ITS MASIHARA AGAIN
View attachment 1473714
Kuna dada mmoja anauza duka la samaki, kwa kuwa naendaga kununua akachukua namba ili siku wakileta pweza anijuze
Akawa anatuma tuma whatsapp status mara kwa mara, mara anatuma picha zake mara maneno ya kwenye kanga siku akigombana na nani huko sijui.
Kuna siku akatuma picha yake nzuri, mi nikachukua muda wangu nika creat video nikamtumia, akafurahi kishenzi.
Juzi tena akatuma picha nyingine, mi nikajifanya tena producer kama Ramar, nikatia soundtrack, vocal, animation na mazaga kibao yakisindikizwa na wimbo mzuri wa mzee wangu Zahir Zorro akiwa na bendi ya mass media kitu beatrice. Maana kinavyoanza tu" nipe nafasi niwe mpangaji wa kudumu ndani ya moyo wako, moyo thabiti uliojaa mapenzi sawa sawa na yangu..." nikamtumia mtoto akafurahi kinoma. Akaomba nimfundishe ku creat video
Mi sikuwa na hiyana kama Kagere tu akivutwa kati kati ya uwanja anadondokea ndani ya box la penati. Nikamwambia njoo nikufundishe.
Akasema ooh mi naogopa kuja huko nifundishe hapa kwa sms.
Nikamwambia huwezi kuelewa mpaka uje .
Aksema mi naogopa yatatoke mambo ya batari nikija huko.
Nikamuuliza kwa umri huo unaogopa nini. Akasema ooh mie bado mtoto
Alivyotoa jibu hilo tu nikachekelea kama nimeshinda m 50 za biko. Nikamwambia basi huna haja ya kuogopa kwani mi mtoto mwenzio hakuna kitakocho haribika.
Akasema haaaaaa. Nikamwambia watoto kazi yao kunyonya na kucheza mchezo wa kombolelea. Akuliza kunyonyo nini?
Nikamwimbia kwa kuwa mama yetu kasafiri itabidi tunyonye chupa za nyonyo.
Akacheka sana sana
Leo asubuhi nilivyoamka nikaenda kununua chupa zile za kunyonyea watoto nikapiga picha nikamtumia tiyari nimeshazinunua mtoto mwenzangu.
Akasema ntakuja kuzikagua jioni.
Jioni baada ya kufunga duka kaja, hakukuwa na zaidi kama Yanga na KMc tu. Mpaka sasa hivi nimesahau ilibidi nimfundishe nini sijui, anaekumbuka somo alojia kujifunza huyu binti ani pm kesho asubuhi maana saa hizi nalala baada ya kumsindikiza kwao
YADUMU MASIHARA