King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 946
- 1,747
Salamu kwa wote,
Nia yangu siyo kumsimanga mtu bali nataka tujifunze na si vinginevyo,
Twende kwenye hoja ya msingi,
Mtu anakupigia simu kwamba amekwama kwa jambo fulani linahitaji pesa, anaomba msaada wa kifedha kwa sababu amekama,
Unamwambia haina shida ntakusaidia, unaamua kumtumia pesa kwa njia ya mtandao na inaonesha kabisa pesa imetumwa, unasubiri akufahamishe kuwa pesa imefika au laa, unaona muda unazidi kwenda, unaamua kumpigia anakwambia nimepata nilisahau kukwambia, hii tabia inakera sana
Imewahi kunitokea mara kadhaa, wakati anaomba msaada anakupigia simu mara kibao, ukimtumia harudishi feedback, anakufanya upoteze muda kwenye banda la M-pesa ukisubiri mrejesho.
Yangu ni hayo tu kwa leo.