Umeniandika

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
234
Mimi sina hili wala lile , mtu mmoja akanifuata nikasalimiana nae kisha akaniambia nimemwandika , nilipojaribu kumdadisi kujua haswa yeye ni nani , akaniambia kampuni yake niliyoandika katika habari husika akanitajia mpaka sehemu ambapo kitu hicho kilijadiliwa .

Nikamtuliza tukaanza kuongea mambo mengine nilimwambia awe huru kufanya mambo yake lakini aangalie kile nilichoandika kama kina mantiki au la au aache tu kama ilivyo kwa sababu imeshaandikwa na watu wameshajadili .

Jioni ya siku hiyo nikapata simu toka kwa mtu mmoja tukawa tunaongea biashara zingine tu ,katika maongezi yetu tukapanga tuonane siku ya jumatatu ,nilimwamini huyu jamaa kwa sababu alisema simu yangu amepewa na mtu mmoja ambaye ni rafiki yangu akataja mpaka jina .

Siku hiyo naenda kuonana nae ndipo niliposhangaa nimezungukwa na jama wengine na hapo nilibebwa katika gari , mpaka katika kituo cha polisi nikawekwa katika chumba cha peke yangu , huku nimenyanganywa simu , na vitu vyangu vingine vya kazi .

Sikupewa sababu za mimi kuwa pale mpaka kesho yake asubuhi ndio akaja mtu mwingine kwa ajili ya kufanya mahojiano na mimi , kwanza akaanza kuniambia ‘nasikia wewe ni mtaalamu sana wa komputa unaandika sana watu wewe unachafua watu sana katika mitandao tulikuwa tunakutafuta sana .

Baadaye kidogo yakaletwa mafaili ya kesi zaidi ya 20 mmoja wa wale polisi akaniambia nisiposema jina kamili la katika ile tovuti ninayochangia mambo yangu zile kesi zote zitakuwa zangu , agizo lingine nililopewa ni kumpigia simu huyo mwenye tovuti kwa sababu wameambiwa mimi najuana nae .

Tulisumbuana sana sikusema chochote kile , lakini akanirudishia simu na yeye akatoka kidogo hapo ndio niliandika sms fupi kutuma kwa jamaa zangu wengine ambao huwa tunashirikiana kwa hili na lile .

Yule askari alivyotoka nje kumbe alienda kuleta laptop fulani nakumbuka hata majina yaliyosajiliwa nayo wakaniambia mtu yoyote akiniuliza nini kinaendelea niseme ni masuala binafsi nimekuja kuongea nao kumbuka nilikuwa ndani polisi na sikuweza kubisha au kukataa baadhi ya vitu kwa sababu niko katika himaya yao >

mpaka muda huo ulikuwa ni saa tatu asubuhi imeshafika na sijaonyeshwa karatasi zozote za mashitaka na hata sijaambiwa vitu vyangu walivyochukuwa wamepeleka au kumpa nani na sikuruhusiwa kuonana na jamaa zangu wengine walisema mtu yeyote akija watanipoteza .

Zile laptop ziliwashwa na zilionyesha zilikamatwa kutoka kwa watu mbali mbali ambao ni waandishi au wanaojihusisha na kuandika au vitu kama hivyo , kwa sababu ukiangalia usajili wake zimebeba usijili wa hizi kampuni za habari majina siwezi kutoja kutokana na usalama au zinaweza kuwa zimeshafutwa saa hizi >

wakaleta hata ile laptop niliyokuwa nayo mimi akaja na mtaalamu mmoja wa ict huyu mtaalamu ni mwanachama wa ethinktanktz.org huyu mtu akajitambulisha kama askari pia akaanza kunihoji maswali haya na yale .

wakanihangaisha sana mwisho wa siku wakaniambia niwape laki nne ili hii ishu isiwe kubwa yaani wasinibambikize zile kesi zingine walizonionyesha pia wasimwambie mkubwa wao kwamba wamefanikiwa kukutana na mimi >

walipotoa madai hayo nami nikawaambia wanibambike hizo kesi zilizokuwa katika makaratasi na wamwambie huyo kigogo anayenitafuta tunaweza kwenda kuongea katika mahakama kwa muda ule sikuwa na chochote cha kusema .

