Ulishawahi kutapeliwa na member wa JF? Ilikuwaje?

Mara ya mwisho kutapeliwa/kuibiwa ilikuwa mwaka 2000 Ubungo Stand ,walinipiga KANYABOYA ,nilinunua Kiwi kumbe ndani waliweka LAMI.

kudhulumiwa mara ya mwisho ilikuwa April -2024 ,nilidhulumiwa laki na elfu 10 ,kuna mtu aliniomba kisha atanirudishia mwisho wa mwezi ,sasa ni miaka miwili na nusu hajarudisha na kila siku naona naye wala hakumbushii kitu na mimi sijawahi kumuuliza ,najua kashajipunguza mwenyewe kwasababu hata akipata dharura ambayo inahitaji elfu 10 hawezi kuniomba...Na ndipo aliponifunza mambo ya kumkopesha mtu.
Hii ilete huku😂

Visa vya matapeli na watoto wa mjini | Page 24 | JamiiForums Tanzania https://share.google/8Bj2DDHPAnko1DkgW
 
Ulimpataje??
6f7ac537-73f9-4473-a9f7-560d0da892d5.jpeg
 
Nilikua sijui kama JF nayo iko na matapeli, Mimi sijawahi kutana na hiyo changamoto ila kuna watu humu hatujawahi onana live ila tumewahi kufanya mambo mawili matatu yaliyohusisha pesa na vitu zikaenda vizuri sana...

Ningepata ruhusa kwao ningewatag hapa😊...
 
Mara ya mwisho kutapeliwa/kuibiwa ilikuwa mwaka 2000 Ubungo Stand ,walinipiga KANYABOYA ,nilinunua Kiwi kumbe ndani waliweka LAMI.
Daah! Pole jamani.

Enzi hizo si wengine hata hatuna dalili kukanyaga kwenye hilo jiji. 😃

#Borntown.
kudhulumiwa mara ya mwisho ilikuwa April -2024 ,nilidhulumiwa laki na elfu 10 ,kuna mtu aliniomba kisha atanirudishia mwisho wa mwezi ,sasa ni miaka miwili na nusu hajarudisha na kila siku naona naye wala hakumbushii kitu na mimi sijawahi kumuuliza ,najua kashajipunguza mwenyewe kwasababu hata akipata dharura ambayo inahitaji elfu 10 hawezi kuniomba...Na ndipo aliponifunza mambo ya kumkopesha mtu.
Na wewe hata humgusii?
 
Back
Top Bottom