Umeshawahi kutenda wema na ukakutokea puani?

Umeshawahi kutenda wema na ukakutokea puani?

upi uo mkuu
Nilifahamiana na dada kupitia group la watsap alikuwa Mtu wa Singida tukawa marafiki siku moja akanieleza dada nimepata kazi dar ila sina sehemu ya kufikia naomba nifikie kwako, baada ya kumuuliza maswali roho ya huruma ikanijia nikamwambia aje,Alisafiri nikaenda kumpokea Ubungo ila tulipo kuwa kwenye gari mda wote alikuwa bizze na simu nilikuwa na wasiwasi nikajipa moyo ngoja alale usiku mmoja asubuhi nitajua nini cha kufanya,Story ndefu nimechoka kuandika kifupi yule dada aliiba simu na pesa kidogo.
 
Pole; Aliamua kutufungia milango ya ridhiki ya kuja kwako.
 
Mwingine ni mdada wa humu ndani aliniomba nimsaidie jambo fulani,sababu yeye alishindwa basi nikajitahidi kwa moyo wangu kumsaidia na kumkopesha juu ili jambo lake lifanikiwe,kilichotokea sasa mpaka leo kaniblock kwenye whatsapp messenger na simu zangu hapokei nikitumia namba nyingine akijua ni mimi anakata.
Mbona hiyo story hujanipaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie msaada nilitoa mwaka 1996 kimeniweka chini mpaka leo hii kwa maradhi na mikosi.Mdogo wangu kwa mama mdogo aliniomba aishi kwenye nyumba yangu kwa kuwa mie nilikuwa naenda kufanya kazi ktk mkoa mwingine nikamkubalia kwa kuwa anaanza maisha ngoja akae angalau mwaka hivi itakuta ameshajipanga ,halo kuumbe huyu bwanamdogo kaanza tu kutengeneza hati kwa kwa lengo la kunidhulumu nyumba na kwenda kwa waganga bariadi lengo nife abaki na nyumba. Baada ya mwaka kumalizika nikampia simu kumwomba atoke sasa ili niipangishe lakini naye akaniomba kwamba nimpangishie nimwachie tu mwezi huu tu ili mwezi ujao alipe kodi ya miezi 6. Mwezi ukaisha nikapiga simu simu haipatikani nikatuma dada yangu, akamwambia kesho namtumia pesa na kusema kwamba simu yake iko kwa fundi. Sikupata pesa hizo ikapita wiki dadayangu akaenda tena kwake, alimjibu kwa ujeuri na kumwambia asimfuate tena. Ghafla nikaanza kuugua mguu wa kulia ..ndugu wana jf tokea muda huo mpaka leo hii mie ni mgonjwa na nimeeleza kidogo tu nikiwa nimelala chali
Mkuu pole sana.
Inatia huruma sana.
Wakati mwingine kuwa mwema kunatuponza sana basi tu.
Ubinaadamu kazi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan mkuu we acha tu unamdai mtu af anakujibu "subiri siku nikipata nitakupa" hapo ni baada ya kumpigia simu kwa mda mrefu bila kupokelewa anaamua kukujibu kwa msg

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi kuna anayenijibu
"Najua nadaiwa pesa yako nitakupa"
Ila huu ni mwezi wa sita unaenda ukimpigia hapokei na siku akipokea hayo ndio majibu.
Inauma sana basi tu.
Unamsaidia mtu kwa roho moja ila baadae anaona sawa kabisa kukudhulumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom