Umeshawahi kutenda wema na ukakutokea puani?

Umeshawahi kutenda wema na ukakutokea puani?

Ile nyumba tulikuwa tunapanga watatu akuna ata aliyetoa kikombe. Nilifungua kesi ila niliposikia kwamba ata akikutwa na kosa atafungwa ila mm sitolipwa mahakamani sikuludi tena. Kwahyo hakimu aliita ile kesi mara tatu mimi sikwenda ila kwa maneno niliyoongea mwanzoni wakati kesi inaanza nadhani hakimu alilizika nayo kwahyo alimfunga miaka minane.
Dah, aisee ni ningemkomalia hadi angefungwa maisha kama wale madogo waliochoma kituo cha polisi...angeniibia kisha akakimbia ningemuacha, ila unichomee vitu vyangu vyote ndani nikuache?

Ilikuwa ni mwaka gani mkuu? Hajatoka bado?
 
Hii mda jamaa wa Radio Upendo FM anaitwa John Pazia ameiweka leo ktk kipindi chake kinachorushwa kila siku saanane mchana. Nilimsikia nikasema hiiii...hahaaaaaa...

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Ukiona ivo ujue yy ni member wa humu ndan
 
Dah, aisee ni ningemkomalia hadi angefungwa maisha kama wale madogo waliochoma kituo cha polisi...angeniibia kisha akakimbia ningemuacha, ila unichomee vitu vyangu vyote ndani nikuache?

Ilikuwa ni mwaka gani mkuu? Hajatoka bado?
Nilikuwa nawaza kama wewe ila nikajiuliza ata akifungwa nafaidika na nn? Mm bado kijana mdogo vitu vinatafutwa nikimsamee kuna swawabu fulani unapata. Kwahyo kwa moyo wangu nilimusamee ila hakimu alikataa kumusamee ilikuwa 2015.
 
Pole sana mkuu mimi nilimkopa mtu laki nane alikua na matatizo haswa leo mwaka wa tatu hataki kunipa pesa yangu anachofanya ananitegeshea mbunye nipige ajilipe na mimi namkwepa hawa wanawake hovyo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwingine ni mdada wa humu ndani aliniomba nimsaidie jambo fulani,sababu yeye alishindwa basi nikajitahidi kwa moyo wangu kumsaidia na kumkopesha juu ili jambo lake lifanikiwe,kilichotokea sasa mpaka leo kaniblock kwenye whatsapp messenger na simu zangu hapokei nikitumia namba nyingine akijua ni mimi anakata.
 
Nakumbuka mwaka 2012 kuna mzazi aliwahi kunikabidhi binti yake wa kidato cha pili nihakikishe anafaulu,maana kichwa chake hakikuwa na uwezo sana,alisharudia mara moja kidato cha pili
Nami sikufanya hiyana nilimsaidia/kumuwezesha kufaulu kulingana na kichwa chake
Lakini binti alitamani anilipe fadhila bila wazazi wake kujua
Kilichotokea hadi leo binti ana mtoto wa miaka mitano,na mimi kazi ya ualimu niliacha,na naishi nchi jirani koloni la Mreno
Kwa hiyo hapo nani kamfanyia mwenzake fadhila?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilikuwa nafanya kazi mahali sasa kulikuwa na mwenzangu tunafanya nae kazi lakini ilitokea akawa anachukiwa sana na mke wa boss kutokana tu na sababu za wivu wa kike. sasa nilikuwa namuhurumia sana kutokana na jinsi alivyokuwa ananyanyaswa, ikatokea mimi nikapata kazi mahali pengine ambapo kwenye hiyo ofice nikapewa kuwa supervisor wa wafanyakazi wengine, yani akitoka boss ndio mimi, kwa huruma zangu nikamfanyia mpango yule mwenzangu aliyekuwa ananyanyasika kule akaja akapata kazi pale nilipokuwa, nikamfundisha kazi mpaka akaiva haswaa, aisee alianza kuyapika majungu ya hatari kuanzia kwa boss mpaka wafanyakazi wengine, nilichukiwa na kila mtu bila kosa, nikashangaa tu napewa likizo,na boss mpaka hapo nitakapoitwa, huwezi amini ndio ilikuwa mwisho wa kibarua changu na yeye akachukua nafasi yangu. sitasahau hili jambo mpaka nakufa
Duh aisee pole sana mzee
 
