Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,582
- 28,566
Ilikuwa inanyesha upande wa kushoto Mahakamani au kulia?Mwaka 2001 nilikuwa ndani ya Hice "public transport" ikiwa natokea Wilayani Kahama naelekea Kakola. Tulipo fika kijiji cha Lunguya, gari nilivyo panda ikiwa imesimama barabarani ikishusha abiria, nikishuhudia Mvua kubwa ikinyesha upande mmoja wa barabara na upande mwingine ikiwa hainyeshi na ardhi ni kavu kabisa.....
Hili jambo lilinishangaza sana hakika
Chai watu wa eagle hawapigiwi saluti na hawajitambulishi hovyoNaendelea sasa akaja kwangu akanigongea kioo nikashusha kidogo akaanza kuporomosha matusi..bila kujua pembeni yangu kushoto alikuwa amekaa mtu mmoja mkubwa sana kutokea pale eagle house,alivomuona akaomba radhi na kupiga saluti na kisha kuondoka zake kurudi kwenye gari yake.
Ha ha ha!Tulikuwa kwenye kwenye foleni ya junction ambayo haina taa wala askari,sasa magari ya mbele yakawa yanajichomeka chomeka bila mpangilio tu mwisho wakazua foleni gari hazitembei.
Nikawa napiga honi kwa mtu wa mbele yangu za kumtia mtu hasira ajione mzembe(kama zile za mabasi ya mkoani au fuso) .
Kumbe yule wa mbele alikuwa ni mjeda akashuka kwenye gari yake bhana akanifwata nyuma....
Nitarudi ngoja kwanza niende toilet
Kitu inakua na 240 hahahaha hongera sanaUkiwa barabara kubwa na gari haina pulling da unateseka sana mi nakuwaga na V8 dereva anavyowakataga naona raha sana hadi dereva wangu ananionaga muhuni huwa namwambia tu watembezee moto hao basi anawakata tu ha ha ha ha ha njiani raha sana
Nilijua tu we mwanamke ungekuja kupinga andiko langu.Chai watu wa eagle hawapigiwi saluti na hawajitambulishi hovyo
Usitie shaka, anza na baiskeli kwanza!Meeyah mnanitenga kisa sina gari,sawa tu
baiskeli mkuu nikija barabarani IST ikinisukuma tu si mtanikuta muhimbili na POP kweli?Usitie shaka, anza na baiskeli kwanza!
Hizo ni ligi za wazoefu barabarani.Kisa cha pili, mwaka 2016 tunakwenda kula Pasaka Tanga, nilikua na kigari kidogo DUET ndio kwanza kimetoka kwa fundi, katikati huko tumeshapita Wami mbele huko kuna sehemu tamu sana zile...unapenda unshuka, unapanda unashuka aaaaghhh, wakaja jamaa wana Subaru nadhani zilikua Impreza kama sikosei, Subaru mbili na BMW saloon nadhani, wakanipita, muda huo kigari changu kimetoka gereji na kimewasha taa ya ABS, aiseee nikapelekana nao....wakaniacha mazima, sasa nikanogewa na ile ligi ya washkaji, nikawaona wameshuka kwenye down moja tamu sana nadhani ni KIMANGE pale halafu nikawaona wanapandisha kilima kingine, nikakanyagia na mimi DUET ikafika 130km/hr kana=suffocate vibaya, asa wakati napandisha kwenye kile kilima na mimi, mbele kukawa na lory limebeba mbao....nikaanza ku-overtake, ghafla ni lory lingine linashuka speed, na ile sehemu ilikua nyembamba...ninachokumbuka ni kwamba nilifunga break hadi gari ikajaa moshi kule mbele, nilikua naona kabisa naenda kuingia nyuma ya Lory, MUNGU saidia nilisimama kama mita tatu nyuma ya Lory, baada ya pale aaghhh acha tu. Nilisikia kiu kama vile nakufa
Yeah, Kaka MANI anaujua mziki wa Subaru, tulifuta kile kisahani. Ila ni enzi zile saa hizi sithubutu kuzidi hata mia japo mwaka jana tulimaliza kiasahani tukiwa na Crown AthleteHizo ni ligi za wazoefu barabarani.
Kama gari yako haina explosive pulling(rapid acceleration) usijarb hiz ligi.
