Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,444
11,941
Salaam
Vyombo vya usafiri tunavitumia kutusaidia kutoka sehemu A kwenda B hivyo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, lakini pia vyombo hivi vinahitaji umakini wa hali ya juu sana uwapo barabarani kwani kosa moja linaweza kupelekea umauti, kilema, uharibifu au hata kupata kesi.

Pia muda mwengine unaweza kujitahidi kuwa makini sana katika uendeshaji wako lakini akatokea mtu tu akakosa umakini na kukusababishia matatizo, lakini pia yapo matatizo ya kiufundi yanaweza yakajitokeza na kusababisha ajali na dhahama.

Wapo wanaotukanwa au kutukanwa barabarani, wapo wanaopigana kisa uzembe wa barabarani, wapo waliopigwa risasi au kutishiwa kisa makosa ya ki uendeshaji na pia wapo wanaojikuta safari yao inakuwa chungu kutokana na jambo linalowakuta barabarani.

Uzi huu ni maalum kwa mikasa ya barabarani na kama limekukuta tueleze iwe kama somo kwa wengine, si lazima uwe na gari inaweza kuwa pikipiki, bajaji, na hata kama wewe ni abiria pia share yaliyo kukuta.
1573716052-picsay.jpeg
 
Mwaka 2001 nilikuwa ndani ya Hice "public transport" ikiwa natokea Wilayani Kahama naelekea Kakola. Tulipo fika kijiji cha Lunguya, gari nilivyo panda ikiwa imesimama barabarani ikishusha abiria, nikishuhudia Mvua kubwa ikinyesha upande mmoja wa barabara na upande mwingine ikiwa hainyeshi na ardhi ni kavu kabisa.....
Hili jambo lilinishangaza sana hakika

Alafu... Sijui kwanini tu nimechangia kwenye huu Uzi, maana naona wachangiaji wote wanamiliki mikebe Daslam...
 
Mwaka 2001 nilikuwa ndani ya Hice "public transport" ikiwa natokea Wilayani Kahama naelekea Kakola. Tulipo fika kijiji cha Lunguya, gari nilivyo panda ikiwa imesimama barabarani ikishusha abiria, nikishuhudia Mvua kubwa ikinyesha upande mmoja wa barabara na upande mwingine ikiwa hainyeshi na ardhi ni kavu kabisa.....
Hili jambo lilinishangaza sana hakika
Mkuu ichi kitu sio maajabu sana.. Huwa inatokea mara kwa mara
 
tembea tembea yangu bila kuangalia

saa ngapi nisijikwae kidole cha mwisho hiki kidogo

asee hiyo siku nilivaa sendo,iliuma hiyooooooo

niliruka na ku danki danki kama mpira wa basket ball

sema siku hizi nikitembea Macho chini,sipend kabsa jikwaaa

Halafu leo asubuhi, saa ngapi nisidumbukie kwenye tope nilizani kumekauka

naweka mguuu mara umezama wote chubwiiiiiiiii

Bara Barani kuna maswaiba ndugu zangu acheni kabisa
 
Mimi niliwahi kusimamishwa na wana usalama nikakaidi mara ghafla nikaona mkonga inaingizwa road kunifukuzia, nilinyoosha goti na mtanange ulichukua takribani dakika 45 nikawaacha mbali sana ila walifanya mawasiliano nikafungiwa njia na gari kama nne hivi za jeshi la Polisi kutoka mji mwingine na hapo mambo yakafikia tamati.
 
Ni kitu cha kawaida sana kama unasafiri barabarani unatoka dar kwenda mwanza unaweza kukutana na mvua hata mara tano na jua pia unajikuta unaendaa kuna bonge la mvua mara kidogo unakuta imekata jua kaliii na mbele kukavuuu
Hazungumzii vijiji bali hapo alipokuwepo upande mmoja kuna mvua kubwa upande wa pili kuko safi.
 
Jamaa hawakukupiga kweli...
maana ukiwakimbia wakikudaka...
wanakuwa kama mbogo
Ni kweli ila nyakati hizo nilikuwa bado bwana mdogo sana na hata ujinga huo nilioufanya ulichochewa na umri, kilichonisaidia nilikuwa na watu watatu ndani ya gari na wao walikuwa wakubwa sana kwangu hivyo wao ndio walichezea kichapo na kuhojiwa kwa nini waniruhusu mimi nikimbie ilihali wao ni wakubwa zangu.
Hata hivyo baada ya upekuzi mkali hawakugundua chochote zaidi ya bima iliyokwisha....nilifuata hatua za kisheria na yalikwisha salama.
Barabarani kuna mengi sana ndugu.
 
kifinga, ekata jua kaliii na mbele kukavuuu

lkn ya Ushimen kiboko mvua imegawa barabara, kushoto radi na mafuriko kulia jua na vumbi
Hata Makuyuni kutoka Minjingu kwenda Arusha nilikuta mvua kubwa lkn ulikuwepo Mnada wa siku nikaona pakavu hasa, wakasema Wamasai wamezuia mvua hadi mnada uishe, ilibidi nisogee na mimi nikale nyamachoma ya kutundika, nikaenda kutafiti uganga wa mvua
 
Tulikuwa kwenye kwenye foleni ya junction ambayo haina taa wala askari,sasa magari ya mbele yakawa yanajichomeka chomeka bila mpangilio tu mwisho wakazua foleni gari hazitembei.
Nikawa napiga honi kwa mtu wa mbele yangu za kumtia mtu hasira ajione mzembe(kama zile za mabasi ya mkoani au fuso) .
Kumbe yule wa mbele alikuwa ni mjeda akashuka kwenye gari yake bhana akanifwata nyuma....
Nitarudi ngoja kwanza niende toilet
 
Back
Top Bottom