Nilikuwa nawaza kama wewe ila nikajiuliza ata akifungwa nafaidika na nn? Mm bado kijana mdogo vitu vinatafutwa nikimsamee kuna swawabu fulani unapata. Kwahyo kwa moyo wangu nilimusamee ila hakimu alikataa kumusamee ilikuwa 2015.
Dah, basi mkuu una huruma sana, mtu anatakiwa apewe stahiki yake bana, mambo ya kuwahurumia wahalifu yanaweza kukutia matatizoni tena huko mbele...unamsamehe mtu badala ya kumpeleka anakostahili unashangaa anakurudia tena, unasema tena ningejua
 
Pole sana ndugu. Kisa chako kinasikitisha sana.
Mie msaada nilitoa mwaka 1996 kimeniweka chini mpaka leo hii kwa maradhi na mikosi.Mdogo wangu kwa mama mdogo aliniomba aishi kwenye nyumba yangu kwa kuwa mie nilikuwa naenda kufanya kazi ktk mkoa mwingine nikamkubalia kwa kuwa anaanza maisha ngoja akae angalau mwaka hivi itakuta ameshajipanga ,halo kuumbe huyu bwanamdogo kaanza tu kutengeneza hati kwa kwa lengo la kunidhulumu nyumba na kwenda kwa waganga bariadi lengo nife abaki na nyumba. Baada ya mwaka kumalizika nikampia simu kumwomba atoke sasa ili niipangishe lakini naye akaniomba kwamba nimpangishie nimwachie tu mwezi huu tu ili mwezi ujao alipe kodi ya miezi 6. Mwezi ukaisha nikapiga simu simu haipatikani nikatuma dada yangu, akamwambia kesho namtumia pesa na kusema kwamba simu yake iko kwa fundi. Sikupata pesa hizo ikapita wiki dadayangu akaenda tena kwake, alimjibu kwa ujeuri na kumwambia asimfuate tena. Ghafla nikaanza kuugua mguu wa kulia ..ndugu wana jf tokea muda huo mpaka leo hii mie ni mgonjwa na nimeeleza kidogo tu nikiwa nimelala chali
 
Halo mawasaliano yalikwepo nikiwa nafanya kazi ATLAS LOGISTICS UN-argency kule benaco refugees camp tulikuwa na simu kama kawaida ingawa zilikuwa zinatumia un radio call frequency na huku dar mzee wa kinyakwusa pale Changombe polisi, muda mrefu tokea nasoma high school pugu, nimetumia radio call ya changombe polisi kwa msaada wa mzee wangu yule ingawa mitambo ilichoka sana. Ndo ilinisaidia kuongea na huyu dhulumati marehemu kwa msaada wa dada yangu aliyeenda kwa mzee Bruno
 
Nakumbuka mwaka 2012 kuna mzazi aliwahi kunikabidhi binti yake wa kidato cha pili nihakikishe anafaulu,maana kichwa chake hakikuwa na uwezo sana,alisharudia mara moja kidato cha pili
Nami sikufanya hiyana nilimsaidia/kumuwezesha kufaulu kulingana na kichwa chake
Lakini binti alitamani anilipe fadhila bila wazazi wake kujua
Kilichotokea hadi leo binti ana mtoto wa miaka mitano,na mimi kazi ya ualimu niliacha,na naishi nchi jirani koloni la Mreno
Dah...kwa hiyo uliamua kutorokea Mozambique mkuu? Hahahahahaha
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom