Umeshawahi kumsikia nyoka aitwaye Kifutu?

Anawameza watoto ili awazae baadaye??!! Anawameza wanakwenda tumboni, wanaingiaje kwenye njia ya uzazi ili wazaliwe? Biology yako ina walakini!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyoka wapo watagao (oviparous) ambao ndiyo wengi na aina chache ya wazaao ( viviparous). Wameumbwa wamekamilika hivyo, anatomy haipo ya nyoka kutaga, kisha kumeza mayai halafu kuzaa watoto baadaye!!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa twashukuru lkn yule anaeitwa kiboko au black mamba aisee ni nyoko yule kwasababu kabla hajaanza timbwili anakuonya kwanza
Story hii niliikuta humu Na ilinisaidia baada ya kukutana nae yule nyoka hafai nilimpiga akajifanya kafa nilimsogelea na kijiti lkn nkaona ngoja nimshtue na jiwe kwanza aisee alinyanyuka na kuligonga jiwe Mara tano

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungeweka link yahiyo story nasi tujifunze mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu nyoka mpole sana wanapatikana sana maeneo ya baridi , siku moja nikiwa mafinga jkt nilitoroka mkesha nikaenda kulala porini nilikuwa na blanket nikiwa nmelala kumbe likaja likifutu na kuingia kwenye blanket asubuhi nashtuka linanitekenya...
Wala halikunidhuru
Ulikuwa nanga na doja wa platoon
 
Kwa wale walio soma UMOJA sekondari miaka ya 2000-2002, kwenye bweni linaloitwa PEACE chumba namba kumi,wakati huo tukikaa form six pekee, tulipata kuua KIFUTU mkubwa mwenye sifa zote hizo,na ilibidi tumwache awe kama wa maonesho.Meno yake marefu ya juu yalifanya kila aliyemwona asisimuke.Na ndilo bweni ambalo tulipata kumuua COBRA mrefu na mweusi mpaka anang'aa,pia nyoka wengine wengi,lakini kifutu alitia fora.
 
Niliwahi kukutana na vifutu wakijaribu kupandana kule Kigwa, Tabora. Nafikiri Kigwa ndiyo makao makuu ya nyoka hapa Bongo, yaani kuna nyoka wa hajabu sijawahi kuona hapa Bongo. Kifutu si rahisi kuuma mtu, na ile siku nilikutana nao pale Kigwa nilijaribu kuwapisha ila wenzangu sasa walikuja kuwaua bila hata sababu. Nilisikitika sana.
Kigwa ipi mkuu maana A na B
 
Very interesting story,I wish wangemleta pale kwenye maonyesho ya sabasaba ningemwona manaake paliwekwa nyoka wa aina nyingi hata black mamba alikuwepo lakini kifutu hakuwepo. pia inasemekana kifutu wanapatikana kwa wingi kwenye mashamba ya miwa .
Hapana, Black Mamba huwezi kumuona kwenye Maonesho ya Saba Saba...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfahamu Nyoka Mpole Na Hatari Zaidi Duniani

Leo tuingie tena darasani kidogo kusoma mambo yetu ya wanyamapori angalau kwa uchache. Kwa siku ya leo ningependa tuhame upande kidogo kutoka kwa mamalia twende kwa reptilia yaani (wanyama wanaotembea kwa kutambaa-(TAMBAAJI). Na moja kwa moja tuna muangalia NYOKA. Lakini kumbuka kuna aina nyingi sana za nyoka duniani, mbali nakuwepo kwa aina nyingi hizo lakini nyoka wenye sumu hatari ni wachache sana na hawafiki hata asilimia 30%. Leo kwa ufupi tumfahamu nyoka aitwae “KIFUTU” Kuna aina nyingi sana za nyoka hawa jamii ya kifutu duniani na hasa hapa kwetu Tanzania pia. Sasa nadhani itakuwa vizuri tukichagua jamii moja ya kifutu nakumueleze ambae ni “KIFUTU MSITU”

KIFUTU MSITU
ndio kifutu mkubwa kuliko jamii nyingine za kifutu wapatikanao barani Afrika. Sio tu nio mkubwa kwa jamii za vifutu wapatikanao barani Afrika bali pia ndio anaongoza kwa uzito kuliko vifutu wote duniani. Nyoka huyu barani Afrika anapatikana nchi mbalimbali kama Guinea, Ghana, Togo, Nigeria, Cameroon, Equatorial Guinea, Gabon, DR Congo, northern Angola, Jamuhuri ya Arika ya Kati, South Sudan, Uganda, Kenya, kusini mashariki mwa Tanzania, Zambia, Malawi, mashariki mwa Zimbabwe, na Msumbiji .

