Umewahi Kumbana Na Vibaka?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi Kumbana Na Vibaka??

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Katavi, Aug 24, 2011.

 1. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Licha ya kukwapuliwa simu na vipesa ndani ya daladala lakini matukio haya mawili sitayasahau.....
  1..Siku moja j/pili nimetoka zangu kanisani mida ya saa saba, nikaamua kwenda kupunga upepo ufukweni. Nikashuka pale sokoni feri na kuanza kutembea taratibu kuelekea pande zile ilipo "white house". Ghafla mvua ikaanza kunyesha, ikabidi nijisitiri chini ya mti maana ilikuwa kubwa. Muda kidogo ile mvua iliongezeka na mara nikaona raia kama wanne wakija upande niliopo. Wakaja mpaka pale nilipo nao wakajifanya wanajikinga na mvua katika ule mti, sikuwa na wasiwasi(mbele ya ikulu ulinzi wa kutosha). Ghafla nilipigwa bonge la mtama na kabla sijatua chini nikatiwa kabari ya hatari, na wengine wakaanza kunisachi na kuchukua kila kilichokuwa mfukoni. Nashukuru Mungu hawakuchukua coins 250, ambayo ilinisaidia kiasi kama nauli ya kurudia nyumbani Mbezi.

  2..Tukio la pili lilinitokea miaka 11 iliyopita, napita vichochoro vya Ubungo maziwa ili nitokee ubungo stendi ya daladala nirudi zangu Mbezi. Ghafla akatokea jamaa nyuma yangu akaniambia "dogo simama nikuulize", kwa kumuona alivyo sikuwa na wasiwasi kabisa. Aliponifikia nilishangaa napigwa mtama na jamaa wengine wawili sikujua wametokea upande gani wakaanza kunisachi. Walichukua kila kitu hadi viatu, nusura wanivue hadi jinzi na tisheti kama si wapita njia wengine kutokea na wale jamaa kukimbia. Ilibidi "nijitoe fahamu" na kutembea pekupeku hadi Mbezi kwa mguu(hii siku sitaisahau), na sikumsimulia mtu yeyote huu mkasa mpaka leo hapa JF..

  Hawa watu ni balaa...Hivi umewahi kukumbwa na hawa jamaa???
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  duh, pole sana.. Mi walishawahi kunivua viatu kipindi nipo kidato cha kwanza,.. Hawa jamaa siyo kabisa!
   
 3. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Nashukuru Mungu umbo na muonekano wangu wa kimazoezi walau vinanisaidia kutokumbana na masaibu haya. Ila siku nikikumbana nayo nitakuja hapa kutoa ushuhuda wangu. Asante na poleni wandugu!
   
 4. Ipi dot com

  Ipi dot com JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 267
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Walinibana kekomwanga walinipa roba ya nguvu nikajikuta navua viatu mwenyewe
  waliponiachia nilipata nguvu baada ya dkk 5
  niliuguza shingo wiki 2 sitasahau
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Ahahahaah!! Ni noma kweli hawa jamaa, sijui wana roho za vipi!
   
 6. The great R

  The great R Senior Member

  #6
  Aug 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MTAA YA CHANG'OMBE,ctasahau tena nikiwa na hubby jamani ndani ya self car,walikwapua haandbag nzimaa.kila kitu kilienda cunajua cc tunaweka everything ndani ya handbag
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa kuwa na mwili wa mazoezi, ila inabidi uwe makini kila wakati maana hawa jamaa hawatabiriki.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Dah!! Pole sana...
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Pole sana, inaonekana ulilia sana siku hiyo!
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sina hamu na vibaka walishawahi kunishambulia kama mara mbili.
  Nilikuwa napita mitaa ya kinondoni mosko njia ya kwenda muhimbili Hospitali, nilivamiwa na vibaka kama watoto mmoja akanivisha ndoo ya plasitiki kichwani ikanifunika mpaka mabega nikawa sina ujanja wakachuwa pesa, simu, viatu, raia wema ndio wakanisaidia kuivua ndoo, nikaomba na maji ya kunywa kwa jinsi koo lilivyokauka kwa kiu
   
 11. mbongowakweli

  mbongowakweli Member

  #11
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Poleni wazee, mie nlivamiwa wakati fulani nikitokea kwenye maraha, mitaa ya tegeta uninuo, naingia tu kwenye taksi baada ya kushuka kwenye daladala, washenzi kumbe walishanimaki, wakachukua simu zangu 2, alfu tano na kuchana suruali yangu.

  Mara ya pili nilivamiwa nyumbani, wakavunja vidude vya geti vya kuweka makufuli halafu mlango, nikapiga simu kwa mapolisi defender, walivyosikia jamaa wana gobole, hawakuja!

