Jeshi la Polisi Mwanza na LATRA tatueni changamoto hii ya Daladala kukatisha ruti kibabe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Kwa sasa Mwanza kuna tabia ya asilimia kubwa ya Daladala kutofika katika ‘ruti’ zao husika walizopangiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) hasa zile zinazotoka Nyashishi kwenda Kisesa, nyingi zinaishia Igoma na wanasema kabisa wanaishia Igoma kama hutaki shuka.

Kwa hivyo, abiria wa Kisesa atakaepanda basi ajue akifika Igoma atafute gari nyingine au usafiri mwingine jambo linalosababisha kero na kuongeza gharama za usafiri kwa raia wa kawaida ambaye anaenda kwenye mizunguko yake ya kila siku.

Nilijaribu kuwasilisha jambo hili kwa mmoja wa maafisa wa usalama barabarani na alinipatia namba ya simu ikitokea nimepata changamoto hiyo.

Pamoja na kuwa mara kadhaa nimempigia kila tunapokutana na changamoto hiyo msaada hauonekani zaidi ya kuniambia ngoja niwasiliane na Askari aliyepo barabarani.

Ukimpigia tena anakwambia askari wote hawapo barabarani licha ya kwamba inakuwa bado mapema saa 11 au 12 Jioni ndio muda ambao kero hii inakithiri.

Tunaomba Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) upande wa Mwanza mtusaidie, tunaoteseka ni sisi Wananchi wa kipato cha chini kwa kulazimika kulipa nauli mara mbilimbili na kupoteza muda mwingi pia njiani.
 
Sio hivyo tu... Kuna zile zinazoenda Ilemela mahakamani, na zile za kwenda Airport... Ikifika usiku mara nyingi zinaishia Sabasaba au mitaa karibu na sabasaba...

Kuna za nyanshishi zingine wanakwambia wanaishia Buhongwa... Hawafiki mwisho
 
Unafikiri polisi traffic hawalijui hilo
Naona mnapaka rangi upepo

Ova
 
Achen makasiriko mnajua mda halisi wa kufunga kazi ya daladala kulingana na sheria za latra
 
Back
Top Bottom