Mi nimejaribu huo mchezo na gari kali tofauti, ni hatari lakini lazima uwe master wa control ama sivyo kama Kitona waweza jikuta unapaa hewani.
16/09/2016 tukiwa miongoni mwa abiria Mimi na mchumba wangu kwny basi la newforce kutoka DSM kuelekea songea,majira ya saa mbili usiku maeneo ya kifanya njombe basi lilipinduka na kutamatisha maisha ya mchumba wangu, sitakuja kusahau maneno ya mwisho mchumba wangu aliyonitamkia muda mfupi kabla hajakata roho,inauma sanaSalaam
Vyombo vya usafiri tunavitumia kutusaidia kutoka sehemu A kwenda B hivyo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, lakini pia vyombo hivi vinahitaji umakini wa hali ya juu sana uwapo barabarani kwani kosa moja linaweza kupelekea umauti, kilema, uharibifu au hata kupata kesi.
Pia muda mwengine unaweza kujitahidi kuwa makini sana katika uendeshaji wako lakini akatokea mtu tu akakosa umakini na kukusababishia matatizo, lakini pia yapo matatizo ya kiufundi yanaweza yakajitokeza na kusababisha ajali na dhahama.
Wapo wanaotukanwa au kutukanwa barabarani, wapo wanaopigana kisa uzembe wa barabarani, wapo waliopigwa risasi au kutishiwa kisa makosa ya ki uendeshaji na pia wapo wanaojikuta safari yao inakuwa chungu kutokana na jambo linalowakuta barabarani.
Uzi huu ni maalum kwa mikasa ya barabarani na kama limekukuta tueleze iwe kama somo kwa wengine, si lazima uwe na gari inaweza kuwa pikipiki, bajaji, na hata kama wewe ni abiria pia share yaliyo kukuta. View attachment 1262811
Traffic police kunipokonya ndizi mbivu zangu kisa Sina kipoza makosa on cash
Hahaha nina mikasa mingi tu
ngoja nianze na hii ninayokumbuka, Mkasa wa kwanza, nilikua naenda Kyela, naendesha na niko alone, safari ilianza saa kumi jioni, nikajivuta hadi Kiabaha ilikua siku ya Jumamosi nikamfuata Bro, tukala Mbuzi kwanza nikaendelea na safari nikafika Moro nikaonana na rafiki yangu kipenzi, tukapiga story hivi kidogo saa nne nikaanza safari. Niliendesha usiku mzima, Makambako nikafika saa kumi usiku, sasa pale mbele Ilembula kuna mji nadhani siju ndio Igawa...kulikua na road maintance, nilikua nimechoka kwahio hata vision ilikua ndogo, mbele kulikua na lori, ghafla kumbe nimefika mwisho wa lami nimeanza rough road duuhhh, nikafunga break ghafla ili kupunguza mwendo aiseee, yaani gari iliserereka kuifuta lile lory. Kulikua na baridi lakini nilihisi kuloa jasho. Sitakaa nisahau
Nimekubali Boss, kesho asubuhi nitafika pale junction MkuuLeta kesho ofisini leseni yako tuikague!ikiwezekana tusikuruhusu kbs!
PoleGari yangu kugongwa na daladala kwa nyuma.
Alikuwa na njaa huyoTraffic police kunipokonya ndizi mbivu zangu kisa Sina kipoza makosa on cash
Ukaenda ku.......Mimi niliwahi kusimamishwa na wana usalama nikakaidi mara ghafla nikaona mkonga inaingizwa road kunifukuzia, nilinyoosha goti na mtanange ulichukua takribani dakika 45 nikawaacha mbali sana ila walifanya mawasiliano nikafungiwa njia na gari kama nne hivi za jeshi la Polisi kutoka mji mwingine na hapo mambo yakafikia tamati.
Aiseee,alisemaje16/09/2016 tukiwa miongoni mwa abiria Mimi na mchumba wangu kwny basi la newforce kutoka DSM kuelekea songea,majira ya saa mbili usiku maeneo ya kifanya njombe basi lilipinduka na kutamatisha maisha ya mchumba wangu, sitakuja kusahau maneno ya mwisho mchumba wangu aliyonitamkia muda mfupi kabla hajakata roho,inauma sana