maisha yanasonga.
Ahaaa maboss bana wote wabafanana baadae ya shule nikaanza kutafuta kazi tena kha! Huyu interview alitaka nimfate hotelin, sikwenda, akatoa offer twende nje ya nchi alikuwa anaenda kikazi, Nikablock. Kazi za watu ni mateso ila kama kazi ni yako unapata bila mashariti.
In short siwezi kutoa penzi kisa kazi bora ikose, mm sio mremavu nitafanya shughuri nyingine.