  Wakuu sikieni hadithi tu, ila ikikutokea, wazee hata kulala inakua taabu mno, na ukipata usingizi unaota unavamiwa, ukisikia sauti roho inakwenda mbio.

  Na ndio maana nikisikia wanachomwa moto kwa kweli sina huruma nao, pamoja na kwamba sa ingine wanaochomwa wanakua wamesingiziwa.

  Nachukua vibaka na majambazi ile mbaya kabisa wakuu!!
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  vibaka stay away from me MEEEEEEEEEEEN narepresent ki sharabaaaaro zaiedi MEEEEEEEEEEEEEEEEEn stay fakaut from me vibakazz
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Dah!! Hao walidhamiria kuua kabisa, hawa jamaa ni hatari..
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Pole sana, hiyo ya kuvamiwa hadi nyumbani ndio mbaya zaidi...
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Na wao watakuibukia kisharobaro.....
   
 16. D

  Derimto JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ee Bwana sio kitu cha ajabu bongo kushambuliwa na vibaka nakumbuka kwa mara ya kwanza kabisa walikuwa sio wa nguvu sana walikuwa mateja mitaa ya sekei arusha kipindi hicho uchochoro wa mt.meru hotel kutokea mahakama kuu kulikuwa kumepoa sana saa 12: jioni wakadai za fegi nikawatolea nje wakataka kunifanyizia mara wapita njia wakongezeka nikasepa.

  Mara ya pili nilikuwa na shemeji yangu yangu tunatoka kwenye msiba unga limited na nilipewa jukumu la kuhakikisha namvusha mto aeleke upande wa lemara mida ya saa mbili usiku tukapita mfereji tukapishana na watu zaidi ya 10 kumbe walikuwa wanaelekea kazini na baada ya kuwapita walipotuona wakanyamaza kimya na kumbe 4 kati yao waligeuka njia na kuanza kutufuatia mgombani ili tufike mtoni watumalize na walikuwa wanaume wanaojitosheleza hasa 1 akatupita haraka akatangulia mbele bondeni kugeuka nyuma nikamwona wa pili anawaonyesha ishara ya mkono wale walioko nyuma wafanye haraka mzee nikajua nimekwisha sikumshtua shemeji yangu nilichofanya yule aliyekuwa anaita wenzake alipotaka kunipita kwenda mbele ili wa nyuma waje wanikabe nikenda mbele nikutane na wao kwa ujasiri nikamwuliza unawaita wale wenzako kwa mikono mnataka kufanya nini? Yule aliyetangulia mbele akadakia kwa matusi na kuanza kuturudia ili kumwongezea nguvu mwenzake huku wale wa nyuma wakiongeza mwendo kutujia sikutoa hiyo nafasi kabisa na sijui nguvu zilitoka wapi maana sikumbuki kama nimeshawahi kumpiga mtu ngumi ya kiwango hicho tena maana nilimpiga usoni ngumi ya woga aliye karibu yangu ambaye alikuwa na mwili mkubwa kuliko wote na alidondoka kama gunia la chumvi na mwenzake ambaye alikuwa anakuja kupanda kutoka mtoni nilimpiga teke la kifuani wote wakawa chini shemeji alipiga ukunga mkubwa ajabu vibaka waliobaki walivyoona wenzao wako chini na kelele imekuwa kubwa waktimua mbio. Ki ukweli haikuwa ni ujanja na uzoefu wangu bali aliyesaidia siku ni Mungu maana waliokuwa nyuma walikuwa na zana zao za kazi tungeweza hata kuuliwa.
   
 17. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  walishawahi kumchapa sana mdogo wangu, wao walijifanya wanachangisha pesa za mpira wakamwomba dogo, dogo akadai hana hela wakaruhusu aende, dogo alipopiga tu hatua kama saba likajitokeza litoto likampiga mtama hadi akaanguka, basi dogo akakazibua kibao kale katoto...
  Kilichofuata.....
   
 18. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa mida ya saa 3 asubuhi pale relini karibia na kurasini beach, yaani kama movie vile kisimu changu kikakwapuliwa alafu mwenzangu akapokonywa pochi! We acha tu ndugu, nikimkuta kibaka anapigwa wala simuonei huruma kabisa!
   
 19. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lakini ata mimi nilishawahi kumfanyia unyama kibaka mmoja alikwiba home.
  Nilivyomkamata nilimpa kikombe cha chai nikamwambia nataka asombe maji kwa kikombe mpaka ajaze pipa huku akichezea bakora za mgongo huku mguuni nimemfunga kamba
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Dah!! Hiyo adhabu ilimfaa sana..
   
Loading...