SIFA ZA KIFUTU MSITU

1. Jike uwa ni mkubwa na mzito kuliko dume
2. Huweza kukua na kufikia urefu wa futi 6-7
3. Uzito wa kifutu msitu wakati mwingine hufikia mpaka kiligramu 20.
4. Ana meno marefu na hata kufikia nchi 2
5. Ana kichwa chenye umbo la pembe tatu,shongo nyembamba, mwili mkubwa na mnene.
6. Magamba ya chini uwa yana rangi ya uzurungi au zambarau.
7. Pia anakuwa na magamba yenye rangi ya njano na zambarau ubavuni yaliotengeneza maumbo ya pembe tatu.
8. Macho yake yana rangi ya kijivu na mboni ya jicho huponekana kuwa na rangi ya fedha.
9. Jamii yao ambao wanapatikana Afrika ya magharibi wana pea moja ya pembe ambazo zipo katikati ya matundu ya pua.
10. Mwili wa kifutu huwa na rangi ilio pauka.

TABIA ZA KIFUTU MSITU

1. Kifutu msitu hufanya mawindo yake usiku kwasababu ana uwezo wakuona usiku zaid kuliko mchana.
2. Ni miongoni mwa nyoka wavivu sana hasa kwenye kutembea.
3. Rangi yake iliyo pauka humfanya asionekane kirahisi na hii hasa humsaidia katika kuwinda na kuwaepuka maadui zake.
4. Ni nyoka ambae huwa haumi mpaka atakapo kuwa kajeruhiwa au kukanyagwa na wakati mwingine unaweza mkanyaga asikuume pia.
5. Kifutu msitu ni nyoka ambae huwinda kwa kushitukiza na si kufukuzana na kiumbe amuwindae.
6. Ndio vifutu wavumilivu kuliko vifutu wengine wote hasa kwa upande wa kuuma. Nimara chache sana nyoka huyu kumuuma binadamu.
7. Hutoa sauti pale anapo kasirika na kufafanya kichwa chake kuwa bapa zaidi.
8. Ana macho ambayo yanaweza kuona sehemu mbili tofauti. Jicho moja likiwa linatazama mbele linguine lina uwezo wakutazama nyuma.

MAZINGIRA

Kifutu msitu ni nyoka wapeneleao maeneo yenye misitu ya mvua na maeneo yenye miti mingi na unyevu nyevu. Hapa nchini Tanzania nyoka hawa hupatikaa maeneo yenye kilimo zaidi hata mazao ya biashara.

UWINDAJI NA CHAKULA
Kama tulivyoona hapo juu nyoka hawa hawana uwezo wakukimbizana na wanyama wanaowawinda na hii ni kutikona na uzito pamoja na maumbile ya miili yao. Anapo muona mnyama humrukia ghafla na kumuuma kasha huendelea kumshikilia na meno yake marefu huku akiendelea kuingiza sumu mwilini mwa mnyama huyo na hatimae mpaka ahakikishe kafa ndo humuachia na kummeza. Kwa barani Afrika ndio nyoka mwenye uwezo wakutoa kiwango kikubwa cha sumu kwa wakati mmoja.

Kifutu msitu huwinda wanyama wadogo wadogo kama panya na wakati mwingine sungura. Pia huwinda mijusi na vyura hali kadhalika ndege waishio aridhini.

KUZALIANA
Nyoka hawa maranyingi hujamiiana msimu wa mvua na hasa kuanzia mwezi wa 9-12. Ikumbukwe kuwa nyoka hawa hawatagi mayai nje kama walivyo baadhi ya nyoka wengine. Mayai hurutubishwa na kuendelea kukua na kutunga watoto yakiwa ndani ya mwili wa kifutu msitu jike.