Niliwaambia kwanini wameniweka ndani zaidi ya masaa 24 bila kuniambia sababu za mimi kuwa pale wananizungusha tu hata ndugu na jamaa zangu hawana taarifa zozote inakuwaje au kwa sababu wameniona mimi mnyonge ndio maana waamue kufanya lolote ?

kabla sijakaa sawa mmoja wa rafiki zangu alifika pale huyu ni mwanajeshi ndio maana wakaogopa na nikaruhusiwa kuongea nae nikamwambia ukweli ikabidi nichukuliwe kinguvu toka mikononi mwa polisi na kuondoka zangu ?
Watu hawa hawakuchoka baada ya miezi nne hivi nikapigiwa tena simu na mtu akaniambia yuko offisi fulani nimpelekee mali fulani mimi nikanunua dukani kwenda kumpelekea

aliniambia nikifika chini gorofani nimwambie atakuja kunichukuwa anionyeshe alipo nilifika pale nikampa taarifa mara watu wengi wakaja kunivamia nikatekwa nyara >

Hiyo ilikuwa ni jumamosi ya siku hiyo , vitu nilivyokuwa navyo wakachukuwa na tena nilikuwa nimebeba laptop ninayotumia kuhifadhi vitu vyangu ninavyofanya ninapokuwa sehemu fulani fulani >

Lakini mara hii sikupelekwa polisi wakati huu nilipelekwa nyumbani kwa mtu ambaye inasemekana ni jaji wa mahakama za umoja wa mataifa aliyenishika mkono yeye alijitambulisha ni usalama wa taifa .

Kule ndani nilikaa kwa siku 2 mpaka jumatatu asubuhi kwa kuwa nilikuwa mzima nilienda nyumbani kidogo kisha nikaenda zangu kazini bila mtu wowote kujua nini kilichokuwa kinaendelea ila wale ninaofanya nao kazi za kuandika walishituka wakajitoa hewani ili kuepusha shari zaidi .

Kwahiyo mpaka sasa hivi naamini kuna wengi wamekumbwa na kash kash hizi za watu ambao wanajifanya au wanatumiwa na hawa jamaa ambao tunawaandika au kuwasema kwa njia ya mtandao kutukamata na kujaribu kutunyamazisha .

Lakini wanajiuliza waanze na nini au waje na njia gani ili mashitaka yao yawe ya kweli na yakubalike na yawe halali kabisa ?

Mfano mimi ninatafanya kazi katika sekta haswa ya ufundi ya vitu vinavyohusiana na ict sasa wengi wanatumia ujanja wa kujifanya wanahitaji huduma zangu na unapoenda huko unajikuta unakumbana nao na wanatumia mwanya huo kukutia kashkash .

Uzuri wangu mimi ninachoandika hata kama nimetumia majina bandia ni vya ukweli nina uwezo wa kwenda kujitetea hapo sheria inapoamua kuchukuwa mkondo wake lakini kwa njia za kutekana kama hizi sintoweza kuongea au kugusia chochote kile >

wengi wanatumia vyeo vyao katika serikali na sehemu zingine kututisha sasa wawe makini na macho sana kwa maana wengine hatutaki kuamua kuwataarifu wenzetu ambao wako huko huko serikali kuhusu michezo yao michafu

Tukisema nasi tuwatumie hao ndugu na jamaa zetu ambao wako huko huko serikalini si itakuwa mvurugano jamani ? Sasa kama wewe unataka usiandikwe haitawezekana kama unafanya mambo ambayo yanavitia habari .

Ukifanya jambo jema basi jumuia ya habari haina budi kutangaza jambo hilo na kukusifia lakini kama umeamua kufanya ubaya kwa kuuwa uchumi wetu bila na destrui zetu jumuiya hiyo hiyo ya habari itaongoza mapambano dhidi yako

Kisha utaamua kuachia ngazi mwenyewe au uendelee kukaa ulipo jumuiya ikuvue nguo zote mpaka vizazi vyako ?

