Mimi mkasa wangu ni watofauti kidogo. Huwa napenda sana kusafiri usiku nikiwa naendesha gari mwenyewe. Nakumbuka mwaka jana around April nilikuwa natoka kigoma naenda Geita. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuendesha hiyo njia kwa hiyo nikatumia msaada wa Google Map.
Safari ilianza saa mbili usiku, saa tatu na nusu nilikuwa kasulu, saa sita kasoro nilikuwa Kibondo. Hapo nikashuka nikanunua Redbull, nikanywa saa saba kamili nikaamsha. Sasa ukiwa unatoka kibondo unaitafuta Kakonko, kuna sharp corner moja ambayo kama sio mzoefu au unapita usiku ni vigumu kuiona. Na bahati mbaya hapo network ipo chini.
Sikuiona hiyo corner, nikanyoosha. Network inakamata nilikuwa kama km 60 hivi niingie Burundi. Nikaona isiwe kesi nikageuza gari nikarudi nikaipata ile corner safari ikaendelea.
Ubaya wa Google map kwa wakati ule walikuwa hawaja update barabara hii mpya inayounga Kakonko na Kibondo, so walikuwa na ile ya zamani ambayo ilikuwa haitumiki. Bwana wee nikapita hiyo njia, Mungu saidia nikatoboa nikaipata njia mpya mwendo.. nikapita Kakonko vema mpaka Nyakanazi.
Sasa ukiwa Nyakanazi, Google Map inaonesha njia ya kufika Geita ni kupitia Biharumo, wakati kiuhalisia kuna hii ya Runzewe (Hii nilipita wakati narudi).
Hiyo safari ilikuwa ndefu sana , ilinifurahisha maana nilijifunza na maeneo mengi. Gari niliyokuwa natumia ilikuwa Land cruiser Prado, na mimi sio mkimbiaji sana. So safari hiyo ya Biharamuro, nikazunguka nikaingia Geita Saa nne Asubuhi.
Tired but excited
