Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 2,008
- 3,805
Kuna huyu samaki hatari anayepatikana Afrika. Kwa kiswahili anaitwa Mbenga. Kwa kiingereza Tiger Fish hasa anapatikana kwenye Mto Congo na matawi yake. Hadi ziwa Tanganyika anapatikana sababu ni sehemu ya system ya mto Congo.
Ni samaki lakini ana meno kama ya mamba au wanyama wengine wakali. Pia ana magamba magumu ya kuweza hata kuhimili kuumwa na mamba.
Inadaiwa hakuna zindiko kali kama la samaki huyu. Watu humtumia kufanya mazindiko mawili. Moja la kujilinda, hili hutumia magamba yake magumu. Na lingine la kushambulia, hili hutumia meno yake.
Meno au magamba ya samaki huyu huchomwa kwenye moto. Kisha husagwa na mtu hunywa majivu yake yakiwa yamechanganywa na dawa za mitishamba pamoja na damu.
Wakongo wengi hutumia kinga hii. Inadaiwa mtu aliyetumia meno ya samaki huyu akianza kukushambulia ni ngumu sana kumzuia. Labda uwe ulitumia kinga ya kujilinda ya magamba mengi sana, au ya samaki mkubwa kuliko yule aliyetumia adui anayekushambulia.
Pia magamba hayo huwekwa juu ya milango ya kuingilia ndani. Wachawi na nyoka huwa hawagusi nyumba hizo. Watu wengine huwa wanavaa hirizi zenye vipande vya meno na magamba ya samaki huyu.
Wakazi wengi wanaozunguka ziwa Tanganyika wanafahamu zindiko hili. Mtu huko akimpata Mzenga anakuwa kama amepata dhahabu. Meno na magamba yake yanasoko zuri sana .