Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

Kwenye mguu nina kovu la pkpk xl, nilikunywa pombe nikawa narud zangu home, mvua ilikua imetoka kunyesha dah sijui ilikuaje nkajikuta mguu mmoja joto limezid kuinua pkpk siwezi wee,
Lakini sahiz mm ni mshindi aliye fanikiwa kuacha pombe kabisa.
Dah! Hongera sana kwa kuacha tembo mkuu.
 
Mimi nilikoswa na semi nilikuwa naendesha bajaji Natoka stendi kuingia barabara kuu ya lami nikasimama kucheki kushoto na kulia kuangalia usalama niingie lami mzee kushoto kwangu nikaona gari kwa mbali sana inawaka mataa nikajiaminisha ni basi liko mbali kwa hiyo nikaingia lami,ile nakanyaga lami tu kama sekundi tu semi likafunga breki kali sana nyuma ya bajaji hadi tela likapinda likaziba barabara.

Ili kukwepa kunigonga basi mapigo yangu ya moyo yalienda kwa kasi sana kwa kukosa kugongwa na lori nilichanganyikiwa nikawa sijielewi kabisa kama ni mimi, sasa dreva wa semi akaanza kunitukana sana mimi nikawa namuomba msamaha tu maana nilikuwa na kiwewe cha kufa mtu,huku tena abiria nilikuwa nimembeba akawa ananitupia lawama eti nataka kumuua familia yake itabaki na nani.dreva wa semi alikuwa kafungulia mafuta mpak mwisho ilikuwa mida ya saa mbili usiku muda ambao malori yanakuwa mengi barabara ya dar-mwanza hili tukio limeacha kumbukumbu miongoni mwa masaibu niliopitia ilikuwa natoka stendi mpya naelekea mjini Nzega Tabora.
Dah! Mungu alikunusuru aisee
 
Nilitoka boda horohoro sa 11 jioni na gari haina namba kuja bongo ila full dokomaa, nilipofika segera nikachukua cartoon ya castle ili nizugie na pakt ya embassy nikafungua moja nikainywa nikaitupa ili nivuke kabuku rd block. Askari pale akanikagua mwisho akaona laga siti ya nyuma akauliza za nani nikamwambia za kwangu ili nitakapochoka nizinywe nilale akasema nazikabidhi ktuoni Sikh nikipita siendeshi nizipitie akabeba na embassy 10. Iliniuma sana

Huyo Polisi alikuwa na akili sana.
Sigara ilitakiwa akuachie uende nazo, lakini kukunyang’anya kilaji alifanya jambo la maana.
Aliokoa uhai wako na wa wengine huko ulikokuwa ukienda.
 
Mimi mkasa wangu ni watofauti kidogo. Huwa napenda sana kusafiri usiku nikiwa naendesha gari mwenyewe. Nakumbuka mwaka jana around April nilikuwa natoka kigoma naenda Geita. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuendesha hiyo njia kwa hiyo nikatumia msaada wa Google Map.

Safari ilianza saa mbili usiku, saa tatu na nusu nilikuwa kasulu, saa sita kasoro nilikuwa Kibondo. Hapo nikashuka nikanunua Redbull, nikanywa saa saba kamili nikaamsha. Sasa ukiwa unatoka kibondo unaitafuta Kakonko, kuna sharp corner moja ambayo kama sio mzoefu au unapita usiku ni vigumu kuiona. Na bahati mbaya hapo network ipo chini.

Sikuiona hiyo corner, nikanyoosha. Network inakamata nilikuwa kama km 60 hivi niingie Burundi. Nikaona isiwe kesi nikageuza gari nikarudi nikaipata ile corner safari ikaendelea.

Ubaya wa Google map kwa wakati ule walikuwa hawaja update barabara hii mpya inayounga Kakonko na Kibondo, so walikuwa na ile ya zamani ambayo ilikuwa haitumiki. Bwana wee nikapita hiyo njia, Mungu saidia nikatoboa nikaipata njia mpya mwendo.. nikapita Kakonko vema mpaka Nyakanazi.

Sasa ukiwa Nyakanazi, Google Map inaonesha njia ya kufika Geita ni kupitia Biharumo, wakati kiuhalisia kuna hii ya Runzewe (Hii nilipita wakati narudi).

Hiyo safari ilikuwa ndefu sana , ilinifurahisha maana nilijifunza na maeneo mengi. Gari niliyokuwa natumia ilikuwa Land cruiser Prado, na mimi sio mkimbiaji sana. So safari hiyo ya Biharamuro, nikazunguka nikaingia Geita Saa nne Asubuhi.

Tired but excited
Hici wameacha kuteka maana kati kati ya kakonko na kibondo hua wanateka
 
Nilikamatwa naendesha ndiga nikiwa tungi kipimo kilikuwa kinasoma 265 alcohol
Polisi waliniambia mimi sio mtu labda mzimu, wakanisweka ndani kesho yake kwa court.Hakuna rangi niliacha kuona kwani pesa ilimwagika vya almanusura ninyanganywe leseni ambayo ndo kibarua changu
Hakika sitarudia tena kunywa kwa kiwango hicho na kudrive
 
Kuna traffic police mmoja kituo cha kivukoni pale ana tabia ya kuvizia uki park pale kwenye zile parking pembeni ya kituo .. hana kazi nyingine zaidi ya kubahatisha makosa pale kweny parking.. alinizuia kisa natembea na spare tairi wakati nimetoka kupata pancha nikabadili muda si mrf.. alichukua pesa yangu kwa kuwa nilikua na haraka sikutaka mambo yawe mengi.. huwa namuona sana anavizia watu pale kwenye parking
 
Pale Barabara ya 15 nilikuwa zangu misele kama unavyofahamu vijana wengi wa ki Tanga,
Basi nimefika makutano ya barabara ya jamaa kwa 15 nakuta ugomvi vibaka na Mpemba.

Akaniambia yakhe nianzimishe baiskeli yako sheikh
bila hili wala lile nikampatia.

Mara akatoa tube upepo... aaakh huyu Mpemba vipi tena...nikathubutu kumuuliza yakhe mie sikuelewi wafanyaje?

Mara akaanza kujaza upepo....hee si dakika nyingi nikaskia mtu analia ..."jamani tumbo langu..."

Ikabidi tumbembeleze Mpemba atoe upepo mtu apone
Akarejesha poshi lakini wapi.....


Funzo
"Kama wewe unajiita baba lao ujue kuna mwamba lao...."
 
Yalaaaaa, nimepigwa pasi ya mkaa!
259a1289d394b9205f252e941a42e575.jpeg
 
Nilikamatwa naendesha ndiga nikiwa tungi kipimo kilikuwa kinasoma 265 alcohol
Polisi waliniambia mimi sio mtu labda mzimu, wakanisweka ndani kesho yake kwa court.Hakuna rangi niliacha kuona kwani pesa ilimwagika vya almanusura ninyanganywe leseni ambayo ndo kibarua changu
Hakika sitarudia tena kunywa kwa kiwango hicho na kudrive
Ulimwaga pesa ukiwa mahakamani au ulivokuwa ndani police
 
Mimi niliwahi kusimamishwa na wana usalama nikakaidi mara ghafla nikaona mkonga inaingizwa road kunifukuzia, nilinyoosha goti na mtanange ulichukua takribani dakika 45 nikawaacha mbali sana ila walifanya mawasiliano nikafungiwa njia na gari kama nne hivi za jeshi la Polisi kutoka mji mwingine na hapo mambo yakafikia tamati.
Ulikosea,baada ya kuwaacha kwa mbali sana ungechepuka pembeni halafu uwaangalie wakipita tu unarudi road,unageuza kurudi ulikotoka. Machafuuuuu
 
Ulikosea,baada ya kuwaacha kwa mbali sana ungechepuka pembeni halafu uwaangalie wakipita tu unarudi road,unageuza kurudi ulikotoka. Machafuuuuu
Yote hayo yamefanyika na nimesha eleza humu mkuu.
 
Yalaaaaa, nimepigwa pasi ya mkaa!View attachment 1264933
Bodaboda wanaopakia vitu vipana kuliko pikipiki kisha wanajaribu kupenya kama pikipiki wananichemsha damu vibaya mno!

Yani mtu ana mzigo mpana kama gari kisha anaendesha kama vile hana mzigo kupenya katikati ya magari.

Hiyo ishu iliishaje hapo? Maana kwa kuangalia michirizi ni yeye aliyeforce kupita kati yako wewe na basi, ngoma ikawa ngumu mbele.
 
Kilichofuata?
Mimi niliwahi kusimamishwa na wana usalama nikakaidi mara ghafla nikaona mkonga inaingizwa road kunifukuzia, nilinyoosha goti na mtanange ulichukua takribani dakika 45 nikawaacha mbali sana ila walifanya mawasiliano nikafungiwa njia na gari kama nne hivi za jeshi la Polisi kutoka mji mwingine na hapo mambo yakafikia tamati.
 
Back
Top Bottom