Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Mkuu nyoka huyu kifutu(Puff adder) anasumu inayoozesha misuli(Myotoxin). Akikuuma usipofanya hima kutafuta matibabu, kama ameuma mguu basi mguu huo utaishia kukatwa kwa sababu utaoza na hakuna jinsi ya kurudisha misuli(nyama ) zilizooza ila kuziondoa kwa kukata. Sumu yake haiendi haraka kama sumu ya wale wengine wenye sumu inayoathiri mishipa ya fahamu (Neurotoxins) nerves au damu.
 
Nyoka akikung'ata unapaswa ufanye nini ili kupona?
 
Unahurumia snake!? Yeye hawezi kukuhurumia jombaa... Na tumeagizwa tuwaponde vichwa, hivyo hao jamaa walitimiza maandiko....

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Mkuu Fernando; Nyoka hakushambulii kwa lengo la kukushambulia tuu. La hasha. Mara zote nyoka anajihami mathalani umemkanyaga, umemfikia karibu mno na hana pa kukimbilia au kujificha au umeng'ngana kumuua. Sumu yake ni kwa ajili ya kujipatia chakula au tuseme kukamata mawindo yake. Tena ukumbuke anapokung'ata hakupi "Full Dose" kwani anaihitaji sumu hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa. Tena nyoka kifutu (na wengineo) wanafaida ya kula panya kama afanyavyo paka tunayemfuga. Kumbuka Tanzania(By then Tanganyika) tuliwahi ku-import vifutu from Malawi kwa ajili ya kudhibiti panya waharibifu kwenye ule mradi mkubwa wa Karanga Kongwa.
 
Nikweli kabisa au unamshika mzima unamweka ili akung'ate kibamia akishakung'ata tu kibamia kinaanza kukua ndani ya masaa matatu tu
Hivi kweli binadamu au tuseme MTU hasa ww Mgiriki unathubutu kumwelekeza mwenzio hivy? Akifa utafaidika nn? Tupendane, tusaidiane, tushauriane.Acha kuwaelekeza wenzio kwenye kifo.
 
Nyoka akikung'ata unapaswa ufanye nini ili kupona?
Mkuu nyoka wa aina gan na amekung' ata mazingira gan?
Kila nyoka ana njia za kufanya ili kujiponya lkn common ni kukimbilia hospitali


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa sie watu waporini huu ndo msimu wao kwetu kiangazi na joto huwa wanakuwa ni comon.. ni wazur na wanaminofu mizuri kama samaki sato
 
We kuna nyoka nao ni aina ya vifutu yaani viper wanaitwa rattle snake wao wanaspika kwenye mkia yaani wakiona hatari wanawasha spika ukisikia inabidi ukimbie ni hatari hao. Ndio lipumba anataka akaimport amweke nyumbani kwa lipumba
 
Nyoka hata kama ni Swila ama Koboko huwa ni wapole kinachotokea tu wakati mwingine ni kujihami...nyoka wengi hata wale wakali akimuona binadamu hutoka nduki ila kama kwa bahati mbaya ukaingia kwenye anga zake ndipo pale atakapokomaa na wewe kwa kusimamia mkia na ukijifanya mtaalamu wa kumpiga au kukimbia anakumaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…