Ulishawahi kutapeliwa na member wa JF? Ilikuwaje?

Ulishawahi kutapeliwa na member wa JF? Ilikuwaje?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,403
Reaction score
867,063
Mojawapo ya matukio ambayo sitakaa niyasahau ni la kupigwa na mgonjwa wangu kilingeni Msata😂❗😂❗
Wallah nilipigwa kiboya Sana!
Yule mwana sijui alipata wapi namba yangu ila akasema anatokea Shinyanga na angependa kufika Kilingeni Msata kwa ajili ya tiba za kiroho

Tukawasiliana almost a week na akanitumia 30K ya shukrani hata kabla ya kufika kwenye matibabu😀🙌🏿❗
Siku ya siku akaanza safari yeye na jamaa zake wawili wanaoenda Dar kuuza madini😂❗ walikuwa na self drive Pajero intercooler🤪
Basi kesho yake mishale ya mchana siku ya Ijumaa jamaa akanipigia akaniambia wamepata breakdown maeneo ya Ubena Zomozi
Walikwepa basi wakaingia kwenye shimo, tairi, rim shockup rack end na lower arm vyote kwishney pamoja na sample guard 🙆🏿‍♂❗😀

Kwa haraka gharama ni kama 2.6M.. Hapo sasa nikaanza kutengenezwa

Jamaa akadai wao wana 1.5 hivyo niwaongezee wataweka mzigo wao bond au hata kuwatafutia wateja watanilipa na commission🤪😂❗

Na akasema nisiwape cash bali kama kuna mtu anayeuza vipuri niwaunganishe naye halafu vipuri viletwe Msata na gari wataivuta mpaka Msata kila kitu kifanyikie hapo🤣🙌🏿❗

Nikaingia mkenge nikampigia jamaa yangu Ilala wa vipuri akasema atapata vyote kwa 2.2M

Nikamrudia jamaa nikampa na namba ya mwanangu ilala nikaendelea kuagua wagonjwa wangu😂❗

Jamaa baada kama ya dakika 20 akanirudia.. Kwanza akanishukuru Sana kwa kumuunganisha na mtu sahihi.. Changamoto wao wakawa hawana pesa kwenye simu hivyo nilipe advance 1M kisha vifaa viletwe, by then noo watakuwa wamefika❗

Halafu baada kama ya dakika tano nikapigiwa na namba ngeni.. Nikasalimiwa kwa heshima sana na kuombwa hiyo advance ya vipuri nitume kwenye namba hiyo kuna gari inaenda Moro itaenda navyo😀❗

Sikuwa makini na ubize wangu nikatuma hela! Nikamtumia msg mgonjwa wangu tapeli na akanishukuru kwa wema wangu mkuu🤣🙌🏿😂❗

Masaa mawili baadae mwanangu wa vipuri ananipia kuwa anataka kufunga mapema hivyo kama biashara ipo nifanye haraka🤣🤣🤣❗

Sikutaka hata kujihoji zaidi nikajua tu hapa tayari❗❗❗Nikampigia mgonjwa wangu hola! Namba haipatikani

Kumweleza mwana scenario mpaka nikatuma 1M akaishia kunipa pole kubwa😃❗
Mganga kapigwa mchana kweupe siku ya ijumaa weekend loading.❗❗❗
 
Kuna jamaa alitukatia mimi na mdogo wangu nje ya basi ambalo lilikuwa linakaribia kuondoka engine inaunguruma kuashiria linaondoka muda wowote pale msamvu .. Baada ya kupewa hela akaingia ndani ya basi akasema hili limejaa twendeni tuangalie basi lingine. Jamaa akatusaidia kubeba mzigo tukaanza kuelekea kwenye basi alilotuambia. Aisee kulikuwa na msongamano wa mabasi jamaa alikula kona fasta fasta akapotea. Katika kumtafuta tukauona mzigo wetu ukiwa kwenye mlango wa basi moja hivi kwenda kucheck hilo basi mlango ulikuwa wazi ila ndani hakuna mtu. Mzigo aliuacha atukimbie kiurahisi au kwa sababu lilikuwa ni furushi la viazi? 😅😅
 
Kuna jamaa alitukatia mimi na mdogo wangu nje ya basi ambalo lilikuwa linakaribia kuondoka engine inaunguruma kuashiria linaondoka muda wowote pale msamvu .. Baada ya kupewa hela akaingia ndani ya basi akasema hili limejaa twendeni tuangalie basi lingine. Jamaa akatusaidia kubeba mzigo tukaanza kuelekea kwenye basi alilotuambia. Aisee kulikuwa na msongamano wa mabasi jamaa alikula kona fasta fasta akapotea. Katika kumtafuta tukauona mzigo wetu ukiwa kwenye mlango wa basi moja hivi kwenda kucheck hilo basi mlango ulikuwa ila ndani hakuna mtu. Mzigo aliuacha atukimbie kiurahisi au kwa sababu lilikuwa ni furushi la viazi? 😅😅
Huyo jamaa ni member wa JF ??
 
Umetapeliwa kijinga 😹
 
Kaka ulimpataje, na ulijilipaje nichukue mbinu kaka
9fd85eab-8a71-4ecb-8cd6-354f2acdfaa7.jpeg
 
Back
Top Bottom