Umeshawahi kutenda wema na ukakutokea puani?

Umeshawahi kutenda wema na ukakutokea puani?

🤣🤣🤣daah m staki ata kukumbuka

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakuna kitu kinaweza kukuingiza kwenye matatizo makubwa kiutaniutani kama kutoa ama kupewa lifti. Mimi ni mzee wa kutembea kwa miguu sana na watu huwa wanajitolea kunipa lift na huwa nakataa. Ila kuna siku nilipewa lifti na mtoto mkali asee nisingeweza kukataa sema niliposhuka nikajiuliza je kama angekuwa mtekaji si ningeshakufa kwa tamaa ya wanawake.
Wenye magari msipende kutoatoa lifti.
Tusio na magari tusipendepende kuomba lifti.
 
nilikuwa nafanya kazi mahali sasa kulikuwa na mwenzangu tunafanya nae kazi lakini ilitokea akawa anachukiwa sana na mke wa boss kutokana tu na sababu za wivu wa kike. sasa nilikuwa namuhurumia sana kutokana na jinsi alivyokuwa ananyanyaswa, ikatokea mimi nikapata kazi mahali pengine ambapo kwenye hiyo ofice nikapewa kuwa supervisor wa wafanyakazi wengine, yani akitoka boss ndio mimi, kwa huruma zangu nikamfanyia mpango yule mwenzangu aliyekuwa ananyanyasika kule akaja akapata kazi pale nilipokuwa, nikamfundisha kazi mpaka akaiva haswaa, aisee alianza kuyapika majungu ya hatari kuanzia kwa boss mpaka wafanyakazi wengine, nilichukiwa na kila mtu bila kosa, nikashangaa tu napewa likizo,na boss mpaka hapo nitakapoitwa, huwezi amini ndio ilikuwa mwisho wa kibarua changu na yeye akachukua nafasi yangu. sitasahau hili jambo mpaka nakufa
 
Nakumbuka mwaka 2012 kuna mzazi aliwahi kunikabidhi binti yake wa kidato cha pili nihakikishe anafaulu,maana kichwa chake hakikuwa na uwezo sana,alisharudia mara moja kidato cha pili
Nami sikufanya hiyana nilimsaidia/kumuwezesha kufaulu kulingana na kichwa chake
Lakini binti alitamani anilipe fadhila bila wazazi wake kujua
Kilichotokea hadi leo binti ana mtoto wa miaka mitano,na mimi kazi ya ualimu niliacha,na naishi nchi jirani koloni la Mreno
hahahaha dah! ulikuwa mwalimu bora sana, sasa hivi unaipeperusha bendera yetu kimataifa
 
Pole sana mkuu mimi nilimkopa mtu laki nane alikua na matatizo haswa leo mwaka wa tatu hataki kunipa pesa yangu anachofanya ananitegeshea mbunye nipige ajilipe na mimi namkwepa hawa wanawake hovyo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani una maana kuwa ulimkopesha/ulimkopea kwani ingekuwa umemkopa basi ni wewe ulitakiwa umlipe. Anyway, visa vya kukopesha watu na wakakataa kurudisha ni vingi mno. Nadhani kila mtanzania laiyewahi kukopesha mtu fedha amekumbana na hili tatizo.
 
nilikuwa nafanya kazi mahali sasa kulikuwa na mwenzangu tunafanya nae kazi lakini ilitokea akawa anachukiwa sana na mke wa boss kutokana tu na sababu za wivu wa kike. sasa nilikuwa namuhurumia sana kutokana na jinsi alivyokuwa ananyanyaswa, ikatokea mimi nikapata kazi mahali pengine ambapo kwenye hiyo ofice nikapewa kuwa supervisor wa wafanyakazi wengine, yani akitoka boss ndio mimi, kwa huruma zangu nikamfanyia mpango yule mwenzangu aliyekuwa ananyanyasika kule akaja akapata kazi pale nilipokuwa, nikamfundisha kazi mpaka akaiva haswaa, aisee alianza kuyapika majungu ya hatari kuanzia kwa boss mpaka wafanyakazi wengine, nilichukiwa na kila mtu bila kosa, nikashangaa tu napewa likizo,na boss mpaka hapo nitakapoitwa, huwezi amini ndio ilikuwa mwisho wa kibarua changu na yeye akachukua nafasi yangu. sitasahau hili jambo mpaka nakufa
Ndiyo maana wahenga walisema "tenda wema nenda zako"!
 
Kuna Jamaa alichukua mkopo bank baadae mambo yakamwendea sivyo marejesho ya mwisho mwisho yakamshinda..bank wakataka kuuza nyumba yake mshikaji kaja kanieleza kwa uchungu mbya yaan Jamaa alivyokua anaeleza mpaka nikamurumia aisee

Akaniomba kiasi cha pesa kwa ahadi ya kunirudishia kabla ya siku 2 mm nikampatia maana ni rafiki Wa kitambo hapa mjini,.. Ikapita siku2,wiki,mwezi sasa ni miezi karibu 6 kila nikimuliza majibu ninayopewa ni bora angeniambia nimpe bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nshawahi kumkuta mwana mmoja mlevi katumbukia kweny korongo anakoroma tu,,watu wanampita tu,,kujinasua na kesi cha mauaji au ushahidi polisi nami kam wengne nkajikausha tu nkasepa zangu.
Hii kitu niliwai kuiona siku moja nazani jamaa alichukua mahali malaya sasa yule malaya akazingua basi jamaa alimpiga sana then akamtupa kwenye shimo la takataka asubui tunaamka tukamkuta huyo demu kwenye shimo tukajua kafa nabae akaanza kujigeuza geuza hakuna mtu aliyesubutu kupiga simu polisi wala kumgusa tulimuacha humo humo manake kwa sheria zetu zilivyo za kisenge ukijifanya kumsaidia kumpeleka hospitali akifia njiani wako huyo
 
Wewe unafikiriaje? Umesoma kichwa cha thread hii vizuri? Kisa cha kweli hicho. Mimi nilipata kufanya kazi katika nchi hiyo. Wakati wa orientation (kama unaelewa maana yake - kwa sababu unaonekana hauna exposure), tuliambiwa kuwa hakuna kutoa lift kwa wenyeji hata siku moja.
Ni kwa mujibu wa sheria za nchi au ndio mambo ya hongo au akikaza kwamba hajakubaliana malipo hayo inakuaje
 
Maisha ya sasa hivi na walimwengu wa kizazi hiki wengi tusio na shukrani, ukitaka tenda wema au kaa pembeni. Ila nakushauri usifanye kitu chochote kibaya ukaonekana ww ndio mgomvi. Nilikutana na mtu mmoja miaka kadhaa nilipoanza kazi 2005 tukawa marafiki, alikua kiongozi kanisani ,alikua na elimu ya kawaida akiwa kibarua kampuni yetu. Nilimsaidia sana nilivyoweza,ikafika mahala matatizo yake nikayafanya yangu. Alipooa nilijitoa vya kutosha, mama yake akiumwa namsaidia, alipooa alikaa kama miaka 2 hana kazi, nkamsaidia kumlipia kodi, chakula ananitegemea, mpaka mke wake alipojifungua ilikuwa kama mke wangu ndio amejifungua maana kila kitu alinitegemea mm. Ila huwezi amini alikuja kunifukuzisha ile kazi tuliokuwa tukitegemea sote, mahusiano yangu akawa hayadumu kumbe akijua alikua ananizunguka, alinifanyia vitu ambavyo nina uhakika hata shetani mpaka leo anamcheka na kumdharau. Leo akiniona anajificha hayuko tayari kukutana na mm uso kwa uso. So ukiweza tenda wema na kubali lolote litakalokutokea. Kingine nashauri usije ukawa chanzo cha kutenda mabaya. Binadamu hatuna shukrani
 
Nimekuelewa sana mkuu. Kudos
 
Mie msaada nilitoa mwaka 1996 kimeniweka chini mpaka leo hii kwa maradhi na mikosi.Mdogo wangu kwa mama mdogo aliniomba aishi kwenye nyumba yangu kwa kuwa mie nilikuwa naenda kufanya kazi ktk mkoa mwingine nikamkubalia kwa kuwa anaanza maisha ngoja akae angalau mwaka hivi itakuta ameshajipanga ,halo kuumbe huyu bwanamdogo kaanza tu kutengeneza hati kwa kwa lengo la kunidhulumu nyumba na kwenda kwa waganga bariadi lengo nife abaki na nyumba. Baada ya mwaka kumalizika nikampia simu kumwomba atoke sasa ili niipangishe lakini naye akaniomba kwamba nimpangishie nimwachie tu mwezi huu tu ili mwezi ujao alipe kodi ya miezi 6. Mwezi ukaisha nikapiga simu simu haipatikani nikatuma dada yangu, akamwambia kesho namtumia pesa na kusema kwamba simu yake iko kwa fundi. Sikupata pesa hizo ikapita wiki dadayangu akaenda tena kwake, alimjibu kwa ujeuri na kumwambia asimfuate tena. Ghafla nikaanza kuugua mguu wa kulia ..ndugu wana jf tokea muda huo mpaka leo hii mie ni mgonjwa na nimeeleza kidogo tu nikiwa nimelala chali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom