Naibu Waziri Michezo, Mwana FA adai Uwanja wa Arusha utachukua watu 30K kwa sababu Kwa Mkapa unaochukua watu 60K kwenye mkoa wa watu wengi haujazwi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Naibu Waziri wa Saana, Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amedai sababu moja wapo ya kujenga Uwanja wa Michezo unaochukua watu 30,000 mkoani Arusha ni kuwa kwa wastani katika mechi watu hawataujaza uwanja huo ukizingatia kuwa Uwanja wa ‘Kwa Mkapa’ unaochukua watu 60,000 ukiwa katika mkoa wa Dar kwa wastani wa kujaza ni watu 7,000 kwa mechi

Amesema hayo wakati akijibu swali la mdau huko X (zamani Twitter) aliyehoji sababu ya kujenga uwanja ambao yeye anadhani ni idadi ndogo ya watu

IMG_9702.jpeg

IMG_9703.jpeg

Swali hapa linakuja, kwanini hatujaangalia miaka mingine mingi ijayo ambayo Jiji linakuwa na pia tukiwa na michuano ya Kimataifa itakuwa inafanyika Dar es Salaam tu? Katika kukuza nchi nadhani ingekuwa vema michezo hiyo kuchezwa katika mikoa mingine
 
Sijawahi kua na Imani na watu walosoma Kwa KUUNGAUNGA yaan ujanja ujanja shotkati anajikuta ana Masters !!!.

Ukweli ni kwamba , IQ hujielezea kupitia Elimu Darasa.

Kwa bahati mbaya sana , Wenye IQ ndogo wanapopata Uongozi, Huwa wanakasumba ya kubebana.
 
Mji unaweza kuwa na idadi ndogo ya watu ila mashabiki wakawa wengi wakuujaza uwanja wa watu 50k
Ni kweli kabisa hapa Naibu Waziri amejibu kisiasa. Watu wanaweza hata kutoka mikoa na nchi nyingine kuja. Mashabiki wa Yanga walisafiri kutoka hapa kwenda Rwanda kuangalia mechi yao dhidi ya Al-Merrikh SC
 
Yap
Ikijengwa arena hapo matukio mbalimbali yakiwa yanafanyika ukijumlisha na utalii na nchi za jirani tunazopakana nazo uwanja kujaa sio ttz
 
Huyu alishika nafasi ya 4 kule kwenye kura za maoni, Jiwe akafosi apitishwe!! Ona sasa madudu yake!!

Ila Wizara ya Michezo nayo, huku Ndumbaro huku Mwana FA yaani kwa kifupi “Both Teams to Score”
Hii Wizara tumepigwa na kitu kizito. Nilidhani kwa kuwa Mwana FA ni mtu wa michezo atakuwa mtu safi pale ila nimegundua ameshaingia kwenye na sasa anawaza kama waliokuwepo tu
 
Yap
Ikijengwa arena hapo matukio mbalimbali yakiwa yanafanyika ukijumlisha na utalii na nchi za jirani tunazopakana nazo uwanja kujaa sio ttz
Mambo mengi sana yangeweza kufanyika hapo. Hii ni kama wamejiwekea njia ya ulaji wa baadaye, utakuja kusikia baada ya miaka mitano wanafanya ukarabati mkubwa wa kuongeza uwanja
 
Simba na Yanga ndio timu pekee zinazojaza viwanja vya bongo.hata Lupaso ni mpaka hawa mazezeta wawe na mechi.
Kwa sasa ni Simba na Yanga. Vipi kwa baadaye? Acha baadaye, vipi kwa michezo ya Kimataifa kwa Klabu na Taifa? Huoni leo ukisema Taifa Stars inacheza na timu fulani Arusha faida tutazopata?
 
Mji unaweza kuwa na idadi ndogo ya watu ila mashabiki wakawa wengi wakuujaza uwanja wa watu 50k
Tukiacha siasa za kutaka kupinga,
Hapo Arusha, kwanza sio wapenz wa mpira, pili mpaka wafike uwezo wa kujaza watu 30k kwenye matukio japo 15 kwa mwaka, itakuwa ni baada ya miaka 30-40, ambapo uwanja huu utakuwa outdated hivyo kulazimika kujenga mwingine, kingine sio lazima kujenga mauwanja makubwa, chelsea uwanja wao ni wa watu 44k,
PSG 40k, city 55k
 
Kwa sasa ni Simba na Yanga. Vipi kwa baadaye? Acha baadaye, vipi kwa michezo ya Kimataifa kwa Klabu na Taifa? Huoni leo ukisema Taifa Stars inacheza na timu fulani Arusha faida tutazopata?
Yan stars hii inayochukiwa na wabongo ndio iwe na uwezo wa kujaza watu 60k,
Mara ya mwisho stars imeweka watu 10k taifa ni lini ?
 
Tukiacha siasa za kutaka kupinga,
Hapo Arusha, kwanza sio wapenz wa mpira, pili mpaka wafike uwezo wa kujaza watu 30k kwenye matukio japo 15 kwa mwaka, itakuwa ni baada ya miaka 30-40, ambapo uwanja huu utakuwa outdated hivyo kulazimika kujenga mwingine, kingine sio lazima kujenga mauwanja makubwa, chelsea uwanja wao ni wa watu 44k,
PSG 40k, city 55k
Umeongelea suala la ushabiki wa mpira kuwa chini pande hizo angalau ina make sense
Kiongozi wako amelinganisha tu idadi ya watu kati ya Dar na Arusha
 
Yan stars hii inayochukiwa na wabongo ndio iwe na uwezo wa kujaza watu 60k,
Mara ya mwisho stars imeweka watu 10k taifa ni lini ?
Umeangalia mechi ya Taifa Stars dhidi ya Morocco? Uwanja ulikuwaje? Na hiyo ni ya mwaka jana tu mwishoni
 
Umeongelea suala la ushabiki wa mpira kuwa chini pande hizo angalau ina make sense
Kiongozi wako amelinganisha tu idadi ya watu kati ya Dar na Arusha
Hata kama ushabiki upo chini sio kweli kwamba wataingia watu wa Arusha peke yake (ni kweli sio kwa mechi zote), ila ametoa sababu ambayo kwa kweli sio sababu. Iweje tunafanya vitu bila kuwaza mbele?
 
Hizo kauli zinadhihirisha huo uwanja haukutakiwa kujengwa Arusha. Ungejengwa Mbeya au Mwanza ambapo siyo tu kuna mwamko mkubwa wa mpira lakini pia kuna timu zilizopo ligi kuu ambazo zinaweza kuutumia.

Wao wanajenga uwanja wakitegemea mtalii aliyeshuka Mlima Kilimanjaro ndiyo aje uwanjani. Kwanza kwa mechi gani?

Poor Tanzania.
 
Back
Top Bottom