Visa vingine hadi vinachekesha kwa masikitiko. Kweli tatizo la vibaka ni kubwa sana Nchi hii karibu kila sehemu isipokua labda Makete tu maana huko kuna imani za kishirikina balaa. Nasikia ukidondosha hela yako kesho utaikuta palepale hamna atakaegusa. Natamani hiyo teknolojia yao wangeiweka kwenye vitabu itusaidie na sie wa maeneo mengine.<br />
<br />
Mie nimeondokewa na Mjomba wangu mwaka huu mwanzoni huko mbeya, alikua nyumbani kwake na mkewe majira ya saa 2 usiku maeneo ya airport akapata msg ya ugonjwa toka nyumbani kwa mama yake, hakuwa na credit kwy simu akatoka kwenda dukani kununua vocha umbali kama wa dkk 5 hivi. Akiwa anaweka vocha pale dukan kumbe vibaka walikua pembeni wanamuangalia, alipotoka tu kwenda home, kuna kijinjia chenye giza wakamvamia wakitaka simu, alikua na ubavu sasa katika vurugu ile walipoona wanazidiwa wakamzushia mwizi wa simu kamkaba mtu. Basi raia walitoka kwa wingi wakampiga sana mmoja wao akawasihi wammulike coz alikua kesha anguka chini na kapoteza faham, ndipo wakagundua ni jirani na wakati wananchi wanaingilia kati vibaka walichomoka mmoja baada ya mwingine. Alichukuliwa kwenda police ili apelekwe hosptali lakini alipofika police ali fariki bila hata kutoa kauli yeyote. Ina niuma mpaka leo hii. <br />
<br />
Poleni wote mliokumbwa na maswahibu ya hawa vibaka.