Moto ni ule ule tena sasa unaongezeka kwa kuwa tumeshajua haswa watu tunaopambana nao ni wakina nani mpaka vijukuu vyao tumeshavijua >

sisi tutatumia mitandao tu na njia zingine za usalama ambazo ni ngumu kwa mawazo yako kufutwa au kwa mawazo yako kuharibiwa kama blogu < forum > podcast na njia zingine nyingi sana >
 
walikuwambia usiwataje majina?We dare talk openly.au ni storry ya kutunga.kama ni kweli waanike Hadharani.hakuna mambo ya EthinkTankTZ wala nini,wanataka tuwalinde mafisadi?
 
Ndiyo Kwanza Mapambano Yaanaanza. Wale Wote Ambao Wanafanya Uchafu Huu Ndiyo Ubao Wa Kuwaaanika Wazi Wazi,kama Hawataki Kuanikwa, Wafanye Mema Na Warudishe Fedha Za Wananchi. Shy,tupe Majina Ya Unaowahisi Live Hapa Ubaoni Tupambane Nao,hatuna Uwezo Wa Fedha Ila Tunaweza Kupambana Nao Hapa. Long Live Shy And Jf
 
OK OK OK, Here we go..

Sikumoja nikiwa home nilipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwanausalama akitaka nimpe ushirikiano kwa kazi yao kama raia mwema.

Nikakubali kuonana naye, alipofika nikamuuliza jina na kazi anayofanya hakuniambia wakaja wenzake, nikawekwa ndani ya gari tukaelekea kwenye kituo. Tulipofika wakanihoji kma namtambua mwananchama yeyote wa JF nikakataa. Nikawekwa ndani mpaka jumapili (nilikamatwa ijumaa) hapo simu yangu waliizima.

Siku ya jpili wakanichukua tukatoka nikapelekwa kwenye jumba moja kubwa mikocheni, huko ilikuwa ni jumba la mkuu wa majeshi fulani lakini yeye alisema ni polisi nikahojiwa sana na kuonyeshwa JF na kuulizwa kama ni mwananchama na nawafahamu baadhi yetu humu.

Nikakataa. Mwishoni nikatishiwa sana na kuambiwa niwaambie wenzangu tusipoacha kuandika humu tutakamatwa na kusekwa lupango, na wakaniambia pia wana monitor simu yangu na IP addresses zinazoingia humu jambo forum.

Nikarudi nyumbani, kwakuwa hawakunidhuru sikuchukua hatua yoyote. bado wananipigia simu kunitisha!

End of story. No NAMES. NO POLICE POST NAME, U have logged on with anonymous name.. no dates, no how I realised it was mkuu wa majeshi and not police. NOTHING.

Absolutely nothing!

Gud day guyz.
 
Ok Du yu wanti nems?

here we go.. Yule sajenti alikuwa anaitwa Mchafukoge Msabalahi alikuwa na jamaa mmoja wa usalama wa Taifa jina limenitoka.

Yule jaji ni yule wa mahakama ya UMOJA WA MATAIFA, KWANI HAUMUJUI?

Lile jumba nimesahahu, yule wa ethinktank anaitwa Abdallah Omary

Jamani siwezi hata kuwashtaki, naogopa maisha yangu..

Give me a break! your dad has money somehow, surely he can fight 4 his son if it is indeed true that..
 
walikuwambia usiwataje majina? We dare talk openly.au ni storry ya kutunga.kama ni kweli waanike Hadharani.hakuna mambo ya EthinkTankTZ wala nini,wanataka tuwalinde mafisadi?

Pole. Lakini ni kweli inaonekana kama story ya kutunga. Taja angalau kituo cha polisi ulikoswekwa Lupango. Wanakuteka nyara siku mbili, wanakuchia na huchukui hatua zozote?
 
Pole sana ndugu SHY.....!Kati ya vitu ambavyo mtu anatakiwa kuwa navyo ni ujasiri! Lakini kama wasemavyo Wahenga ........KIDOLE KIMOJA........! NA MTU ANAPOKUWA THREATENED SANA HALI YA WOGA INAINGIA,(naomba nitoe mfano ila usitafsiriwe nisivyomaanisha).."YOU CAN CHASE A DOG WHEN ITS ALONE AND MOVING ALONG THE STREETS.....BUT THE SAME DOG BECOMES FURIOUS&DANGEROUS WHEN YOU REACH ITS HOMESTEAD"HAPA TUNAONA NI NAMNA GANI MTU ANAPOKUWA NYUMBANI(anapowaeleza wanaJF wenzake)ANAVYOKUWA MORE ACTIVE SIMPLY KNOWING KUNA SOLID MAJORITY BEHIND HIM!.....CHAPA KAZI NDG. SHY.....HAKI ITASHINDA NA DHULUMA ITASHINDWA!!!!
 
Haka nako ni kamchezo kakuigiza.
We Shy unauwezo wa kuandika, na mahali pa kuandikia; kitu gani kilikufanya usiandike pindi ulipotoka huko ulikotekewa?
usiseme uliogopa; kwani nini kimekusababisha leo uiandike hiyo story?
Gimme a break!
 
FD,na wewe umekaa kimya muda wote huo baada ya kutokea kwa hilo suala husemi, mpaka yamemkuta shy amesema na wewe ndiyo unaleta ya kwako. Hongera kwa kumtaja jina live huyo mhusika hapa ubaoni kama kawa at JF we dare to talk openly. Kama wameaanza mchezo huo inabidi watuzimishe wote wanaJF,is difficult to win Guerilla war. How can you target all JF members all them together? Hapa we speak freely. Shy tunaomba majina yao tafadhali? na vituo ambazo vimekuwa vikitumika kuwashikilia SHY na FD
 
this guy is actually funny! yaani ana kipaji cha kutunga, lakini ame lack kitu kimoja, stori haina maelezo yenye kujitosheleza inaacha maswali mengi ambayo ni kazi ya mtunzi kuyajibu, mie si critic mzuri sana wa mambo ya utunzi wa hadithi lakini ni rahisi kwa mtu yoyote kuona mapungufu hayo, jamani lakini if the story iz true, well, pole sana, kama wakikujia tena hao majamaa i hope u find courage ya kuwaanika hadharani ili lolote likikutokea cye tujue who to hold responsible for that.
 
Hii story inaharufu kali ya kutungwa tungwa na ni ya kusadikika. Upewe taabu zote hizo si mara moja na una watu tena wanajeshi wanaoweza kuja kukutowa kiubabe halafu ushindwe kuweka wazi ni wapi na nani na lini ulifanyiwa hivyo? Yona Maro sasa naona unakatatizo hapo.
 
Kwanza nitaenda pale wizara ya mambo ya ndani leo jioni kuona kinachoendelea ndio nitaweza kusema jina la mmoja wao ila ni Dokta
 
Kwanza nitaenda pale wizara ya mambo ya ndani leo jioni kuona kinachoendelea ndio nitaweza kusema jina la mmoja wao ila ni Dokta

Shy please,

spare us pain!
wengine hapa tunalia kwa kilichotokea na wewe unaleta jokes hapa! tafadhali sana acha hili maana kilichotokea ni very serious na kinatuumiza wengine hapa!
 
Mi sisemi sana kinachotakiwa ni ku kaza kudu kusudi waumbuke siku zote ukweli una uma.
 
Shy,

So there was the Kimara home incident and this one with the "police"? Or is it the same one?
 
Definitely possible!
May be the guy is hiding something! Or is he selling Jf to them?

Huyu Shy is a joke hapa na anajaribu kupoteza mwelekeo hapa wa jambo ambalo ni very serious na ambalo linahusisha maisha ya wana JF ambayo yako hatarini sasa hivi!

Achaneni naye kwa sasa!
 
Huyu Shy is a joke hapa na anajaribu kupoteza mwelekeo hapa wa jambo ambalo ni very serious na ambalo linahusisha maisha ya wana JF ambayo yako hatarini sasa hivi!

Achaneni naye kwa sasa!

heeeeeeeeeeee heeeeeeeeeeee nacheka uchungu

huyu shy kweli shy sawa baba unanikumbusha hadithi ya jamaa alipooona kuna msiba watu wanalia na yy akaamua kulia na kutengeneza dili alipoulizwa mbona unalia sana nasema mshkaji wake huyu aliekufa alikuwa akimdai, jamaa walishangaa maana mtu wenyewe ni mtoto wa miezi michache tu
 
I am shaken na jambo la Shy . Hakuwataja siku zote na leo kaamua kuandika . He went far a little deep kasema mmoja wapo ni Dr.Je haogopi tena kutishiwa na kukamatwa weekend hii ?
 
Back
Top Bottom