chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,009
- 20,684
Ni dhahiri Lissu ni mwanasiasa wa matukio, na huwa anapata nguvu panapokuwa na misuguano kati yake na viongozi wa juu. Na yeye amegundua hilo, kwamba ana thrive kisiasa katika mazingira ya ugomvi na kutukanana.
Ndio maana anaona kwamba wenzake wanapoenda katika maridhiano, ni kama "wanamchimbia kaburi" la kisiasa na anapotezwa. Kwa hiyo anayabeza na kuyakwepa.
Wanasiasa kama Mbowe, ni magwiji wa aina zote za Siasa, za mezani, na jukwaani, na mivutano. Na bado wameendelea kuwaka nyota kisiasa.
Lissu alikuwa maarufu enzi ya JPM kwa sababu kulikuwa na Siasa za ugomvi na kusutana, Sasa katika kusutana nani kama Lissu?
Alipotoka ubeleji na kuingia Tanzania mara ya kwanza, alipokewa na maelfu ya watu, barabara zikajaa watu, baada ya muda alirudi ubeleji bila kusindikizwa na yeyote, baadae akarudi Tanzania, alipokelewa na watu wawili.
Pale singida, alijaribu kuingia mitaani, watu wa Lissu wakitarajia umati mkubwa kumfuata, haikuwa hivyo, alikuwa na viongozi wanne tu wa chama chake.
Morogoro, alikuwa na umati wa kawaida kabisa, ambao unaweza kukusanywa na diwani au Abood katika ngazi ya Kata.
Je, wananchi wamechoshwa na aina ya Siasa zake? Au wamemchoka?
Katika mikutano mingi, hana hoja yoyote zaidi ya kuimba katiba, na neno likirudiwa sana, linachosha, na wananchi wanaona wakienda katika mikutano watakutana na maneno yaleyale, wanaacha kuhudhuria.
Humsikii akijadili kilimo, na sera ya chama chake kuhusu kilimo ili wananchi walinganishe, humsikii akijadili viwanda, humsikii akijadili chochote kipya.
Kwa Sasa umaarufu wa Lissu uko asilimia 25-30, asipoangalia, akina Heche wanachukua ufalme wake muda si mrefu.