Umewahi kukutana na Changamoto kama hii?

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Salamu kwa wote,

Nia yangu siyo kumsimanga mtu bali nataka tujifunze na si vinginevyo,

Twende kwenye hoja ya msingi,

Mtu anakupigia simu kwamba amekwama kwa jambo fulani linahitaji pesa, anaomba msaada wa kifedha kwa sababu amekama,

Unamwambia haina shida ntakusaidia, unaamua kumtumia pesa kwa njia ya mtandao na inaonesha kabisa pesa imetumwa, unasubiri akufahamishe kuwa pesa imefika au laa, unaona muda unazidi kwenda, unaamua kumpigia anakwambia nimepata nilisahau kukwambia, hii tabia inakera sana

Imewahi kunitokea mara kadhaa, wakati anaomba msaada anakupigia simu mara kibao, ukimtumia harudishi feedback, anakufanya upoteze muda kwenye banda la M-pesa ukisubiri mrejesho.

Yangu ni hayo tu kwa leo.
 
Pole sana Mkuu.

BINADAMU AKIWA NA SHIDA HUWA MTU MWENYE MANENO MENGI SANA, SHIDA ZIKIISHA HUWA ANASAHAU WALIOMSAIDIA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hapo kinachokupa tabu ni nini? Hilo ni funzo la siku nyingine
 
Wenzako tuliumizwa na jambo hilo tulipokuwa tunawatumia wapenzi wetu,tuliumia si kwa sababu mpenzi hana shukrani NO,ila sababu hiyo ni dalili mpenzi hana hisia na wewe,anakutumia kwenye shida zake tu.

Kama ni mtu baki kwanini akushughulishe!!maana umetoa bila kutarajia lolote kutoka kwake ni kama umetoa msaada tu.

kama ni mdogo wako tu tumbo moja sio kaka wala dada,au laah awe mwano wa kumzaa hapo ni rukhsa kumkemea na kumkumbusha,maana ni watu walio mikononi mwako bado.
 
Sawa mkuu
 
Kutokujua thamani ya kushukuru ni kipimo cha utu wa mtu pia.

Asieweza kutoa shukrani kwa msaada hata mdogo hawezi kuthamini hata neema kubwa za Mungu wake.

Ukiachilia mbali kutoa asante ni uungwana kutoa taarifa tu kuwa umepata ulichotumiwa.
 
Back
Top Bottom