Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

jana bwana mitaa ya melela trafiki kanikamata gari haina tatizo ananiuliza hujakaguliwa huko kote nikamwambia niko full nikamuonesha triangle na fire extinguisher nimeziweka siti ya mbele akaniambia sijala nikampa elfu 3 nikasepa alafu alikua wakike nusura niombe namba manake akawa ananiuliza naenda wapi
Umezingua why hujaomba namba..!!
 
jana bwana mitaa ya melela trafiki kanikamata gari haina tatizo ananiuliza hujakaguliwa huko kote nikamwambia niko full nikamuonesha triangle na fire extinguisher nimeziweka siti ya mbele akaniambia sijala nikampa elfu 3 nikasepa alafu alikua wakike nusura niombe namba manake akawa ananiuliza naenda wapi
Dah! Si mchezo.
 
Kuna traffic police mmoja kituo cha kivukoni pale ana tabia ya kuvizia uki park pale kwenye zile parking pembeni ya kituo .. hana kazi nyingine zaidi ya kubahatisha makosa pale kweny parking.. alinizuia kisa natembea na spare tairi wakati nimetoka kupata pancha nikabadili muda si mrf.. alichukua pesa yangu kwa kuwa nilikua na haraka sikutaka mambo yawe mengi.. huwa namuona sana anavizia watu pale kwenye parking
Njaa mbaya.
 
Salaam
Vyombo vya usafiri tunavitumia kutusaidia kutoka sehemu A kwenda B hivyo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, lakini pia vyombo hivi vinahitaji umakini wa hali ya juu sana uwapo barabarani kwani kosa moja linaweza kupelekea umauti, kilema, uharibifu au hata kupata kesi.

Pia muda mwengine unaweza kujitahidi kuwa makini sana katika uendeshaji wako lakini akatokea mtu tu akakosa umakini na kukusababishia matatizo, lakini pia yapo matatizo ya kiufundi yanaweza yakajitokeza na kusababisha ajali na dhahama.

Wapo wanaotukanwa au kutukanwa barabarani, wapo wanaopigana kisa uzembe wa barabarani, wapo waliopigwa risasi au kutishiwa kisa makosa ya ki uendeshaji na pia wapo wanaojikuta safari yao inakuwa chungu kutokana na jambo linalowakuta barabarani.

Uzi huu ni maalum kwa mikasa ya barabarani na kama limekukuta tueleze iwe kama somo kwa wengine, si lazima uwe na gari inaweza kuwa pikipiki, bajaji, na hata kama wewe ni abiria pia share yaliyo kukuta. View attachment 1262811
Juzi tu, kijasho chembamba kilitoka
255743464998_status_6ef2f22533f94292be1012f69f9f469d.jpeg
 
Juzi juzi hapa natahamaki boda boda na abiria wake wako mvunguni, waliingia barabara kubwa ghafla bila kuangalia.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom