Mm nimesoma vingi hata cjui niweke kipi
Wakuu ni mwisho wa mwaka tutumie hizi siku zimebaki kujitathmini usomaji wetu kama ilivyo deaturi yetu.
Mi usomaji wangi haukuwa mzuri. Nimesoma vitabu vitatu na vingine viwili sikumaliza.
1.A god who hate. Hiki kuna member Alisina niliona amekiupload.Nikakipakua na kikanivutia kusoma. Huyu mama muandishi anaeleza maisha ya mwanamke wa kiislamu na magumu yake. Pia anashutumu imani hiyo. Kinavutia na rahisi kusoma.
View attachment 969204
2. 1984
Hiki kitabu nilianza kusoma muda ila mwaka huu nikashawishika kukimaliza. Ni fiction lakini kipo serious sana. Kinazungumzia ubaya wa ujamaa, serikali ya mabavu, uminyaji wa uhuru nk.Wakati wa Nyerere kilipigwa Marufuku sijui kama wamekifungulia.
View attachment 969669
3.The Capitalist Nigger. Haka kakitabu kuna mdau alikaweka humu ndani. Ni katkitabu kafupi kama page 50. Kanazungumzia hali ya mtu mweusi hasa kiucgumi na kielimu. Kana idea nzuri ya jinsi mtu mweusi anaweza kukomboka. Ila kaba lugha kali.View attachment 969670
4.Kitabu changu.Niliandika na kuchapa kakitabu mwaka 2013. Huwa karibu kila mwaka nakasoma. Na kila nikikasoma napata kitu kipya!!!
5.The man who mistook his wife for a hat.
Hiki kitabu nilianza zamani kusoma lakini sijakimaliza. Ni kitabu kifupi na kinavutia sana.Kinazungumzia wagonjwa wa akili wenye matatizo adimu na ya kushangaza.
View attachment 969679
6.The politics book.
Haka kakitabu kanaelezea historia ya siasa toka zama za zamani kabisa. kanaeleza kwa njia rahisi na fupi. Ni kazuri ila sijakamaliza bado.
View attachment 969683
Malcom Lumumba , Kiranga Wick mitale na midimu Nalendwa zitto junior MSEZA MKULU et al