Kisa kingine, natoka Mwanga, kuna watu nilienda nao, narudi alone niko kwenye Noah, nikafika Mombo ilikua Jumamosi nikakuta vichwa kibao, sasa lile gari lilikua linakunywa mafuta hakuna mfano, nikaamua kupunguza gharama ngoja nile vichwa, sa kumi na moja jioni hio, destination ni Dar na gari haina Taa za Maana kwahio inabidi nikimbie niwahi kufika mjini kidogo.
Tukio la kwanza. ukipita kijiji cha mandera kabla ya kufika Wami, nikakutana na Fuso limeharibika na wameweka majani, kwakua nilikua speed kiasi nikayavaa yale mamiti wanayoweka, nusura niingie nyuma ya Fuso. Nikatoka hapo nikawa nalifuata basi la TYahmeed ili at least nioapte mwanga,
Tukio la pili, nikiwa nakaribia Bagamoyo saa tatu kasoro usiku, ghafla nikawaona punda watatu hivi wanakatiha barabara, wawili wanamalizia kuvuka halafu mmoja ndio amejaa kwenye site yangu, dah ilibidi nimvamie tu, gari iliyumba kiasi but ikusimama hadi pale Total Filling station Bagamoyo nikakuta gari imemumia kidoogo