Kuna siku miaka ya 2008 nikiwa nimetoka naelekea zangu misele mida ya jioni saa 10, gari ilikua Haina road license kwa miaka ile, nikaingia barabara ya lami, nikachochea Niko speed 90, kipindi hicho hizi local roads magari machache na traffic wachache hivyo unafungua a tu, hamadi Kuna daladala ananichomekea, kushika break nimpishe yaani ni upepo Hadi mwisho was pedal. Breki hamna, nilipanick vibaya mnooo, lakini nilivyo maneuver kupita Kati Kati ya magari ni mungu tu Mana sikujiona Nina skills hizo, uzuri mbele unashuka mteremko halafu Kuna kilika kibwa hivi, nikacheza na gia Hadi moja, kwenye kupanda kilima gari ikapunguza speed Hadi nikaipaki diagonal ikasimama. Nikashusha pumzi Kama do 40 ivu, Kisha nakaanza Sasa kuisereresha kilima kutudi huku nacheza na gia, taratibu nkamaliza lami ile nainguia vumbi majembe hao, walikua na tenda ya kukamata magari yasiyo na bima na road license, gari Haina breki kusimama siezi nikaunga mbele kwa mbele wakanifata na toyo mi narnda taratibu tu Mana Sina breki tunaongea kabisa, nawaambia gari halina breki imekata nasereresha Hadi nyumbani, nilipofika nyumbani nikatafuta mwinuko nikapaki diagonal fasta nikashuka nikatia jiwe wakanimaind Sana na ukijumlisha Sina road license Sina bima yani ilikua noma, ila niliwaza 20 walikua wawili, nikawaambia mkizungua hate hiyo twenty hampati Mana gari nimepaki ni mbovu, ile gari sikuendesha Tena Hadi leo, nilikua kuiza Bei Chee sana