Mara tu baada yakujamiiana na mayai kurutubishwa kifutu msitu jike huchukua muda wa miezi saba (7) mpaka kuzaa watoto. Mayai hupasukia tumboni kasha kuzaa watoto 8-43 na mara nyingi ni takribani watoto 24 tu ndo hukua mpaka kufikia hatua ya kuzaa. Watoto huzaliwa wakiwa na urefu wa wastani wa Sm25sm- Sm32 na uzito wa wastani wa gramu 25-45.

Mara tu baada ya kuzaliwa watoto hujitegemea kwa kila kitu ndio mana wengi hufa hasa kwakuliwa na mijusi pamoja na viumbe wengine msituni. Kifutu msitu huzaa kila baada ya miaka 2 au 3 wakati mwingine hufika mpaka miaka 5 .Umri wa kifutu msitu ni mpaka huweza kufikia mpaka miaka 18.

SUMU NA ATHARI YAKE
Nimara chache sana kusikia mtu kaumwa na kifutu msitu na hii ni kutokana na nyoka hawa kutokuwa na hasira sana. Lakini tahadhari sana nyoka hawa wana sumu mbaya sana japo haijafikia ya kobra au koboko. Mara nyingi huuma pale anapo kanyagwa au anapohisi anataka kujeruhiwa.

Sumu ya kifutu msitu huathiri tishu na mpaka hupelekea tishu kuoza na wakati mwingine kama ni mguuni mtu huweza kukatwa mguu kama alicheleshwa kupelekwa hospitali. Tofauti na vifutu wengine,kifutu msitu yeye uwa hatowi sumu tu mara anapo uma.hukusanya sumu kwa wingi baada yakuuma kutokana na kuwa na matezi yanayo zalisha sumu nyingi kisha huanza kuingiza sumu ile mwilini mwa mnyama aliye muuma

Athari nyingine mbali nakuoza sili na tishu, mara baada ya mtu kuumwa na kifutu msitu hupelekea kizunguzungu, kutembea bila uelekeo, kutokwa na haja kubwa, kutokwa na haja ndogo, ulimi na macho kuwa vizito, kutoka damu mfululizo na wakati mwingine maeneo ya ndani.

ANGALIZO

Mara mtu aumwapo na kifutu msitu au nyoka yeyote yule basi awahi haraka hospitali ili apatiwe matibabu kutokana na aina ya nyoka aliye muuma. Matumizi ya mawe ya asili wakati mwingine husababisha vifo visivyo na ulazima wakutokea.

UHIFADHI NA CHANGAMOTO

Ikumbukwe kuwa kila kiumbe kina faida yake katika mazingira ambapo kinaishi bila kujali kina athari jinsi gani kwa binadamu.
Kifutu msitu wanapokuwa wadogo huuliwa sana na mijusi,ndege,samaki pale wanaingia kwenye maji. Lakini kama walivo nyoka wengine, adui mkubwa wa kifutu msitu ni binadamu hasa kutokana na ongezeko la watu maeneo ya misitu kutokana nakutafuta makazi yakuishi.

Binadamu huwauwa nyoka hawa hasa kwa uoga na pia wengine huwauwa kwa ajili ya nyama. Maana kuna makabila mengine hapa duniani hupenda sana nyama ya nyoka.

Jambo jema nikwamba nyoka hawa bado hawajawa tishio la kutoweka duniani kama walivyo baadhi ya nyoka wengine au wanyama wengine.

HITIMISHO

Sio kila nyoka ana sumu yakusababisha kifo kwa binadamu na mara nyingi nyoka wenye sumu mbaya huwa hawakai karibu kabisa na makazi ya binadamu. Tusiwe na tabia yakuwauwa nyoka hovyohovyo mana tuna haribu maumbile asili na rasilimali tulizonazo. Nyoka hawezi kukuuma kama hujaanza kumchokoza au kumjeruhi. Nadharia zinasema kwamba nyoka ni miongoni mwa viumbe wanaopenda sana stori hasa pale wanapo sikia binadamu wanaongea hupenda kusogea maeneo yake nakuskiliza sauti japo hawaelewi nini kinaongelewa. Tuwapende viumbe hawa jamani.

Ahsanteni sana.

Kwa mawazo na ushauri kuhusu wanyamapori tuwasiliane kupitia bujibuji@jamiiforums.com

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom