Umebaini tofauti gani Uwanja wa Mkapa na Uwanja wa Samia unaotarajiwa kujengwa Arusha?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya #Tanzania na #China, mpango uliopo mezani ni mchakato wa ujenzi wa uwanja mwingine wa kisasa ambao Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo imesema itawasilisha mapendekezo uitwe Uwanja wa Samia Suluhu Hassan.

Pia, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nayo ilieleza mipango iliyopo ni kuwa Uwanja wa Samia ukamilike kabla ya Mwaka 2027 ili utumike kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Uwanja wa Mkapa
Mkoa: Dar es Salaam
Idadi ya siti: 60,000
Ulizinduliwa: Mwaka 2007
Gharama za Ujenzi: Dola Milioni 56 (Tsh. Bilioni 64 wakati huo)
Umiliki: Serikali ya Tanzania
Mkandarasi: Beijing Construction Engineering Group (BCEG)

Uwanja wa Samia
Mkoa: Arusha
Idadi ya Siti: 30,000
Kuzinduliwa: Kati ya Mwaka 2025 hadi 2027
Gharama za Ujenzi: Dola Milioni 112 (Tsh Bilioni 286) kabla ya kodi
Umiliki: Serikali ya Tanzania
Mkandarasi: China Railway Construction Engineering Group (CRCEG)

Snapinsta.app_434050298_372680895676540_9068932460512879115_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434062024_951928449778632_4170277385847892644_n_1080.jpg

Muonekano wa Uwanja wa Samia unavyotarajiwa

Mkapa.jpg

Uwanja wa Mkapa​
 
Hii nchi wajinga ni wengi sana. Yani kabisa mtu unalinganisha gharama za miaka 17 iliyopita na leo hii?
Mfano mdogo, mfuko mmoja wa cement mwaka 2007 ulikuwa bei gani na leo hii ni bei gani? Kibarua atakayepewa kazi pale atalipwa sawa na 2007? Hapo hatujaongelea skilled labor.

Wakati mwingine ni vyema kutumia akili kabla ya kupinga kila kitu.
 
Yani kabisa mtu unalinganisha gharama za miaka 17 iliyopita na leo hii?
Mfano mdogo, mfuko mmoja wa cement mwaka 2007 ulikuwa bei gani na leo hii ni bei gani? Kibarua atakayepewa kazi pale atalipwa sawa na 2007? Hapo hatujaongelea skilled labor.
NAKAZIA

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hii nchi wajinga ni wengi sana. Yani kabisa mtu unalinganisha gharama za miaka 17 iliyopita na leo hii?
Mfano mdogo, mfuko mmoja wa cement mwaka 2007 ulikuwa bei gani na leo hii ni bei gani? Kibarua atakayepewa kazi pale atalipwa sawa na 2007? Hapo hatujaongelea skilled labor.

Wakati mwingine ni vyema kutumia akili kabla ya kupinga kila kitu.
Bei katika dola za kimarekani imeongezeka kwa kama 50%, yaani iwapo uwanja wa Mkapa ukiwa prorated kwe bei za leo basi thamani yake itakuwa $84M ambayo bado ni ndogo sana kulingana na huo wa Arusha ukizingantia na ukubwa wa uwanja wenyewe.
 
Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya #Tanzania na #China, mpango uliopo mezani ni mchakato wa ujenzi wa uwanja mwingine wa kisasa ambao Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo imesema itawasilisha mapendekezo uitwe Uwanja wa Samia Suluhu Hassan.

Pia, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nayo ilieleza mipango iliyopo ni kuwa Uwanja wa Samia ukamilike kabla ya Mwaka 2027 ili utumike kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Uwanja wa Mkapa
Mkoa: Dar es Salaam
Idadi ya siti: 60,000
Ulizinduliwa: Mwaka 2007
Gharama za Ujenzi: Dola Milioni 56 (Tsh. Bilioni 64 wakati huo)
Umiliki: Serikali ya Tanzania
Mkandarasi: Beijing Construction Engineering Group (BCEG)

Uwanja wa Samia
Mkoa: Arusha
Idadi ya Siti: 30,000
Kuzinduliwa: Kati ya Mwaka 2025 hadi 2027
Gharama za Ujenzi: Dola Milioni 112 (Tsh Bilioni 286) kabla ya kodi
Umiliki: Serikali ya Tanzania
Mkandarasi: China Railway Construction Engineering Group (CRCEG)

View attachment 2940937
View attachment 2940938
Muonekano wa Uwanja wa Samia unavyotarajiwa

View attachment 2940941
Uwanja wa Mkapa​
Kwa kweli watuonee huruma hawa viongozi wetu raisi atufafanulie hizi tofauti maana haingii akilini
 
Mkuu uchanganuzi wako uko hauko sawa, mimi naapinga kwa kuangalia bei ya mfuko wa cementi kwa mwaka 2007 bila kuangalia factors zingine,mfukowa cementi ulikuwa sh 8000 mikoani,kwa Dar labda ni sh 5000,kwa sasa bei ya cementi kwa mikoani ni sh 23,000 kwa Dar sijui.
 
Back
Top Bottom